hugochavez
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,907
- 1,009
Taarifa za uhakika zilizopatikana kutoka ndani ya kambi haramu ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida ya kupindisha maamuzi yaliyofanyika miaka mingi iliyopita kuwa makao makuu yajengwe katika kijiji cha Ilongero wao wakayapeleka kwenye hifadhi ya msitu wa Sagarumba, hatimaye jana mkuu wa mkoa wa singida eng.Mtigumwe kubatilisha maamuzi hayo ya kijuha na kuyarudisha Ilongero.....
Mwenyekiti huyo ambaye elimu yake ni darasa la saba hivi sasa anahaha kutaka kupinga maamuzi ya mkoa eti akate rufaa kwa rais kuwa amedharauliwa..anasahau kuwa yeye alipindua maamuzi halali ya mwaka 2006 na kilichokuwa kinasubiriwa ni kuhamia tu.
nyuma ya mwenyekiti huyo ambaye hana elimu wapo wapambe wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya Narumba Hanje, mhandisi Ikungu nk ambao wamehodhi maeneo makubwa jirani na eneo la sagarumba hivyo wanajiona wamepokwa tonge mdomoni.
mkuu wa mkoa wananchi tupo nyuma yako, usitetereke. hao ni waganga njaa.