Vibanda vyateketea kwa Moto Iringa

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Habari zilizonifikia sasa hivi ni kwamba vibanda zaidi ya hamsini vimeteketea kabisa kwa moto katika Stendi ya Iringa. Vibanda hivyo ambavyo vilijengwa kuzunguka Stendi kuu ya Iringa vilijumuisha pia na Ofisi za kukatia tiketi za baadhi ya Mabasi yaendayo mikoa mingine hususani Dar es salaam!

Moto huo ambao ulianza usiku wa manane kuamkia leo, mpaka sasa chanzo chake hakijajulikana,ingawa unasadikiwa kuanzia kwenye banda la mama ntilie ambaye alikuwa amebandika sufuria la maharage usiku kucha ili asubuhi yatumike kwa ajili ya kifungua kinywa

Habari za uhakika zinadokeza kwamba Gari pekee la zimamoto la Mji wa Iringa lilifika Eneo la tukio lakini kwa maastaajabu ya wengi bila maji, na baadaye liliporudi na maji lilirudi na maji nusu ya tenki ambayo hayakukawia kuisha wakati moto kwa kusaidiwa na upepo mkali unaoendelea kuvuma katika mji wa Iringa ukishika kasi

Eneo hilo ambalo linamilikiwa na Halmashauri ya Iringa Vijijini linatarajiwa kujengwa jengo kubwa la Ghorofa na tayari Mwanasheria wa Halmashairu hiyo amezuia waliounguliwa kuvijenga upya vibanda vyao
 
Kigarama,

Tatizo ni watu wa zima moto mchekea, yaani hawawajibiki, hebu kweli gari la zima moto laweza kuishiwa maji? lakini pia serikali yetu pia haiwawajibishi hata kama hawajawajibika vema hawa watumishi ktk sekta hiyo, ama wewe unasemaje, na kibaya zaidi wale wajaliamali (wamiliki wa vibanda) huenda walichukua mikopo, sijui wataanza vipi maskini.
 
Back
Top Bottom