Vibanda vya wamachinga juu ya mitaro barabarani ndio chanzo cha harufu mbaya Dar es Salaam

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
5,266
2,000
Jana mchana wakati nimetoka kanisani Pugu Kajiungeni (Njia panda ya Chanika na Kisarawe ) niliamua nikapate viepe na kuku kwa muuza chips aliyeko kando ya barabara.

Nimefika pale nilishangaa yule kijana muuza chips anawezaje kukaa pale angalau kwa nusu saa. Yaani kijana yule pale ndipo maskani yake mahali ambapo wateja wake hula viepe pale.

Ule mtaro ukiuchungulia kwa chini utakutana na uchafu mwingi, sijui ni kinyesi au maozo ya chakula.
Pale hata bure siwezi kula chips.

Hivi kuna mtu ana akili timamu anaweza kula mahali pachafu vile?

Leo nikaamua kufanya survey kukagua mitaro iliyofunikwa na vibanda vya wamachinga.

Kwakweli hali ni mbaya.

Wamachinga waondolewe kwenye mitaro. Huu sio upendo bali ni ushamba.

Afya ni dili, ukiiharibu kwa siku 30 utaijenga kwa siku 60 au zaidi.
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,872
2,000
Ikitokea wamachinga wakaondolewa barabarani halafu Lissu akatua nchini ccm watafurushwa ikulu kwa siku moja.
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,949
2,000
Machinga,bodaboda na mama ntilie wamekua ajenda kubwa KWA wanasiasa,kila mtu anamvizia mwenzie ateleze Ili ajibebee maujiko na wafuasi uchwara. Si CCM, CHADEMA, CUF wala act ni wote wanawatamani na kuoneana wivu kwa Hawa wamachinga
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,947
2,000
Machinga,bodaboda na mama ntilie wamekua ajenda kubwa KWA wanasiasa,kila mtu anamvizia mwenzie ateleze Ili ajibebee maujiko na wafuasi uchwara.
Si CCM, CHADEMA, CUF wala act ni wote wanawatamani na kuoneana wivu kwa Hawa wamachinga
Ndiyo ubaya wa Demokrasia. Watu wengi au wenye sauti wanaweza pitisha jambo lao hata kama si sawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom