Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Rais hawezi kuwafurahisha wafanya biashara wakubwa na wadogo kwa wakati mmoja.

Kariakoo imedorora kibiashara na chanzo ni hizi biashara ndogo za pembeni ya Maduka makubwa.

Itabidi tu hawa wadogo warudi kwenye maeneo yao maalum.
 
Rais hawezi kuwafurahisha wafanya biashara wakubwa na wadogo kwa wakati mmoja.

Kariakoo imedorora kibiashara na chanzo ni hizi biashara ndogo za pembeni ya Maduka makubwa.

Itabidi tu hawa wadogo warudi kwenye maeneo yao maalum.
Maeneo maalum yapi hayo?? Hii changamoto ya wamachinga ni suala la kujua wao wanataka nini!?? Nature ya biashara ya umachinga ni maeneo tu au kuna factors nyingine zinasababisha machinga kuweka kibanda chake sehemu fulani..

Wale wamachinga huwa hawaweki tu vibanda vyao kwa kukurupuka??
 
Hili ninaliunga mkono kwa asilimia 100. Yaani Barabara zote walifanya kuwa vichochoro. Walikuwa untouchables wa mwendazake. Cheap popularity. Kukawa kama jalala. Wenye kulipa kodi hawauzi kabisa. Warudi walikojengewa/tengewa halafu wakakimbia huko. Na Ile pesa ya kitambulisho ya 20,000 ndiyo iliwapa kiburi. Eti wasiguswe.
 
Inahitaji jicho la tatu kuliona hili.
Kwanini nchi imejaa wamachinga wengi kuliko wanaofanya biashara rasmi madukani?!

Ukiishajibu hilo,twende kwenye conclusion,je Tanzania ni nchi yenye wamachinga zaidi au wafanyabiashara rasmi zaidi?

Je,tunataka nchi ya wamachinga au wafanyabiashara rasmi?

Tuna mikakati gani kutomuua au kutompoteza mmachinga na badala yake kumgeuza kuwa mfanyabiashara rasmi?!

Kiwango cha elimu,maarifa,mipango ya maendeleo ya jamii na uchumi katika taifa hili na utekelezaji wake kinatengeneza workforce ya aina gani,skilled au unskilled?!

Aina hiyo ya workforce ina mchango gani kutengeneza machinga au mfanyabiashara rasmi?!

Tuna workforce ya aina gani sasa(majority),tunataka workforce ya aina gani baadae na tunaipataje bila kuathiri uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja?!(smooth transition)?

Haya ni mambo ya kuzingatia.

Tusiingize migambo mitaani na kujifanya sisi ni wamarekani tuliosheheni mabilionea watakaoweza kuinvest,tukavunjavunja ALL THAT WE HAVE tukijivunia kuleta kitu ambacho ni priviledge kwa mhindi,mnaijeria,mkenya,mzungu etc na wale unawaona kero kumbe ndio workforce yako pekee uliyo nayo ambayo unapaswa kuilea kama yai.

Tukifukuza machinga,je,hawa machinga kuna siku tutawakuta wanamiliki maduka wao,au watanzania wenzao?!au tutakutana na wageni wakimiliki njia za uchumi za nchi?!
Suala la machinga ni pana na kiashiria cha tatizo kubwa la nchi kuliko tunavyowaza short sighted.

Tuweke siasa za magufuli-Samia,ccm-chadema kando,tusiwe blinded na ego.

Tuwaze kama watanzania,ni kama mzazi mwenye mtoto mtukutu nyumbani,jambo la kwanza unawaza kumbadili awe mwema,na sio kumtimua.

Tusizungumze kama tunaongelea aliens from another country,planet etc.
Tunazungumzia vijana wa kitanzania,wanaotumia nafasi finyu ya uwekezaji kujikwamua kiuchumi.

Tunazungumzia baba na mama wa wale watoto unaokutana nao kituoni wamevaa uniforms wanakwenda shule!

Angalia upande wa pili wa shilingi.Huko ndiko nchi iliko,ndiko vijana wenu wengi waliko,ni machinga barabarani,machinga maofisini.

Ubinafsi usikufanye uwe blind.

Nina biashara zangu rasmi nalipa kodi nyingi za serikali hapa mjini,na sijawahi kumchukia machinga asiye na duka kama mimi hata siku moja.It pains me kuona mnazungumzia mambo ya kutimua binadamu anayejitafutia riziki kirahisi tu!Yaani mnaona rahisi tu mambo haya ya uwekezaji na uchumi mtu kahangaika wee hadi kaweka banda lake,timua hao!You guys?!😡😡

I expect mtandao kama huu uwe na mawazo critical zaidi,yasiyopatikana kirahisi.

Wajengeeni maeneo yao,warasimisheni kazi zao,wapeni financial support,waelimisheni watanzania waweze kuwa competitive na mataifa mengine then watahama tu bila vurugu kuja mnakokutaka.

Wekeni na simamieni mipango miji kila mtu anayetaka kufanya lolote ajue anafanyia wapi na vipi,na taratibu zikoje,na ziwe condusive kwake,sio alimradi tu.
 
NASHAURI KILA MANISPAA ITENGE MAENEO YA HAWA WATU, WAJENGE COMPLEX ZAO.
Tatizo la hizo complex ni urasimu unafanyika, unakuta wakati complex inajengwa watumishi wa halmashauri au wafanyabiashara wakubwa wanagawana fremu, Complex ikiisha wao ndo wanawapangisha au kuwauzia wafanyabiashara wadogo kwa bei kubwa, hayo ndo yalifanyika Machinga Complex hadi leo hazina watu.
 
karibu mikoa yote Arusha je? utalia
Arusha wataenda lini kweli? Kamji kenyewe kadogooo hapo hapo mabanda machafu yametaradadi kama yote!! Waondoke bana! Pale friends corner hawajaacha hata ka njia ka watembea kwa miguu,wamejaza ma bamia na ngogwe+ maparachichi kila mahali,waondoke sasa,imetosha!
 
Arusha wataenda lini kweli? Kamji kenyewe kadogooo hapo hapo mabanda machafu yametaradadi kama yote!! Waondoke bana! Pale friends corner hawajaacha hata ka njia ka watembea kwa miguu,wamejaza ma bamia na ngogwe+ maparachichi kila mahali,waondoke sasa,imetosha!
Mkuu, wakale wapi aisee, mbona kama unachuki nao Sana mkuu
 
Swala la machinga waondoke tu mjini wanaua biashara watengewe maeneo yao Magufuli alibugi sana


Kwanza hawalipi kodi na wanaponunua bidhaa hawaombi risiti kwenye maduka makubwa so serikali inapata hasara ya kodi.

Vile vile wengi mjini ni wafanya biashara wakubwa wanafanya kutoa pesa kwenye mfuko wa suluali na kuweka kwenye mfuko wa shati.


Ndio maana ukwepaji kodi unaongezeka kwa sababu watu wenye address za kulipa kodi biashara zao wanachukua machinga.

Halafu machinga wenyewe wanauza sana halafu hawana leseni za biashara za kufanyia kazi wengine unakuta ndio wale waliofunga maduka kipindi cha Magufuli unakuta machinga ameweka bidhaa za milio 10 nje hii sio haki hata kidogo.

Watafutiwe maeneo maalumu kama Tandika tegeta, Ubungo mbagala wawe na shopping mail zao na walipe kodi ili tuone kama watauza tens bidhaa ovyo na kuhatarisha hata maisha ya wanunuzi.

Unakuta mtu anauza nyanya kariakoo katikati ya barabara seriously sehemu ambayo mnasema ni soko la kimataifa.?
Swala ni mnyama au maombi kidini. Neno ni suala
 
Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es Salaam.

Ni sahihi kabisa wakafanye hivyo na pale stand ya JPM Mbezi ni kero.....yaani ukitaka kupanda gari za Moro hasa Abood mlango wa gari ulipo hapohapo kuna machinga kapanga bidhaa zake ni kero tupu, pia vituo vingi vya daladala vimegeuka masoko
 
Back
Top Bottom