Vibaka Walimvua Viatu na Kumwibia Pesa Marehemu Semhando

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Vibaka wasio na utu hawakujaribu kunusuru maisha ya Abuu Semhando alipogongwa na gari, badala yake walimvua viatu na kumuibia simu na pesa zote alizokuwa nazo kwa wakati huo.
Wapenzi wa muziki wa dansi hapa nchini wameendelea kupatwa na simanzi kubwa na ya aina yake baada ya kupatwa na misiba miwili mikubwa ya kuondokewa na wakongwe wa muziki wa dansi, Dokta Remmy Ongala na Abuu Semhando.

Siku ya jumapili ya tarehe 12 mwezi huu wapenzi wa muziki wa dansi nchini waliondokewa na gwiji la muziki wa dansi DK.Remmy Ongala ambaye alikuwa akisumbuliwa na Kisukari.

Kabla ya hata kusahau wala hata kumalizika kwa msiba huo ijumaa usiku wa kuamkia jumamosi wapenzi hao tena walipatwa na simanzi kubwa tena ya kuondokewa ghafla na kipenzi chao mkongwe mwingine wa muziki wa Dansi ambaya alikuwa mashuhuri kwa upigaji wa dramu katika bendi yake ya Twanga Pepeta African Stars.

Semhando alikutwa na umauti huo juzi usiku wa saa kumi akiwa ametokea katika onyesho lao la bendi ya Twanga lililokuwa likifanyika katika ukumbi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Wakati wakiwa wamemaliza onyesho hilo wanamuziki wote walipanda katika basi lao ambalo ndilo huwa wanatumia na yeye Abuu Semhando ambaye alikuwa ni meneja wa Bendi hiyo yeye alitumia usafiri wake wa pikipiki akiwa katika usafiri huo eneo la Tangi bovu gari lilimgonga kwa nyuma kiasi cha yeye kuanguka chini na gari tatu zilizokuwa nyuma ya gari lililomgonga zilimpondaponda na kufariki papo hapo.

Katika ajali hiyo Semhando aliibiwa kila kitu zikiwemo pesa za shoo yote, ikiwemo simu na viatu alivyokuwa amevaa.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa jana asubuhi kuelekea Muheza Tanga nyumbani kwao alikozaliwa na shughuli zote za mazishi zilisimamiwa na Kampuni ya ASET ambayo alikuwa akifanya kazi.

Ali Choki, mbunge wa Kinondoni Idd Azzan Zungu na mbunge wa Korogwe, Steven Ngonyani aka Profesa Maji Marefu ni miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi yake.

Kabla ya kifo chake, Semhando aliomba likizo ya mwezi mmoja Twanga Pepeta ili aweze kumuoza binti yake wa kwanza ambaye harusi yake ilipangwa kufanyika jumamosi ambayo usiku wa kumkia siku hiyo Semhando aligongwa na gari na kufariki dunia.

Abuu Semhando alizaliwa mwaka 1953 mwezi wa pili tarehe 20 na alijiunga na muziki kwa mara ya kwanza mwaka 1974 katika bendi ya Solar TV Band na amewahi kufanya kazi kwenye bendi za Super Matimila Band iliyokuwa inamilikiwa na Marehemu DK Remmy Ongala, Toma Toma, Tanza music, Safari Sound, Vijana Jazz ,Diamond Sound, Beta Music na baadaye alijiunga na Twanga Pepeta African Stars.

Semhando ameacha mjane na watoto 12.

Twanga Pepeta imetangaza kuwa itasimamisha shoo zake kwa siku mbili ili kuombeleza kifo chake.

Mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu Abuu Semhando
 
Daah!kweli watu wana roho mbaya.yani mwenzao anakufa wao wanaona ulaji.dawa yao moto tu...R.I.P SEMHANDO
 
Inasikitisha. yaani ni kwamba alifariki usiku wa kuamkia siku ya harusi ya binti yake? Pole sana Binti na RIP Abuu Semhando Babaa Diana!
 
Inasikitisha mno. yaani ni kwamba alifariki usiku wa kuamkia siku ya harusi ya binti yake? Pole sana Binti na RIP Abuu Semhando Babaa Diana!
 
images

MUNGU AKUPUMZISHE KWA AMANI
 
Ulitaka ndugu waje kuuana navyo si bora katoa sadaka hata ahera anaesabiwa heri
 
MIMI NILIVYOKUWA NAMSIKIA KWENYE NYIMBO SIKUTEGEMEA KWA CHEO CHAKE AWE ANATUMIA USAFIRI WA PIKIPIKI-
R.I.P Abuu Semhando-
"Good men must die, but death cannot kill their names"
 
Kama kawaida yao ikitokea ajali kitu cha kwanza wanachothamini ni ulichonacho kwanza hata kabla ya kuokoa maisha yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom