Vibahasha vya khaki vinavyozuia harakati na kuua ndoto za vijana

Kamanda Mawazo ana maono mazuri sana. Pasco kaamka nusunusu akiamka jumla hata vijijini atafanya kazi tena kwa mshiko mzuri tu. Lakini kuamka peke yako ktk nchi hii haitaleta badiliko lolote. Ndio sababu hata vyama vilivyoko sasa havijaamka inavyotakiwa kwani hakuna chama ambacho kimeweza kuaminisha wananchi wote kwa ujumla kuwa tukipita njia hii tutavuna maziwa na asali!.
Mkuu Pembe, nimeamka kamili ila naendelea kubaki kitandani huku nimefunga macho ukidhani nimelala!.
Pasco.
 
Pasco anatetea bahasha au anapinga?haeleweki!Kamanda anazungumzia bahasha na sio pesa halali.mbona wewe unataka kumaanisha bahasha ni haki yako
Mkuu Boban, ni kweli natetea bahasha za halali kama logistic halali kwa waandishi wa habari ambayo ni haki yao!. Hadi Ikulu wanalipa, Chadema wanalipa na yeyeto mwenye kuhitaji mwandishi amuandike, itambidi kulipa!.
Kanisome hapa labda utanielewa [h=3]Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni Rushwa!.[/h]Pasco
 
E bwana huyu ni Pasco? Aisee unatisha inamaaana Lowassa ampe mtu bahasha halafu huyo mtu akamwandike vbaya? Kwani hizo habari hawaziuzi wapate hela za kujikim duu bongo ni zaid ya uijuavyo
Mkuu Kitali, zile bahasha sio malipo ya kuandika habari, bali ni kusupport tuu upande wa logistic!, japo umentaja El usifikiri anaandikwa vizuri kwa sababu hiyo, bali the guy is real good ndio maana hana kibaya cha kuandikwa!, wanaomsema vibaya humu ni chuki zao tuu na uoga wao wa 2015!.
Pasco
 
Lkn waTZ hebu tumuogope mungu kwa sababu ni kweli km hasa vijna ndio wenye nguvu ya kulikomboa taifa lilipofika je kuna haja gani ya kufanya kazi ya kidhalimu kwa ajili tu upate bahasha ya khaki? mbona ni udhalilishwaji wa hali ya juu sana km kijana? hivi km tunadhamira ya dhati juu ya nchi yetu kunahaja gani ya kijna kurubuniwa eti jiunge chama fulani maarufu ili upate ajira!!! je ni ajira gani km c kusugua benchi ktk maofisi ya wakubwa kwa kutafuta udaku ili kuweka ktk vyombo vya habari kwa kumsifia mtu kinyume na astahilivyo? au kijana unakubali kubebwa ktk gari na kupelekwa ktk sherehe ya chama ili kujaza watu wengi na hapo unajua fika kabisa chama hicho ni kichafu? au unakuta kijana kachoka na anakwambia mi bora nipate kazi tu huko hata km amechafuka. Ukombozi wa nchi hii upo kwa vijana na kuamua kwao wazee wa nchi hii hawana nafasi kabisa. Tubadilike vijana na tukatae kuahidiwa ajira wakati tulishuhudia watu elf 15 pale uwanja wa taifa wakipigana kwa nafasi 75 tu, sasa hao wanaokwambia njoo upate ajira jevni kweli au njaa tu inakuponza. It is better to die for things that will live than live for things that will die.
 
pamoja na kwamba waandishi njaa wanavitumia vibahasha hivyo haramu kununulia viwanja MBAGALA , MWANDEGE NA CHAMANZI , LAKINI WANABAKI WAMEDHALILIKA SANA !
 
Ndoto kubwakubwa za wanasiasa na wanataaluma vijana zimeuawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa hata bahasha ndogo.

Kwa wanasiasa vijana wameamua kutumikishwa na wakongwe wa siasa na kazi yao kubwa ni kutumwatumwa kama vijakazi ingawa wanapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na kuitwa majina mazuri mazuri ya uongo.

Kazi yao kubwa Hawa vijana ni kutengeneza fitina na kutukana waliotumwa kuwatukana,wamekuwa kama vijibwa vidogo vidogo vinavyoamuriwa mbwekee huyu au yule bila kuhoji kwa nini.

Utavikuta Dodoma wakati wa bunge utafikiri ni madreva au mautingo wa magari, hulala kwenye hotel cheap cheap huku vikiwinda mademu kwa ajili ya mabosi wao,vina akiri lakini vimeamua kuwa Vijinga,

Kundi la pili ni la wanataaluma,wanalipwa mishahara viduchi sana mwisho wa mwezi,vinabebeshwa mizigo mizito kama punda lakini wanauwezo wa kuanzisha biashara au kufungua ofisi zao kubwa maishani na kujenga taasisi kubwa duniani.

Kama ilivyo kwa punda awekewavyo karoti mbele yake na kuburuta mzigo mzito ili aifikie karoti na akiipata huitafuna yote bila kuacha akiba kisha huwekewa nyingine tena ndivyo ilivyo kwa waajiriwa hawa na vibahasha vya mwisho wa mwezi.

Katika kundi hili la wanataaluma naumizwa zaidi na waandishi wa habari vijana ambao mchana kutwa utawaona wanavyopigwa vumbi na jua kwenye mabenchi ya ofisi za wakubwa kutafuta habari,ukweli ni kwamba hawatafuti habari bali vibahasha vya kaki vyenye elfu thelathini ili waandike sifa za uongo kwa mafisadi na walarushw hao.

Taarifa za ukweli ziko vijijini ambako kuna mateso ya kila aina,matukio ya kutisha ambayo wakiyaandika na kuyaripoti yatawakuza sana sana,shida huko hakuna bahasha ukiwaita watakuuliza bahasha..bahasha...bahasha,ndiyo maana watazeekea kwenye mabenchi ya wakubwa.Hawako tayari kusota,kutembea kwa miguu,kulala na njaa ili wakue na kutimiza ndoto Zao.
Mkuu alphoce Mawazo, na mimi ngoja nikuite kama kaka unavyotambulika humu, hivyo kamanda Alphonse Mawazo, kwanza asante kwa bandiko lako hili!,

Kuhusu vijana kwenye uzi huu umezungumzia vitu vitatu vikuu,

  1. Ndoto
  2. Taaluma, professionalism
  3. Reality, (bahasha)
  4. What is vs what ought to be
Mimi nimeguswa pale tuu ulipowazungumzia vijana waandishi wa habari kwa sababu na mimi ni mwandishi wa habari na mwanzo pia nilikuwa kijana!.

Umeanza hivi

Jee ni kweli hawa waandishi vijana walikuwa na ndoto kubwa kubwa?!. Ndoto gani hizo zilizouwawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa bahasha?!.

Unaumizwa na na jinsi
wanavyopigwa vumbi na jua kutafuta habari?,
wanavyoshinda kwenye mabenchi ya wakubwa bila kutafuta habari?,
wananavyotafuta vibahasha vya khaki vyenye elfu 30?
wanavyoandika sifa za uongo za mafisadi na wala rushwa hao?.

Kumbe taarifa za ukweli ni zile tuu zilizoko vijijini?!, ndio maana wanaandika sifa za uongo?!, ila pia umetoa sababu za wao kutokwenda vijijini

Msingi halali wa bahasha za waandishi ni kuwezesha kutimiza makumu yao kikamilifu, na haswa logistics, mimi naziita hizi ni bahasha halali za uwezeshaji!, waandishi kama taaluma nyingine zote, wanabidi wawezeshwe ili watimize majukumu yao kikamilifu!.

Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini, hivyo ni kweli huko vijijini ndiko kwenye habari nyingi, ila pia ili kuzifikia habari hizo huko ni lazima waandishi wawezeshwe ki logistic ili wafike huko kijijini, hakuna sababu ya waandishi kusota, kutembea kwa miguu, kulala nje, kulala njaa, akifuata story kijijini!, kama hakuna logistic za kuwafikisha waandishi vijijini, then waacheni waandishi tubanane hapa hapa mjini!.

Kwa uelewa zaidi kuhusu Waandishi na bahasha, pitia hapa
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni rushwa!

Pasco
RIP KAMANDA ALPHONSE MAWAZO!. VERY SAD!.

Pasco
 
hakika wewe ni mzalendo wa kweli , umeandika kwa uchungu sana .
.
IMG_20181114_114308.jpeg
 
Back
Top Bottom