Viazi wananunua Kariakoo, Wanatumia Manjis gas, halafu wanaviita "French Fries"!

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Hizi hotel zetu bongo zina matatizo gani?

Chakula wananunua kwenye local markets lakini unauziwa vikiwa na majina ya Kifaransa na Kingereza, ukihoji wanasema ni kwaajili ya kuvutia na kuelewesha watalii!

Hivi wewe ulipoenda China au US kama mtalii ulikuta menu zao zimeandikwa Kiswahili? Maana na wewe kule ni mtalii!

Sasa kwanini viazi walivyonunua Kariakoo waviite "French fries"?
 
Viazi ni raw mkuu.
Hiyo french fries ni aina ya chakula kimekuwa patented hivyo.
 
Nelson Richard, hata ukienda US viazi kutoka Texas vikikatwa vipande vidogo vidogo kisha vikikaangwa wanaviita "french fries".
 
Last edited by a moderator:
Jamani , kuna vitu vingine si vya kuponda tuu , ili mradi uponde .

Kuna mambo yamekaa kwenye formality yake , ww unataka kila kitu kuleta uharakati wako .

Frnch fries , ni jina lilipo kila mahali mahali , wala haina haina sababu ya kubishana hapa , cha msingi ww ukiienda , sema nataka Viazi vilivyokaangwa , si lazima useme French Fries .
 
Hizi hotel zetu bongo zina matatizo gani?

Chakula wananunua kwenye local markets lakini unauziwa vikiwa na majina ya Kifaransa na Kingereza, ukihoji wanasema ni kwaajili ya kuvutia na kuelewesha watalii!

Hivi wewe ulipoenda China au US kama mtalii ulikuta menu zao zimeandikwa Kiswahili? Maana na wewe kule ni mtalii!

Sasa kwanini viazi walivyonunua Kariakoo waviite "French fries"?
Mpendwa Nelson Richard, usipigane vita na kitu kiitwacho 'marketing techniques of branding' kwani hutoweza kuishinda maana imejaa duniani kote. Tunapouza korosho yetu india unataka baada ya kuziprocess waandike kwenye paketi 'tandahimba crunchies'? They will run out of business if they do it. Ulishahudhuria send offs? Kwa nini bibi harusi mtarajiwa anapopewa vitenge na kanga mc husema:'mabibi na mabwana vitenge hivyo mnavyoviona ni wax super toka congo' kumbe ukweli ni vitenge vya kawaida tu toka kiwanda cha mwanza/dar/arusha.
Remember: Careful branding adds value and allure to a product.Wenzetu wanalijua hilo sana na wanalifanya kwa wingi.
 
Hizi hotel zetu bongo zina matatizo gani?

Chakula wananunua kwenye local markets lakini unauziwa vikiwa na majina ya Kifaransa na Kingereza, ukihoji wanasema ni kwaajili ya kuvutia na kuelewesha watalii!

Hivi wewe ulipoenda China au US kama mtalii ulikuta menu zao zimeandikwa Kiswahili? Maana na wewe kule ni mtalii!

Sasa kwanini viazi walivyonunua Kariakoo waviite "French fries"?

Suala sio kuvutia watalii wala viazi vimepatikana wapi!! Suala ni hayo mapishi ya aina hiyo ndio yanaitwa 'French fries.'
Mkate wananunua local bakeries, minced beef pia wananunua kwenye mabucha mitaani na wanatoa kitu kinaitwa 'Burger', kilichoigwa ni mapishi...!
 
hizi hotel zetu bongo zina matatizo gani?

Chakula wananunua kwenye local markets lakini unauziwa vikiwa na majina ya kifaransa na kingereza, ukihoji wanasema ni kwaajili ya kuvutia na kuelewesha watalii!

Hivi wewe ulipoenda china au us kama mtalii ulikuta menu zao zimeandikwa kiswahili? Maana na wewe kule ni mtalii!

Sasa kwanini viazi walivyonunua kariakoo waviite "french fries"?
nawewew.nunua.manzese tumia.mengi gas ita spain.chips
 
Isiwe shida nawewe tengeneza aina ya chakula au kitafunwa kitamu, chenye kupendwa na watu wote then kitangaze kwa jina lako,
 
Back
Top Bottom