Viazi Vya Urojo Na Chana (a.Ka. Mixa au Chana Batata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viazi Vya Urojo Na Chana (a.Ka. Mixa au Chana Batata

Discussion in 'JF Chef' started by X-PASTER, May 18, 2012.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Viazi Vya Urojo Na Chana (a.Ka. Mixa au Chana Batata)

  Vipimo
  • Chana kavu ................................ 2 Magi (mugs)
  • Viazi ........................................... 8-10 Vikubwa
  • Unga wa ngano .......................... ¾ Magi
  • Kitunguu kikubwa kimoja
  • Majani ya kihindi (curry leaves)............. kiasi ( majani 15)
  • Nyanya moja
  • Mafuta ya kupikia kiasi
  • Bizari ya manjano .................................. ½ kijiko cha chai
  • Embe Mbichi kali na Ndimu au ukikosa embe unaweza tumia Ndimu peke yake
  • Chumvi ................................ kiasi
  • Pilipili ya mbuzi au ya unga (ukipenda)

  Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  • Roweka Chana nzima kavu ikiwezekana usiku mzima kisha zichemshe hadi ziwive. Chuja maji yaliyobaki ziweke kavu pembeni.
  • Tia mafuta kwenye sufuria, tia vitunguu vilivyo katwa katwa, Binzari manjano na majani ya kihindi kaanga kidogo kisha tia nyanya zikaangike kidogo. Zikisha wiva kidogo tia embe mbichi ndimu pilipili na chumvi kisha wacha ziwive.
  • Chemsha maji ya kutosha na mimina unga wa ngano na bizari ya manjano kama unavyopika uji mwepesi, koroga usigande mpaka uwive...
  • Katakata vipande vidogo vidogo vya viazi na umimine kwenye uji huo unaochemka, tia chumvi na pilipili ukipenda.
  • Koroga koroga visigande vikikaribia kuwiva mimina Chana zako ulizozichemsha kisha tia ndimu ikolee mpaka viwive.
  • Epua tayari kwa kuliwa hasa na bajia, kachori, chipsi za muhogo na chatini kama utakavyopenda.
   
 2. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona sijaelewa chana ndo nini
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ok thanks ngoja kesho nitengeneze..
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  maana yake ingia HAPA!!
   
Loading...