Fahamu namna bora ya kutengeneza Kachori

Tena ugali na samaki au mlenda

Huo mlenda sasa...ndio unapikwaje?
Alafu kuna siku kuna dada mmoja alipika sijui mboga inaitwaje ile ni majani ya mboga na karanga kama hivi....ila kwa ushamba wangu ilinishinda kula maana ladha yake sikuipenda.
 
Naombeni mnisaidie namna ya kuandaa kachori dada zangu na mama zangu.
 
Fata hii apa

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=7898449

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Aina ya 1...


Mahitaji
Viazi kg 1
Chumvi kiasi
Kitunguu saumu 1/2 teaspoon
Ndimu/limau 2
Pilipili
Unga wa ngano 1/2 cup
Yai 1...
Bizari 1/4 teaspoon (turmeric powder)

Namna ya kutaarisha
1)chemsha viazi vilivomenywa hadi viwive then bondabonda hadi viwe laini
2)weka chumvi,kitunguu saumu,ndimu na pilipili
3)changanya vizuri kisha tengeneza viduara vidogo vidogo

4)weka unga,bizari,yai na maji kiasi changanya vizuri uwe kama uji mzito mzito
5)weka mafuta katika karai
6)chukua viduara vya viazi ulivotengeza na upakae huo uji then kaanga kwenye mafuta..


Kachori tayari kwa kuliwa..
 
KACHORI :

Mahitaji :

Viazi 1/2 kilo
Kotmiri ilokatwa katwa
Pilipili ya kijani 1 ilokatwa ndogo ndogo
Chumvi
Garam Masala kjk 1 cha chai
Manjano ya unga 1/2 kjk cha chai
Sukari kjk 1 cha chai
Tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa kjk 1 cha chai

Mchanganyiko wa kuchomea :

Unga wa dengu gramu.
Hamira ya soda/chapa ya maandazi kidogo .
Maji
Mafuta ya kukaangia

Maelekezo :

Kosha na chemsha viazi
Vikiwiva menya na uviponde kisha weka pilipili, kotmiri, Garam Masala, sukari, tangawizi na kitunguu saumu, chumvi na kamulia ndimu kisha changanya.
Mchanganyiko wa viazi utakuwa tayari.
Tengeneza maumbo ya mipira

MCHANGANYIKO WA UNGA:

Anza kwa kuweka unga wa dengu kwenye bakuli, kisha weka hamira ya soda na chumvi , changanya vizuri kisha weka maji kidogo
Tengeneza uji mzito kisha engeza maji uwe mwepesi kiasi
Weka mafuta jikoni yakipata moto chovya kachori kwenye mchanganyiko wa unga na uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri
Andaa kuliwa kwa chatine
 

Attachments

  • KACHORI.jpg
    KACHORI.jpg
    8.1 KB · Views: 222
Wasalaam wapendwa wa jukwaa hili.

Ni mara kama ya pili najaribu kupika kachori za viazi lakini sipati matokeo mazuri. Tatizo ni nini? Nimeingia Youtube nimeangalia hakuna step ninayo kosea lakini zinatoka zikiwa laini saana.

Angalia picha hapa chini na kingine kuna taste siipati kama navyotaka.

Mchanganyiko na hatua zangu hizi hapa mtaziangalia kisha niambieni napo kosea.
1. Viazi
2. Chumvi
3. Binzari hii nina wasiwasi nayo labda mniambie kuna binzari za aina ngapi.
4. Ndimu
5. Unga wa ngano

Nachofanya nachemsha viazi kwanza kisha naviponda..baada ya hapa natengeneza balls nazidondosha kwenye mafuta ya moto.

Cha ajabu kinachotokea hiki hapa.
BeautyPlus_20200223121353468_save.jpeg
 
Mbona hutumii unga wa mkate,,,yaani mkate Anika juani ukikauka ule unga ndo baada ya kuchovya kwenye Ute wa yai na unga unachovya Tena kwenye bread crumbs
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom