Viazi Vya Madonge (Kachori) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viazi Vya Madonge (Kachori)

Discussion in 'JF Chef' started by MadameX, Sep 24, 2012.

 1. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Haya tena mambo ya Mombasa hayo.....tuburudike  [​IMG]

  Ingredients

  Viazi 10
  Chumvi kiasi
  Masala
  Unga wa dengu 1 cup
  Ndimu 3
  [h=3]Mataarisho
  [/h]
  1. Chemsha viazi na maganda yake.
  2. Vikisha wiva menya maganda na kata kila kiazi vipande viwili.
  3. Katika kibakuli koroga ndimu, chumvi na pilipili ya unga kisha pakaza katikati ya kiazi halafu gandanisha na kipande cha pili kiwe kama kiazi kizima.
  4. Fanya hivyo kwa viazi vyote vilivyobaki.
  5. Kwenye bakuli jengine koroga unga wa dengu , maji na chumvi kiasi uwe kama uji mwepesi.
  6. Kisha chovea kila kiazi kwenye unga huo halafu kaanga kwenye mafuta ukigeuza kama sambusa hadi kuiva.
  7. vikisha wiva panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
   
 2. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Mwanamke mapishi dada, hongera sana!
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  dah ... this stuff is very delicious ... I like it ...

  MadamX ... je nikichovya hivi viazi kwenye Maya kwa huu mchanganyiko nikavikaanga? will it be okay
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  mdizi, maya ndo nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  MadamX .... sorry .. I mean mayai
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. a

  amazon Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madame X, what if baada ya kutoa maganda hivyo viazi nikiviponda na kuvichanganya na viungo kabla ya kuvichovya kwenye huo unga wa dengu.... Will it be Okay?
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mmmh, sidhani kama itawezeka kwasababu lengo la kutumia unga wa dengu ni kuvishikiza viazi viwili pamoja. Mayai hayana uwezo wa kugandisha bila kuachiana unless utachangana na unga ngano kidogo.
   
 8. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #8
  Nov 23, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Aina ya 1...


  Mahitaji
  Viazi kg 1
  Chumvi kiasi
  Kitunguu saumu 1/2 teaspoon
  Ndimu/limau 2
  Pilipili
  Unga wa ngano 1/2 cup
  Yai 1...
  Bizari 1/4 teaspoon (turmeric powder)

  Namna ya kutaarisha
  1)chemsha viazi vilivomenywa hadi viwive then bondabonda hadi viwe laini
  2)weka chumvi,kitunguu saumu,ndimu na pilipili
  3)changanya vizuri kisha tengeneza viduara vidogo vidogo

  4)weka unga,bizari,yai na maji kiasi changanya vizuri uwe kama uji mzito mzito
  5)weka mafuta katika karai
  6)chukua viduara vya viazi ulivotengeza na upakae huo uji then kaanga kwenye mafuta..


  Kachori tayari kwa kuliwa..
   

  Attached Files:

 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Nov 23, 2013
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hii mbona tayari ipo hapa
   
 10. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #10
  Nov 23, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
 11. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #11
  Nov 23, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Ok shukraan kwa kunijuulisha sikujua hilo...
   
 12. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2013
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  bado urojo tu sasa.....
   
 13. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #13
  Nov 23, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Hahahahahah yeah na mishkaki lol....
   
 14. master09

  master09 JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2013
  Joined: Aug 12, 2013
  Messages: 538
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  Umesema unga ni unga upi wa ngano au ......
   
 15. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #15
  Nov 23, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Yeah unga wa ngano..
   
 16. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2013
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Na chips na badia. Na juice ya muwa kwa mbaliiii.


  Ha ha ha haaaaaaaa, farkhina na mimi49 najua nawatoa udenda
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2013
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  kabisaaaa...mhhh mdomo umejaa mate!!
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Nov 23, 2013
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mi nasubiri vipopo
   
 19. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2013
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  hivo mi sivipendagi najihisi ka nakula unga mbichi...wanaitaga vitobosha pia nadhani!!ftari hizoo....
   
 20. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #20
  Nov 24, 2013
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Hiyo juice ya muwa natamani nilie...:mad::mad::mad::mad::mad::mad:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...