Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,806
- 15,379
Viatu vya kisigino kirefu au mchuchumio vimekuwa ni maarufu sana siku hizi, karibu kila mwanamke anavutiwa na aina hiyo ya viatu, awe ni mwembamba au mnene, mrefu au mfupi wote wanavutiwa na viatu hivyo. Lakini wale wanawake wafupi ndio zaidi, hupenda aina hiyo ya viatu ili kuonekana ni warefu, ufupi umekuwa kero kwao, ajabu eh…!
Lakini kwa bahati mbaya uvaaji wa viatu vya mchuchumio huwa unawasumbua sana wanawake wengi, sio tu kuwasumbua, bali hutokea kutembea vibaya kiasi cha kuwafanya kuwa kichekesho na hata ule uzuri walioutarajia unakuwa haupo. Kwa hiyo mwanamke anakuwa kituko badala ya kupendeza.
Tafiti mbalimbali zimebainisha kwamba, viatu hivi vimewahi kuwaumiza sana wavaaji na hata kuwauwa pia. Pamoja na kuumia au kufa, kuna kuingia katika aibu kwa kushindwa kutembea vizuri na kugeuka kituko.
Inashauriwa kwamba ni vyema wanawake wanaopenda kuvaa viatu hivyo wafanye mazoezi ndani kabla hawajaanza kuvaa viatu hivyo vya mchuchumio hadharani. Kwa kufanya mazoezi kutawaepusha na ajali au fedheha watakapokuwa wanatembea barabarani……….
Ujumbe huu uwafikie wafuatao:
cacico, gfsonwin, snowhite, lara 1, Lisa, Ciello, charminglady, nivea, FirstLady, sweetlady, AshaDii, King'asti, @FP, Preta, marejesho, Madame B, na wanyange wengine watumiao aina hiyo ya viatu..............