Viatu virefu (High heels) vilitengenezwa kwanza kwa ajili ya wanaume

Ramsy Dalai Lama

Senior Member
Apr 5, 2021
147
540
Ingawa leo hii high heels ni fashion kwa ajili ya wanawake lakini ukweli viatu virefu viliundwa kwa ajili ya wanaume.

Mwisho wa karne ya 16, ndipo high heels zilianza kutengenezwa huko Uajemi (Persian) kwa ajili ya wapanda farasi.

man%20high%20heels2.jpg

Lakini katika karne ya 17 vilipo ingia Europe vikawa vinavaliwa na wanaume lakini si kwa ajili ya farasi bali ikawa kama fashion trend kwa ajili ya matajiri na wafalme kama wakina King Louis XIV.

man-heels-louis-xiv_nnkovf.jpg

Wanaume wengi walitamani kuvaa viatu hivi na hii ilipekea mpaka baadhi ya matajiri kuvaa higher heels yani virefu zaidi ili kujitofautisha na watu wa hali ya chini.

man%20high%20heels21.jpg

kulingana na Jumba la kumbukumbu la J. Paul Getty, Viatu vya High heels vilionekana kuwa ni upperclass status shoes (yani vya washua) na pia vilikua vya kiume na pia ilitumika kama njia nzuri ya kuongeza urefu wa mtu kwa inchi chache yani kukufanya uonekane mrefu haswa kwa wanaume wafupi.
man%20high%20heels%20vintage.jpg
man-high-heels-closeup-old-fashioned-baroque-heel-shoes-white-stockings-worn-49092182.jpg
 
Back
Top Bottom