Viashiria vikuu vya Mwanaume anayekupenda

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
VIASHIRIA VIKUU VYA MWANAUME ANAYEKUPENDA.

Anaandika, Robert Heriel.

Kutokana na Wadada wengi kunifuata PM kuniuliza "watajuaje mwanaume anayewapenda?" Nikaona isiwe kesi niweke hapa ili kila mtu aone, Kupunguza usumbufu WA hapa na Pale.

Nitajitahidi kuifupisha makala hii Kwa kadiri niwezavyo, ingawaje napendelea maandiko marefu.

Kwenye upendo kuna Kupenda Kwa AKILI na Kupenda Kwa HISIA. Hata hivyo upendo wa wengi umetawaliwa zaidi na HISIA kuliko AKILI.

Pia katika Kupenda kuna Upendo WA KUTOA(GIVE) NA Upendo WA kupokea(Receive), Upendo wa kutoa upo wa Wanaume, upendo wa kupokea upo Kwa Wanawake,
Ingawaje mwanamke mwenye upendo uliopitiliza Huwa pia na upendo WA kutoa. Yaani sio shida mwanamke anayekupenda Kwa dhati yote akakupa pesa.

Kwenye UPENDO KUNA MAMBO MAKUU YAFUATAYO:

1. MUDA NA NAFASI
2. MVUTANO NA MFANANO
3. UMILIKI
4. MAWASILIANO
5. KAFARA

1. MUDA NA NAFASI
Muda na nafasi ndio huwakutanisha watu. Unaweza pata muda lakini usiwe na Nafasi, halikadhalika unaweza pata nafasi lakini usiwe na muda.
Umemuona Manzi kwenye Daladala ambaye hujawahi kumuona, ukavutiwa Naye lakini Kwa bahati mbaya unakosa nafasi ya kupata mawasiliano naye, Kutokana na changamoto mbalimbali, halikadhalika na kinadada vivyo hivyo.

Kuna watu wanajua kutumia muda vizuri kutengeneza nafasi, huu ndio mwanzo mpya wa mahusiano.

2. MVUTANO NA MFANANO
Ukishapata muda ya kukutana kinachofuata na mvutano, umemuona kijana mzuri, ukavutiwa naye kinachofuata ni kuchipua Kwa upendo kutokana na Mfanano. Kumbuka siku ya Kwanza mtu anaweza Kupenda Kwa HISIA tuu labda ni tamaa lakini Kama hakuna mfanano upendo huo hautadumu.

Kwa Sisi wanaume, kila mwanamke mzuri apitapo mioyo yetu humtamani, humpenda Kwa zile dakika chache za uwepo wake, lakini akipita tunamsahau, Kwa sababu hakuingia akilini, zingatia Sehemu pekee ya kuhifadhi kumbukumbu kwenye mwili WA binadamu ni Ubongoni, kuna Short term Memory, na long-term Memory ingawaje ubongo haupo Rasmi Kama sehemu ya kuhifadhia daima kumbukumbu zetu, zipo kumbukumbu zinazokaa Kwa muda mrefu Sana lakini haItakaa Daima.

Baada ya jitihada kufanyika UFANANO Huweza leta upendo wa Akili ambao hudumu zaidi ingawaje sio milele.
Zingatia, mwanadamu hapendi DAIMA/MILELE Ikiwa TOFAUTI Zitaanza kujitokeza.

Upendo wa moyo ni mtamu lakini hauna Guarantee kwa sababu unaendeshwa na hisia kiasi kwamba unapofusha macho yasione na akili isifanye kazi sawia, hata mtu anapoenda kwa mganga wa kienyeji huenda kuipumbaza akili na wala sio moyo.

3. UMILIKI
Kwenye umiliki ndipo wivu unapozaliwa, ushapata muda na nafasi, ushavutiwa na kuona mnafanana, sasa unahitaji kummiliki awe wako peke yako, hapo mtu atamuona mwenzi wake kama Mali yake vile hivyo hataki mwingine yeyote aisogelee. Umiliki ni sehemu muhimu ya Upendo.

Mambo yanayoleta Umiliki:

I/ huduma
Mwanaume anatoa Huduma Kama pesa, nguo, chakula, makazi, na penzi n.k. Mwanamke naye anatoa Penzi, muda wake Kwa sababu mwanamke ndiye mwenye muda Kwa sababu ya nature, wanaume hatuna muda Sisi ni Kama Mungu, ndio maana mwanamke anaenda mwezini, pia huwahi kuchakaa, na kukoma kupata mtoto tofauti na Mwanaume ambaye yeye halimitiwi na muda.

Pia Mwanamke atatoa Huduma Kwa kumpikia na kumtunza mume au Mpenzi wake, huku akihakikisha hakuna mwanamke mwingine anayesogelea Mume wake.

Huduma ni moja kipengele muhimu katika umiliki, huwezi kummiliki mtu usiyemhudumia.

2. Tendo la ndoa
Ukimgegeda mwanamke kwa kiwango cha juu ni wazi umemmiliki, atakuonea wivu na hatataka mwingine apate Raha anazozipata, tendo la ndoa ni moja ya vitu nyeti katika kummiliki mwenza wako, hasa kwa mwanamke.

Mwanamke anaweza kukuvumilia kisa humpi pesa lakini kamwe na haitokuja kutokea akakuvumilia ikiwa humkuni ipasavyo, hakuna mwanamke wa namna hiyo Duniani.

Pia Mwanamke mtundu duarani kunako Sita Kwa sita, fundi wa kuchonga na kubana, kukata na kucheza sebene akaukuja moyo wa mwanaume kunako duarani ataumiliki moyo wa mwanaume.

Sio mwanamke anayejilaza Kama Gogo au asiyejishughulisha kitandani, yupoyupo tuu. Ipo Raha ya mwanamke anayepiga vyenga na kufinya mipira ya maudhi, hapo mwanaume hatoboi.

3. MTOTO
Mwanamke linapokuja suala la mtoto hataki mchezo, kwanza elewe ili mwanamke akubebee mimba ni lazima awe anakupenda, achana na hizi mimba za bahati mbaya.

Mwanamke mwenye mtoto jua mume aliyemzalisha anasehemu ya umiliki wake katika moyo wa mwanamke huyo.

Labda itokee huyo mwanaume awe hampi attention, hamjali wala kumpetipeti. Ndio maana Single mother kumuoa inaleta shida Kwa sababu anakuwa na umiliki wa wanaume wawili Jambo ambalo ni gumu kwake na Kwa aliyemuoa.

Ponapona ya uliyemuoa single mother ni huyo Baby Daddy wake asiwe anamjali wala kumpa attention huyo Mama vinginevyo ni ngumu Sana. Tena huyo Mzazi mwenza akiwa anauwezo WA kiuchumi kukushinda au anahadhi au Cheo Fulani kinachompa utukufu mwanamke. Elewe hakuna mwanamke asiyependa utukufu na sifa. Ndio hayo mambo yanayoendelea Kwa sijui Faiza Ex wa Mhe. sugu.

5. KAFARA
Mwanamke au mwanaume anayekupenda lazima ajitoe kivyovyote Kwa ajili yako. Kuanzia muda wake, Mali, na ikiwezekana mwili na roho yake.

VIASHIRIA VIKUU VYA MWANAUME ANAYEKUPENDA;

1. HESHIMA YA WOGA
Asije kuambia mtu Mwanaume akikupenda lazima atakuwa anaheshima ya woga kwako. Kwanza ataogopa kukupoteza, na hii itamfanya ajitume na kupambana ili uwe wake.
Hata kwenye kutongoza mwanaume anayekupenda hawezi kujiamini moja Kwa moja. Yaani hatakuwa na Swaga nyingi na mara Kwa mara atakuwa anaogopa majibu kwani hataki kukupoteza.

- Heshima ya woga itamfanya asiweze kushobokea mademu wengine mbele yako,

- Heshima ya woga itamfanya awe Kama zoba Fulani, hataona shida kuomba Msamaha na kutaka kumaliza mambo Kwa Amani hata Kama mwenye makosa ni wewe. Hii ipo hata Kwa wanawake.

- Heshima ya woga itamfanya azingatie Kauli zako Kwa nidhamu ya Hali ya juu Sana.

- Heshima ya woga itamfanya apoteze kujiamini pindi uwapo mbele yake.

- Heshima ya woga itamfanya apungue kiwajibu na kimajukumu ya kudhibiti tabia zako mbaya, atakuwa anaogopa kukukanya huku akiwa ni mtu wa kulialia tofauti na Sisi manyang'au.

Mtu anayekupenda hawezi kukupiga wala kukutukana labda awe amelewa, nazungumzia matusi ya nguoni au kukupiga makofi na ngumu zitakazokuumiza.

2. MAWASILIANO
Hapa binti unisikilize zaidi, maana ndipo penye viashiria vya wazi.
Mawasiliano ya mtu anayekupenda huanza tangu siku ya Kwanza mliyokutana. Saikolojia ya mwanaume ni tofauti na Mwanamke. Mwanaume huuona uzuri wa mwanamke akiwa Hana mazoea naye, uzuri huo huanza kupungua kadiri mazoea yanapoendelea.

Mfano, mwanaume akikuona siku ya Kwanza atakuona umzuri Kwa hata 90% akishakusalimia ukamuitikia na kumchekea Asilimia kadhaa hupungua, ukimpa namba zinazidi Kupungua mpaka 50% tafsiri yake anazidi kuona wewe ni wakawaida Kwa kuona mapungufu yako.

Kabla hujamkubalia unakuwa na uzuri zaidi na zaidi kwake, lakini ukimkubalia hata Ile hamu na shauku yake hupungua, akikugegeda ndio Kabisa anajuta Kwa nini alikutongoza kumbe mtu mwenyewe WA kawaida, kilichokuwa kinamsumbua ni Nyege zake.

Wanaume wengi tupo hivyo, ukishamgegeda mwanamke hutaki hata kumuona, na tukishaagana baada ya mechi tunaweza kaa hata siku tatu mpaka wiki bila kuwasiliana na huyo mwanamke ni mpaka Nyege zianze tena😀.

Ingawaje tunawapaga sababu za hapa na pale huku tukificha ukweli.

Hii ni tofauti na Mwanaume anayekupenda, Mwanaume anayekupenda kila siku anayokuona anakuona unazidi kuwa mzuri, anazidisha mawasiliano zaidi na zaidi.

Ukimpa Denda na Kuruhusu achezee mwili wako bila ya ku-sex mpaka amwage bado uzuri wako atauona unazidi kuongezeka, atazidi kukupenda, lakini mwanaume asiyekupenda ukimpa tuu Romance na uachezee mwili wako bila ya sex hicho tu utayaona Mabadiliko katika mawasiliano yake, namna anavyoongea na wewe n.k.

Zingatia, mwanaume anayeigiza hawezi kuigiza Kwa siku 90 mfululizo, usimpe mchezo mwanaume ndani ya miezi mitatu Ila kuwa naye karibu zaidi na zaidi ili uweze kusoma nyendo zake na akili yake.

Sio unamnyima ili kumpima alafu unamuweka mbali, sasa sijui utampimaje mtu ambaye yupo mbali. Jitahidi kila siku mnaonana, tena ukiwa Low Key, sio umejipendezesha utadhani wewe ndio unamtongoza bhana!
Ukaribu utakusaidia kufichua udanganyifu wake, MPE nafasi Kama kukuchumu, muache afanye mambo mengi kwako lakini asikuvue nguo, kisha kesho hivyo hivyo Kwa siku Saba mfululizo alafu note, kila ukitoka kwake mpaka kesho yake ana-act Kama siku ya Kwanza.

Je, anakujali Kama Mwanzoni, anaongea na wewe Kama Mwanzoni,
Je anakuruhusu uende kwake Kwa njia ya wazi au ndio unaingizwa ndani kinyemela Kama Jizi au mganga.

Baada ya mwezi mmoja mjaribu unataka mubadilishane Laini za simu angalau Kwa usiku mmoja tuu! Mpime na mtazame usoni machoni, akikubali kirahisi badilisha laini weka kwenye simu yako kisha endeleeni na Stori wakati WA kuondoka akikusindikiza mpe laini yake.

Akikataa mkomalie, ukiona kang'ang'ana jifanye unaondoka Kwa hasira, ukiona hakubembelezi achana naye Ila akiendelea kukung'ang'ania mpige milio ya pesa huyo muweke kundi la wanaume wa kuwachezea na kuwachuna. HAKUPENDI!

3. KUKUFUNDISHA, ATAKUWA MWALIMU na DAKTARI WAKO
Siku zote mwanamke mwenye akili hujifanya mjinga Kwa Mwanaume ili Kupima Uelewa wa mwanaume. Usijitutumue Kwa mwanaume kwamba unaakili, jifanye mjinga uone atafanyaje na atakuchukuliaje.
Mwanaume anayekupenda atapenda Sana kuwa mshauri wako, Ila wewe jifanye kichwa nazi, akikuambia usivae nguo fupi wewe vaa alafu umwambie huoni shida ya wewe kuvaa nguo fupi Ila shida unaiona Kwa Wanaume wasioweza kujizuia.

Msikilize anauwezo wa kukufundisha Kwa Logic au ndio Wale Wazee WA amri na matusi..Atakushauri namna ya wewe kuwa Bora kuliko historia yako ya zamani, hata Kama amekukuta na mtoto yaani wewe ni single Mother atakushauri na kukupa elimu namna ya kuyafurahia mapenzi na mahusiano mapya licha ya kuwa single mother.

Muulize wewe ni single mother; Kwa nini akupende wewe wakati kuna wasichana wabichi kabisa ambao hawajazaa, msikilize, jifanye unamshauri kuwa ni Kheri afuatane na wasichana wasio na watoto, jaribu kuwaponda single mother na toa mifano ya wazi ya single mother waliozingua, kisha msikilize anasemaje,
Mwambie wewe bado unampenda aliyekuzalisha na unahisi utamsumbua, muulize atawezaje kuondoa hisia hizo ili umpende,

Mwanaume anayekupenda atakuwa mwalimu wako, mwalimu na Daktari hutibu akili na Afya za watu.

4. Atakuwa analitaja jina lako mara Kwa mara Kwa Rafiki na ndugu zake.
Hilo haliepukiki, atashindwa kujizuia katika hili. Mwanzoni ataona shida na aibu kukutaja lakini mwishowe itakuwa dhahiri.

5. Hataona aibu kutembea na wewe na kukutambulisha Kwa watu anaowaheshimu. Usipende kutambulishwa Kwa Mama mzazi, mara nyingi Mama na mtoto wa kiume ni mtu na rafiki yake, Mama siku zote huwa upande wa mtoto wake iwe Kwa wema au Kwa ubaya.

Hii ni tofauti na Baba, penda kutambulishwa Kwa Baba Mkwe, Baba ni Rafiki wa mtoto lakini katika Mambo Mema tuu. Hakuna Baba ambaye atataka kijana wake abadilishe badilishe wachumba, Kwanza ataona kijana wake kama hamnazo na hajakomaa.

Ila Kwa Mama unaweza kutambulisha hata Wasichana kumi, hasa Wamama wasiomcha Mungu, ndio maana hawajui hisia za mabinti wa wengine.

Jaribu kuchunguza ni Nani ambaye Mchumba wako anamheshimu katika maisha yake, the Top ambaye hataki kumuudhi na ambaye anajielewa, ukishamjua, huyo ndiye akikutambulisha kwake ujue anakupenda.

6. Atawaheshimu Wazazi na ndugu zako.
Jitahidi ujifanye unazinguana na Mama yako kisa yeye, mfano; mwambie Mama anataka likizo hii niende kumsalimia, alafu sema; wewe unataka uwe naye(Mpenzi wako), jifanye unachukizwa Sana na tabia ya ndugu na wazazi wako kukufuatilia, alafu Sikilizia atasemaje,

Kama anakupenda atahakikisha anajikita kukuelekeza namna ya ku-balansi upendo wako kwake na heshima ya wazazi wako. Atakuambia Umheshimu Mama na Baba, Kama anaakili na anakupenda hatataka uwaudhi wazazi wako kisa mahusiano yenu, atakuambia utakaa nusu ya likizo kwake kisha siku zilizobaki utaenda kuwasalimia wazazi wako.

Lakini kama mtu hakupendi ataangalia ubinafsi wake, atakuambia ubaki kwake Kama kweli unampenda, au atakuambia uende Kwa wazazi wako Kwa hasira au kukupima,

Zingatia, bado hajakuoa, hivyo akili yake na upendo wake lazima viwe na uwiano.

Jitahidi uwe mjanja ili ujue upendo wa kweli.

7. ATAUMIZWA NA MAMBO YANAYOKUUMIZA
Mwanaume anayekupenda kikamilifu huumia pale anapokuona unaumia iwe unaumia Kwa kujua au Kwa kutokujua.
Mfano, unaenda kanisani au kazini haujavaa vizuri; kuna wanawake ni don'care lakini hiyo haimfanyi mwanaume anayekupenda asigundue Hali yako inaumiza.

Mwanaume anayekupenda ataumizwa na Hali yako kuwa duni, atahangaika hata Kwa kidogo alichonacho kuhakikisha walau nawe unapendeza.

Mwanaume yeyote anajua kuwa mwanamke asipopendez anaumia.

Zingatia pia, wanawake wengi wanaheshimu wanawake wenzao wanaopendeza kuwashinda kwani hiyo ni kiashiria kuwa wanapendwa. Na wanawake wote Duniani wapo Kwa ajili ya Kupendwa na wana-fight Kwa ajili hiyo popote walipo.

- Mwanaume anayekupenda atahakikisha hakuumizi kihisia iwe kwa kuchepuka na wanawake wengine waziwazi, atajificha kadiri ya uwezo wake wote ili kutokuumiza, zingatia wanaume karibu wote Duniani kuchepuko ni Jambo lililowashinda, na hata wasiochepuka ni kwamba hawataki kuwaumiza wenza wao hivyo hujificha Sana.

- Mwanaume anayekupenda hawezi kukutukana matusi ya kuumiza moyo wako, kamwe hawezi kukupiga Kwa ukatili labda kukupiga makofi mawili matatu ya kukuweka Sawa. Sio akupige mpaka utoe Damu au kukukata kata au kukunyoshea bastola.

- Mwanaume anayekupenda hatafuti kuogopwa Bali kuheshimiwa. Kwa maana wenye chuki ndio hupenda kuogopwa na maadui zao,

8. ATAKUWA UPANDE WAKO
Hata kama umekosea Mwanaume anayekupenda atakuwa upande wako na kukutetea hasa mbele za watu.
Ila mkiwa ndani ndio mtapambana kuwekana Sawa.

Jaribu kukosea Kwa makusudi mbele za watu, akiwepo Mpenzi wako kisha msikilize atafanyeje, hiyo hujitokeza Kwenye familia mtu anapooa, unakuta Mke anakuwa bedui mbele za Wafanyakazi wa Ndani ukiona hivyo mwanaume jifanye Kama huoni, Ila mkiwa chumbani muweke Sawa Mkeo kulingana na mashauri na Nasaha za Dini yenu.

Lakini sio uingilie ugomvi na kukaa upande wa Mfanyakazi au mtu Baki Hilo ni kosa la kiufundi.

9. ATAKUJALI WEWE KULIKO KUJIJALI MWENYEWE
Mwanaume anayekupenda utamuona kwenye vitu vidogo dogo. Atakuwa gentleman, kuanzia mambo ya vyakula, mavazi, sehemu ya kukaa atakupa kipaombele. Sio mwanaume yeye ndiye anataka vikubwa kuliko wewe hapo hamna kitu.

Ukienda kwake au akija kwako Mpenzi wako, au mkienda Out Hotelin au popote, mkiagiza muwekee makusudi vitu vizuri na vinono kukuzidi alafu muone atafanyaje, Kama anakupenda atakupa vile vizuri na vinono, mfano atachukua paja na minofu na kukuambia Kula Mpenzi hizi ni tamu Sana. Na sio mara moja au siku ya Kwanza tuu hiyo ndio tabia yake throughout.

Sio unakuta jitu linajijali lenyewe mwishowe likija kukuoa ndio Yale yanakupimia mpaka vipande vya nyama au kuweka Alama ya kiganja kwenye ndoo ya Unga Kwa uchoyo.

Mwanaume anayekupenda hawezi kuwa mbinafsi, atakujali wewe kuliko anavyojijali yeyr mwenyewe na hiyo ndio sifa ya mwanaume au Baba.

Usije ukafikiri kupewa pesa na Mwanaume ndio Kupendwa au kujaliwa Hasha! Wengine wanakuhonga pesa Kwa sababu wanaziada yaani hawatoi Kwa moyo isipokuwa Kwa sababu yakuwa na pesa ya ziada zisizo na kazi.
Mfano, mtu anamilioni Mia moja, akikupa hata milioni Kumi huyo huwezi sema anakupenda, ila mtu mwenye elfu hamsini alafu anamatatizo kibao alafu akakupa elfu 30 huyo anakujali kuliko anavyojijali.

Kwa Leo tuishie hapa!

Ulikuwa nami

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Yaani wewe Jamaa wewee!

Umeona Ufumue Mshono sio!!?

Hayaa.
 
Sawa Mkuu tupe mbinu za Kupata watoto wazuri bila pesa.

Ntakuja na Uzi huo.

Hata siku moja usitafute pesa ukadhani wanawake ndio watakupenda, watapenda pesa zako na watazila mwishowe uanze kurusha RISASI 😀😀

Uwe mjanja tuu, mtanashati na uwe unajua kuutumia ulimi wako sawia. Wanawake huo ndio Uchawi wao mbali na pesa ambao ni mtego
 
Sasa taikon umeuza siri ya kambi, tutaficha nyuso zetu wapi? Bora ungeweka sawa sawa na za kwao pia. Maana wanatupiga sana na macho ya kurembua na mawezere yaliyotuna kama mkia wa kondoo aisee
 
Sasa taikon umeuza siri ya kambi, tutaficha nyuso zetu wapi? Bora ungeweka sawa sawa na za kwao pia. Maana wanatupiga sana na macho ya kurembua na mawezere yaliyotuna kama mkia wa kondoo aisee

Uzi wao unakuja Mkuu!

Wala Hilo lisikutishe wao wameumbwa kudanganywa
 
Ntakuja na Uzi huo.

Hata siku moja usitafute pesa ukadhani wanawake ndio watakupenda, watapenda pesa zako na watazila mwishowe uanze kurusha RISASI 😀😀

Uwe mjanja tuu, mtanashati na uwe unajua kuutumia ulimi wako sawia. Wanawake huo ndio Uchawi wao mbali na pesa ambao ni mtego
Naturally ni wanaume wachache ndiyo hutakiwa na wanawake wengi. Yaani kundi la wanaume wachache sana ndiyo huvutia wanawake karibu wote.

Ukichukua sample yeyote ya population, kwa mfano chuo kikuu cha Dodoma, wanaume wanaotakiwa kiasili kama factors zote zingine zisingekuwepo ni wachache sana wange-qualify kumwaga mbegu zao kwenye gene pool kubwa sana (close to n) ya mbegu za kike.

Kinachofanya wanaume wae wengi ni maendeleo ya mfumo wa kimaisha wa mwanadamu ambao umemfanya mwanadamu kuibadilisha nature in his favor. Mfano mzuri ni pesa, ambayo inakupa nguvu usiyokuwa nayo naturally.

Yule jamaa aliyefichwa na Bi. Aisha kule Tabata, labda naturally asingekuwa na nafasi ya kuchangia kwenye mbegu za kike anazotaka yeye, lakini pesa ambayo si lazima amezipata kwa jasho au akili zake zilimfanya afichwe.

Mfano mwingine mzuri labda ni texts zinavyosaidia madomo zege au kofia zinavyosaidia watu wenye mandonga.
 
Sasa hapa ili picha linoge ungeweka na zakwao ili iwe 1-1 au both team to score

Lakini hii ya 1-0 dah ushachana mkeka
 
Back
Top Bottom