Viashiria katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili na viwakilishi vyake

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Tunaishi katika dunia mbili na nyakati mbili, dunia halisi na nyakati halisi ama dunia ya uwakilishi na nyakati za uwakilishi. Tunaweza pia kuishi kwenye dunia halisi ila nyakati zika za uwakilishi na kinyume chake.

Kiwakilishi ni nini?

Kiwakilishi ni alama inayosimama badala ya kitu fulani. Jina lako unalotumia hapa ni kiwakilishi cha jina lako halisi na jina lako halisi ni kiwakilishi cha wewe katika nafsi hai.

Hakuna kitu kinachokosa uwakilishi kiwe chenye uhai ama kisicho na uhai. Nyumba ni kiwakilishi cha makazi, alama za barabarani ni viwakilishi vya matumizi sahihi, tahadhari na ishara za barabara utumiayo. Bendera mbalimbali, michoro picha na ramani vyote ni viwakilishi vya jambo ama kitu fulani!

Alama pia ni kiwakilishi katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili vinavyotambulisha uumbaji na uundaji. Angalia taa za barabarani kila rangi ina tafsiri na maana yake kimwili na kiroho pia, vile taa nyekundu inavyoashiria hatari ya ajali kiroho vilevile tafsiri ni moja: HATARI.

Chukulia mfano wa pete katika vidole vya binadamu kila kidole kina tafsiri yake kimwili na kiroho unapoivaa, maarufu ikiwa ni pete ya ndoa. Hii ndio ithibati pekee ya wazi kwa kila mtu kuwa huyu mtu yuko kwenye mahusiano rasmi kiimani na kisheria. Pete ya ndoa ni kiwakilishi cha muunganiko wa watu wawili wa jinsia mbili tofauti. Kuna tafsiri nyinginezo na pete za aina mbalimbali tuzivaazo vidoleni mwetu.

Utu wako wa ndani, vile unavyojiona. Kuna mwingine yuko rohoni anakuwakilisha. Rejea mada za vivuli vitatu na nafsi tatu. Chochote kiwe cha kimwili ana cha kiroho hakiwezi kufanyika bila wewe halisi ama utambulisho wako. Jina lako hubeba dhima kubwa ya utambulisho wako mpaka rohoni. Ukiitwa kwa jina lako kamili hakuna mwingine atakayeitika kwakuwa yeye siyo wewe.

Vitu tunavyomiliki vina muunganiko nasi, vitu vinavyotokana nasi pia kiroho ni sehemu yetu. Nguo zetu za ndani na nje, nyayo, nywele, sauti, nafsi pete, n.k vyote hivi ni viwakilishi vyetu halisi na muhimu kabisa! Alama mbalimbali kama picha mawe ya msingi, kumbukumbu ya tarehe za matukio fulani vyote hivi ni viwakilishi vinavyobeba roho za uhalisia wa vitu mbalimbali.

Nimejaribu kuchambua kwa undani na mada hii ni kwa msaada mkubwa wa dada Divine... Natumai atakuja kuendelea na kuongeza palipo pelea.
 
Kwenye mambo kama haya ndo hua nakukubali kaka.ila kwenye siasa pamoja na kwamba siasa ndo maisha yetu lakini imejaa ulaghai mwingi ni afadhari tuwaachie wao maana siasa ninuongo uongo hivi.ila tukija huku mimi ni mshirika wako mkuu.SHIKAMOO
 
Kwenye mambo kama haya ndo hua nakukubali kaka.ila kwenye siasa pamoja na kwamba siasa ndo maisha yetu lakini imejaa ulaghai mwingi ni afadhari tuwaachie wao maana siasa ninuongo uongo hivi.ila tukija huku mimi ni mshirika wako mkuu.SHIKAMOO
kuna makala moja ya uchawi uliita ni bonge na upuuzi ila sikuchukulia negative.. Nadhani kuna kitu kilikukwaza sana kwenye ile post
 
Boss unaweza kunijuza mfano katika pete katika vidole vingine (ukiachana na kile cah ndoa) humaanisha nini?
 
boss unaweza kunijuza mfano ktk pete ktk vidole vingine(ukiachana na kile cah ndoa) humaanisha nini?
Kidole kinachovishwa pete ya ujane
Kidole kinachovishwa pete ya talaka ama kuachika
Kuna pete za kinga..
Pete za bahati
Pete ya useja
Pete za kishetani Freemason nknk
 
Kwenye mambo kama haya ndo hua nakukubali kaka.ila kwenye siasa pamoja na kwamba siasa ndo maisha yetu lakini imejaa ulaghai mwingi ni afadhari tuwaachie wao maana siasa ninuongo uongo hivi.ila tukija huku mimi ni mshirika wako mkuu.SHIKAMOO
Kweli tupu walahi!
Siasa hapana walahi!
 
Sasa Mshana Jr, Sijaona ulipozungumzia Ulimwengu wa Roho na uhusiano wake na Uliimwengu wa Mwili.

Nipe ufafanuzi Mkuu

Bazazi
Soma aya zinazozungumzia vitu vinavyohusiana nasi na pale watu wabaya wanapotaka kukudhuru huvitumiaje?
Viapo! Unaanzaje kuapa? Mimi fulani..... Hapo unajiunganisha kiroho na hicho kiapo..
 
Naomba nifundishe kesho, leo msome kwanza,

Mungu anitie nguvu, mniombee pia.
Karibu na asante sana.. Please sema chochote leo.. Kidogo tu.. Hasa viashiria kama mawe na madhabahu za kifamilia.. Sherehe za kimila, matambiko na makafara kama viashiria
 
Kidole kinachovishwa pete ya ujane
Kidole kinachovishwa pete ya talaka ama kuachika
Kuna pete za kinga..
Pete za bahati
Pete ya useja
Pete za kishetani Freemason nknk
duh!
hiyo ya pete ya talaka kwangu mpya.

shukrani mkuu.
 
Mimi nina jina sawa na mama yangu, kwa kweli mimi binafsi sikumbuki kuwa tegemezi tangu utoto wangu!
Nimesaidia ndugu zangu wakubwa na wadogo!
Nimekuwa kama mama yao mdogo kabisa!
Kweli jina lina nguvu sana!
 
Back
Top Bottom