Viapo Vya Wakurugenzi: Rais Magufuli ameteua Wasomi, aagiza Serikali itumie EFD, Wagawa vyeo kukiona

Mr. Zero,
Kama JPM anaweza kukariri idadi ya dagaa na samaki wote walioko ziwa Tanganyika,Ziwa Victoria na ziwa Nyasa atashindwaje kuwajua watu wake wa karibu?
Wasiwasi wangu ni pale tu anapochemka kwenye kurudia majina yaleyale kwenye nyazifa tofauti toauti. Kwamba leo Luhende kateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri lakini utashangaa kesho anateuliwa kuwa DAS wa Halmashauri ya mji mwingine.....................!!!!!!!Hapa Kazi tu at work.

Hapo sawa. Kama anawajua ni lazima watakuwa ni watu wake wa karibu ... hivyo teuzi zake zitakuwa questionable!!?
 
Raisi anapata muda wa kusoma udaku mitandaoni?nauliza tu

swissme
Tatizo Bawacha mumezidi kuleta udaku humu ndani oneni sasa mnavyoumbuliwa...............mtu mwenye Masters mlisema ana cheti aibu yenu......!!!!!!!!
 
Kumbe anasoma/anapitia mitandao ya kijamii. Sasa mbona suala la binti yake mpendwa, Je.sca hajawahi kulifafanua ama kueleza ukweli licha ya kwamba limenadiwa sana mitandaoni kuliko hata hilo saga la Luhende? Au ndo tuamini kwamba ni kweli huyo binti ameingizwa Chuo Kikuu pasi kukidhi vigezo?
 
View attachment 365501 View attachment 365503

Rais JPM anahutubia Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji Ikulu Dsm
Moja ya jambo analosema limemsikitisha ni mitandao ya jamii kumuandika Luhende kama Msomi mwenye cheti cha hotel Management wakati ana Masters na alikuwa mkaguzi wa elimu wa kanda.

Rais anasema amepitia kwenye mtandao mmoja wa kijamii akaona comment za watu juu ya Luhende akabaki kucheka tu,amemsimamisha Luhende na kuwataka waandishi wa habari wampige picha na waende Sinza kumpiga picha Luhende Meneja wa Hotel na kuzisambaza mitanadaoni

Rais pia anasema anawafahamu Wakurugenzi wake wote,anasikia malalamiko kwenye mitandao ya kijamii,amewaambia wajishangilie wao na si kusikitika kwa kutokushangiliwa na mitandao ya kijamii,anasema hao wasioshangilia kwenye mitandao ni maadui zake,..."Watachonga sana lakini wataka kimya"

Rais anasema zamani nafasi za ukurugenzi zilikuwa "deal",na pale TAMISEMI kulikuwa na mtandao wa kuhongwa ili kuwapatia watu ukurugenzi,aliishagiza Waziri awaondoe wapo watatu pale utumishi ambao kazi yao ilikuwa kuhongwa na kugawa vyeo vya Ukurugenzi.

Rais anasema Wakurugenzi wote aliwapitia jina kwa jina na ndio maana hasafiri ili kufanya mambo yeye mwenyewe na wakati mwingine hulala hata saa nane ili kujiridhisha mambo.

Rais amepiga marufuku Wakurugenzi kutoa "tender" kwa Madiwani na Wanasiasa wafanyabiashara ambao hutumia nafasi zao kushinda zabuni,wapinge kodi ndogondogo kwa wananchi kama za kina mama wauza mchicha,ambao halmashauri zinadai kodi wakati hata mbolea wala mbegu hawakuwasaidia.Watumie madaraka ya kisheria kuwaondoa "watumishi" Miungu watu kwenye vijiji,kata,tarafa na wilaya.

Rais anasema hawezi kuchagua mtu ambaye hawezi kutekeleza sera ya chama cha Mapinduzi wala aamini katika Chama cha Mapinduzi sababu wananchi walichaguwa Chama cha Mapinduzi kutokana na uzuri wa ilani yake.Kwenye mitandao ya Kijamii anasikia kuwa watu wanalalamika anachaguaa watu wasio na "experience",anasema yeye hataki mambo ya ma-experience experience tu,hawezi kuchagua mtu mwenye experience wakati ni mwizi.Kuna watu walijipanga na kutuma "vimemo" ili watu wao wachaguliwe kwenye nafasi hizo,akawafutilia mbali wote waliotumwa na waliotuma.

Rais anasema hawezi kuchagua "******",anajuwa kuna watu hawapendi neno ****** ila yeye hawezi kufanya kazi na ******.Waandishi wapige picha cheti cha Luhende ili watu waongo wa mitandaoni washindwe na walegee.(Vi...la...za)

Rais anasema alistuka sana pale majina ya Wakurugenzi yalivyotoka hadharani na kuanza kuona ukosoaji mkubwa mitandaoni,kiasi akaanza kujiuliza nimekosea nini kuteuwa,akaanza kuwa na wasiwasi lakini baadae akajuwa ni maneno tu ya mitandaoni.

Mwisho Rais amewaasa Wakurugenzi wasikilize maneno ya watu na ya mitandaoni,waende kufanya kazi hata kama hawana uzoefu na kama ni uzoefu wataupata huko huko.Ndio maana katika Wakurugenzi waliokuwepo wamerudi 60+.Hakutaka kurudisha Wakurugenzi wezi na mafisadi eti kisa ni uzoefu.

Rais Magufuli: Haiwezekani tunahamasisha wafanyabiashara watumie EFD, lakini sisi serikali tusitumie.

Rais Magufuli: Ikiwezekana, Wakurugenzi waende na EFD kwenye halmashauri zao wakaanze kuzitumia kukusanya mapato.

Rais Magufuli: Wananchi wa chini wanateswa na kunyanyaswa na vikodi vya ajabu ajabu, nawaomba mkatatue kero zao.

Rais Magufuli: Kwa jinsi ninavyoona sura zenu hapa kweli naamini mnaenda kufanya kazi,kwani sura zinaonesha ninyi ndio wenyewe.

Rais Magufuli: Kuna watu wanalalamika fedha zimepotea, hazitapatikana bila kufanya kazi.

Rais Magufuli: Walisema nimemteua mtu anafanya kazi hotelini, waandishi wa habari naomba mpige picha cheti chake.
Cna uhakika kama alipitia jina kwa jina kama alivyo sema

Make kuna majina yanayojirudia kwenye teuz wakat alishasema hukuna kurundikiwa vyeo
 
Hongera sana mhe Rais kwa hotuba nzuri! Hongera pia kwa wakurugenz wateule!!

Hapa kazi tuuuu!!!
 
Kumbe anasoma/anapitia mitandao ya kijamii. Sasa mbona suala la binti yake mpendwa, Je.sca hajawahi kulifafanua ama kueleza ukweli licha ya kwamba limenadiwa sana mitandaoni kuliko hata hilo saga la Luhende? Au ndo tuamini kwamba ni kweli huyo binti ameingizwa Chuo Kikuu pasi kukidhi vigezo?
Swadaktaaaaaaaaaaaa,hili nalo neno,mkuki kwa nguruwe kwa mwanadamu uchungu.
 
Rais anasema hawezi kuchagua mtu ambaye hawezi kutekeleza sera ya chama cha Mapinduzi wala haamini katika Chama cha Mapinduzi sababu wananchi walichaguwa Chama cha Mapinduzi kutokana na uzuri wa ilani yake

Hapa wasomi wengi inabidi waelewe.Watendaji wote wa serikali wanatakiwa kuwa na ilani ya CCM ambayo ni Ilani ya chama tawala ili wajue kinataka nini.Napendekeza ilani za CCM zigawiwe kwa viongozi wote wa serikali.Ili wajue wakipanga mipango na kufanya kazi ziendane na ilani ya chama wasitunge vyao wanavyoota.

Pia wasomi wengine hawajui kutumia fursa.Fursa mojawapo ni kujiunga na chama tawala ambacho chaweza kukupa fursa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi ndani ya serikali nk wakikuona una uwezo na unafaa

Ukijiunga chama cha upinzani ni kupoteza wakati wako na fursa.Hivi unategemea Raisi achague mkuu wa wilaya au mkoa kutoka kijana aliye chama cha upinzani hata kama ana akili kuliko profesa yeyote? Katiba kwanza haimruhusu.Akimchagua mtu asiyeamini ilani ya CCM ataishia kumhujumu tu na kufanya kazi isivyoelekeza ilani.Ili uaminiwe lazima uwe muumini wa ilani ya CCM sio ya UKAWA ambayo haipo na haikushinda kwenye uchaguzi

Vijana wengi mwangalieni Mkuu wa mkoa MAKONDA ni kijana lakini aliyejitoa kufanya kazi na chama tawala huyo kapaa mkuu wa mkoa akiwa bado kijana kabisa.

Nina uhakika vijana kama akina Zitto Kabwe,John MNYIKA.Halima MDEE wangekuwa CCM siku nyingi wangeshakuwa mawaziri,wakuu wa mikoa na hata mabalozi wa Tanzania nje ya nchi.Lakini walipo mwisho wao ubunge!!!

Vijana wasomi harakisheni jiungeni CCM haraka ingieni jumuiya ya vijana wa CCM anzeni kuwa ACTIVE .Changamkeni kwenye maswala ya Chama onyesheni uwezo wenu huko

Msomi yeyote anatakiwa ajiweke mahali ambapo ana uhakika wa kwenda mbali.Chama tawala ndicho chaweza msaidia kufika mbali.(BIDHAA YOYOTE UNATAKIWA KUIWEKA MAHALI INAPOUZIKA -PRODUCT POSITIONING)

Nendeni matawi ya CCM yaliyo karibu jiungeni haraka CCM
 
Mshenzi
 
Walisema waende na vyeti vya ili vihakikiwe,sasa leo anasema anawajua wote. Ni kwanini alisema waende na vyeti wakati anawajua wote?
 
Jamani naomba kuuliza.... Nasikia Amekanusha kwamba wote hao wanasifa na anawafahamu , Je amekanusha kuhusu kuteua WAKURUGENZI AMBAO HAWAJAWAHI KUFANYA KAZI LOCAL GVT (TAMISEMI) AU CENTRAL GVT (SERIKALI KUU) !!!??? ..... Tanzania ingekuwa gari ningeshuka na nauli sidai.....
 
Back
Top Bottom