barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Rais JPM anahutubia Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji Ikulu Dsm
Moja ya jambo analosema limemsikitisha ni mitandao ya jamii kumuandika Luhende kama Msomi mwenye cheti cha hotel Management wakati ana Masters na alikuwa mkaguzi wa elimu wa kanda.
Rais anasema amepitia kwenye mtandao mmoja wa kijamii akaona comment za watu juu ya Luhende akabaki kucheka tu,amemsimamisha Luhende na kuwataka waandishi wa habari wampige picha na waende Sinza kumpiga picha Luhende Meneja wa Hotel na kuzisambaza mitanadaoni
Rais pia anasema anawafahamu Wakurugenzi wake wote,anasikia malalamiko kwenye mitandao ya kijamii,amewaambia wajishangilie wao na si kusikitika kwa kutokushangiliwa na mitandao ya kijamii,anasema hao wasioshangilia kwenye mitandao ni maadui zake,..."Watachonga sana lakini wataka kimya"
Rais anasema zamani nafasi za ukurugenzi zilikuwa "deal",na pale TAMISEMI kulikuwa na mtandao wa kuhongwa ili kuwapatia watu ukurugenzi,aliishagiza Waziri awaondoe wapo watatu pale utumishi ambao kazi yao ilikuwa kuhongwa na kugawa vyeo vya Ukurugenzi.
Rais anasema Wakurugenzi wote aliwapitia jina kwa jina na ndio maana hasafiri ili kufanya mambo yeye mwenyewe na wakati mwingine hulala hata saa nane ili kujiridhisha mambo.
Rais amepiga marufuku Wakurugenzi kutoa "tender" kwa Madiwani na Wanasiasa wafanyabiashara ambao hutumia nafasi zao kushinda zabuni,wapinge kodi ndogondogo kwa wananchi kama za kina mama wauza mchicha,ambao halmashauri zinadai kodi wakati hata mbolea wala mbegu hawakuwasaidia.Watumie madaraka ya kisheria kuwaondoa "watumishi" Miungu watu kwenye vijiji,kata,tarafa na wilaya.
Rais anasema hawezi kuchagua mtu ambaye hawezi kutekeleza sera ya chama cha Mapinduzi wala aamini katika Chama cha Mapinduzi sababu wananchi walichaguwa Chama cha Mapinduzi kutokana na uzuri wa ilani yake.Kwenye mitandao ya Kijamii anasikia kuwa watu wanalalamika anachaguaa watu wasio na "experience",anasema yeye hataki mambo ya ma-experience experience tu,hawezi kuchagua mtu mwenye experience wakati ni mwizi.Kuna watu walijipanga na kutuma "vimemo" ili watu wao wachaguliwe kwenye nafasi hizo,akawafutilia mbali wote waliotumwa na waliotuma.
Rais anasema hawezi kuchagua "vilaza",anajuwa kuna watu hawapendi neno vilaza ila yeye hawezi kufanya kazi na vilaza.Waandishi wapige picha cheti cha Luhende ili watu waongo wa mitandaoni washindwe na walegee.(Vi...la...za)
Rais anasema alistuka sana pale majina ya Wakurugenzi yalivyotoka hadharani na kuanza kuona ukosoaji mkubwa mitandaoni,kiasi akaanza kujiuliza nimekosea nini kuteuwa,akaanza kuwa na wasiwasi lakini baadae akajuwa ni maneno tu ya mitandaoni.
Mwisho Rais amewaasa Wakurugenzi wasikilize maneno ya watu na ya mitandaoni,waende kufanya kazi hata kama hawana uzoefu na kama ni uzoefu wataupata huko huko.Ndio maana katika Wakurugenzi waliokuwepo wamerudi 60+.Hakutaka kurudisha Wakurugenzi wezi na mafisadi eti kisa ni uzoefu.
Rais Magufuli: Haiwezekani tunahamasisha wafanyabiashara watumie EFD, lakini sisi serikali tusitumie.
Rais Magufuli: Ikiwezekana, Wakurugenzi waende na EFD kwenye halmashauri zao wakaanze kuzitumia kukusanya mapato.
Rais Magufuli: Wananchi wa chini wanateswa na kunyanyaswa na vikodi vya ajabu ajabu, nawaomba mkatatue kero zao.
Rais Magufuli: Kwa jinsi ninavyoona sura zenu hapa kweli naamini mnaenda kufanya kazi,kwani sura zinaonesha ninyi ndio wenyewe.
Rais Magufuli: Kuna watu wanalalamika fedha zimepotea, hazitapatikana bila kufanya kazi.
Rais Magufuli: Walisema nimemteua mtu anafanya kazi hotelini, waandishi wa habari naomba mpige picha cheti chake.
======