Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,217
- 2,354
Madhara ya vyama kutojiandaa ndiyo hayaKesho ndio siku ya kuapishwa mawakala wa vyama katika uchaguzi mkuu.
Tukumbuke kuwa wakala anaapa halafu anaondoka bila utambulisho wowote, yaani anaondoka kama mimi na wewe!
Eti wakala anaenda mikono mitupu kituo cha kupigia kura eti kujitambulisha kwa msimamizi wa uchaguzi ndio apewe barua ya uwakala?
Msimamizi wa uchaguzi atamtambuaje kama huyu ndiye yule aliyeapishwa?
Kwanza msimamizi wa uchaguzi atamuomba kitambulisho cha uraia au leseni ya udereva au pasi ya kusafiria ili atambue kuwa ni yeye -
1) Holaa, hana! anamkataa, anasema nitajuaje kama ni wewe! Mzozo unaanza! Anatolewa
2) Kama anavyo vitambulisho vitamulikwa kwa darubini kuhakikisha havitofautiana hata kidogo mpangilio wa majina au spelling ya jina. Kama kuna tofauti yoyote msimamizi anamkataa. Mzozo unaanza! Afande anapapasa AK47, wakala anatolewa!
Lengo la haya yote ni kuwachelewesha mawakala kuingia vituoni.
Simu zitapigwa weeee, mawakala wakija kukubalika ni baada ya masaa, hapo ujue kura bandia kibao zitakuwa zimeisha penyezwa.
Yaani CCM ni shiiiidaaaa!
Natabiri mzozo mkubwa mwanzo kabisa mwa kupiga kura.
TAHADHARI:
1). HAKIKISHA MWAKALA WANA VITAMBULISHO
2. HAKIKISHA MAJINA YA MAWAKALA MNAYOPELE KWA TUME YANAFANANA KWA MPANGILIO NA SPELLING KAMA VITAMBULISHO WALIVYONAVYO.
3). MAWAKALA MSIJESAHAU VITAMBULISHO VYENU IWE LESENI, PASPOTI, VYA NIDA, AU CHA KUPIGIA KURA, vinginevyo utatupiliwa mbali
Huo ni mtazamo wangu! We unasemaje!
Ufafanuzi huu ni kwa mujibu wa kifungu cha 57 (1) na (2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na kifungu cha 58 (1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292
Chama cha siasa kinaruhusiwa baada ya kupata ridhaa ya Mgombea au Wagombea kuteua na kuwasilisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi orodha ya majina ya mawakala wa upigaji kura siku saba (7) kabla ya siku ya uchaguzi
Ni vema mawakala wapangiwe vituo vya kupigia kura ndani ya kata wanayoishi ili waweze kuwatambua wapiga kura.
Kila chama cha siasa kitakuwa na wakala mmoja tu kwa kituo ambaye atawakilisha wagombea wa chama hicho kwa uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani katika kituo husika
Utambulisho wa Mawakala wa Vyama Vya Siasa
Kwa mujibu wa kanuni ya 50 (6) ya Kanuni Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 43 (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2020, barua ya utambulisho wa kila wakala itakayowasilishwa na chama iainishe kituo alichopangiwa na iambatishwe na picha mbili (passport size) zilizopigwa si zaidi ya miezi mitatu.
Aidha, kwa mujibu wa kifungu 57 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 chama kitaruhusiwa kuteua wakala mbadala endapo aliyeteuliwa awali amefariki au ameshindwa kutekeleza majukumu ya uwakala. Katika kurahisisha utekelezaji wa suala hili, sambamba na orodha ya mawakala wa vituoni, vyama viwasilishe majina mawili ya mawakala wa ziada kwa kila kata ambao watatumika kama mawakala mbadala iwapo itahitajika
Endapo wakala hana picha anaweza kuwasilisha nakala mbili za mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo: -
(i) Kadi ya mpiga kura;
(ii) Kitambulisho cha Taifa;
(iii) Leseni ya udereva; au
(iv) Pasi ya kusafiria. Baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kupokea utambulisho wa mawakala atafanya yafuatayo: -
(i) Ataandaa orodha ya mawakala kwa kila kituo.
(ii) Ataikabidhi orodha hiyo kwa Wasimamizi wa vituo pamoja na barua ya utambulisho yenye picha wakati wa kugawa vifaa. Kama barua haina picha iambatishwe na moja ya nakala za vitambulisho vilivyotajwa hapo juu.
(iii) Atawaelekeza Wasimamizi wa Vituo kubandika orodha ya mawakala watakayopatiwa nje ya kituo cha kupigia kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura.
(iv) Atawaelekeza Wasimamizi wa Vituo wasiombe utambulisho mwingine wowote kutoka kwa mawakala wa vyama. Tume inashauri uteuzi wa mawakala uzingatie uwiano wa kijinsi na makundi maalum kama vile vijana na watu walemavu.
Hata hivyo, vyama vya siasa vina mamlaka kamili juu ya uamuzi wa kuteua mawakala kwa kadri watakavyoona inafaa.