Vetting ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya itokane na maeneo wanapotoka kuharakisha maendeleo, wageni wanafubaza uchumi

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
WanaJF,

Niliposoma katiba ya Kaji waliomba ilichagiza Zaidi wateule wa Rais watokane Na mikoa yao. Hii inaleta maana kwamba Ni rahisi wananchi wa sehemu hiyo kupata mwakilishi mzuri Na Kwa kuwa anakuwa anafahamu vizuri maeneo Ni rahisi kuondoa migogoro ya kwao kuliko kuleta Mgeni asiyefahamu maeneo husika.

Mikoa ya mara, Morogoro, ruvuma, mtwara, kagera Kuna chamoto nyingi Za migogoro ya hapa Na pale, pengine Ni rahisi kama mkuu wa Mkoa na kamati yake wanaweza kusikilizwa Zaidi. Mfano JPM alivyokuwa anazunguka amekutana Na dhuruma nyingi akazitatua, hizi zimetokana Na rushwa au kutokujari Kwa vile hayawahusu.
 
Tuna imani na wataalamu wa vetting walio tuletea 1st son in law na Mwesiga. Msiwafundishe kazi.
 
Nadhani mleta mada anatuletea tu kwa uchache namna utekelezaji wa sera ya majimbo kama ulivyopendekezwa na makamu mwenyekiti wa Chama chake Bwn. tundu kisu.
 
Mkuu wa mkoa/wilaya ni mwakilishi wa Rais kwenye hayo maeneo. Anasimamia maslahi ya eneo lakini pia anasimamia maslahi ya taifa kwenye hilo eneo.

Labda ushauri tuongeze nguvu kwenye local government; meya na wenyeviti wa halmashauri etc, maana ndio wanatokana na wananchi.
 
Mleta mada nimekuelewa. Nafikiri kinachotakiwa ni kuwa na kiongozi mkubwa wa kimkoa mwenye nguvu aliyetokana na wananchi na awenanguvu kama alizonazo mkuu wa mkoa na zaidi. Tuachane na hawa viongozi wa kisiasa ambapo ni mkuu wa mkoa/wilaya - Iringa at the same time anajipanga kugombea Ubunge kwao Mtwara.
 
Ndiyo maana yangu nimekosea uwasilishaji
 
Kama tukiwa tunafanya kazi hasa za kiuongozi kwa mawazo haya, basi taifa litapotea na ubaguzi utarejea na si ajabu hata ukabila ukazaliwa upya, maendeleo hayaji kwa sababu ya uzawa.
 
Kuna mameya wa majiji,manispaa na wenyeviti wa halmashauri labda hawa wapewe power maana wao wanatokana na eneo husika na pia wetokana na wananchi,lakini kwa RC's na DC'S ni wawakilishi wa Rais katika eneo husika yeye ndiye anaelewa flani anaweza kuniwakikisha sehemu flani vizuri,ukisema uteuwe mkuu wa mkoa mwenyeji wa eneo husika uwakilishi wake kwa mamlaka ya uteuzi unakuwa mgumu kiutendaji.
 
Mabwana wale wa serikali za majimbo wamekuja kwa gia nyingine.
Serikali Za majimbo mzuri ndio maana marekani kumeendelea. Ukiangalia Kwa umakini uwezi kumchukua mtu wa dodoma mgogo akapaendeleza Musoma au Kilimanjaro.
 
Kama tukiwa tunafanya kazi hasa za kiuongozi kwa mawazo haya, basi taifa litapotea na ubaguzi utarejea na si ajabu hata ukabila ukazaliwa upya, maendeleo hayaji kwa sababu ya uzawa.
Uzawa Unaweza kuleta maendeleo Kwa sababu zifuatazo.
1. Mtu ataogopa kuharibu Kwa kuwa kizazi chake kitapata laana ikiwa anaharibu kwao.
2. Watu Kuimalisha kwao hakuleti ubaguzi kwani Nani anabaguliwa , ikiwa maeneo mengine wanatakiwa kuiga juhudi Za mikoa iliyoendelea mfano mikoa mingi inavyoiga maendeleo ya Mkoa Kilimanjaro.
 
WanaJF,

Niliposoma katiba ya Kaji waliomba ilichagiza Zaidi wateule wa Rais watokane Na mikoa yao. Hii inaleta maana kwamba Ni rahisi wananchi wa sehemu hiyo kupata mwakilishi mzuri Na Kwa kuwa anakuwa anafahamu vizuri maeneo Ni rahisi kuondoa migogoro ya kwao kuliko kuleta Mgeni asiyefahamu maeneo husika.

Mikoa ya mara, Morogoro, ruvuma, mtwara, kagera Kuna chamoto nyingi Za migogoro ya hapa Na pale, pengine Ni rahisi kama mkuu wa Mkoa na kamati yake wanaweza kusikilizwa Zaidi. Mfano JPM alivyokuwa anazunguka amekutana Na dhuruma nyingi akazitatua, hizi zimetokana Na rushwa au kutokujari Kwa vile hayawahusu.
ujinga mtupu, pumba, mnajidai mnaakili sana, yote hii ni akili ya kung'anga'nia madaraka na ubinafsi
 
Back
Top Bottom