'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Dah!..haya bhana
Jamaa umenifurahisha.....ila ukweli ni kwamba hili somo liko complex sana. Na miaka ijayo binadamu anaweza kuwa wa tofaut sana na sasa.

Hapa napendekeza kwako kitabu kinaitwa Homodeus- a brief history of tomorrow. Unaweza kucheck lectures zake kwenye you tube.

Hakika yajayo yanashangaza mno...alot is goin on...!
 
Daah, at last kuna mtu anaetumia akili walau kidogo
Asante...watu wengi wameathirika sana na mafunzo ya dini. Jambo moja hawafikri ni kwamba kwa zaidi ya karne mbili..dini haijawahi kuja na jambo jipya zaidi ya kujifunga katika mambo ambyo hali halisi inanonesha vinginevyo.

Sipingi uwepo wa Mungu...lakin pengine original creation haikuwa mtu kabsa....sijui ilikuwa kitu gan...kwasababu hata leo ukiwaangalia wanadamu hawafanani kwa asilimia mia....so somehow walibadilika sana....kutoka yule mmoja....be it kitu au mtu...but not necessary mtu...!

Nafikiria tu...!
 
Scientific unge kuwa approved kama ungeweka na picha . so unadhan tumetokea wap
Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.

Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.

Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!

=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================

Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
 
akili za bangee
 
Acha miaka, wewe nenda gym kwa miezi miwili tu, mwili wako utabadilika kulingana na mazingira mapya ya mazoezi magumu, misuli ya mwili itaimarika.., ila kuna changes za muda mrefu ambazo hutumia hata miaka milioni 200 na kuendelea.., mfano kuna samaki wanaotembea ardhini kisha wanarudi majini, yaani yale mapezi yao wanayatumia kama miguu. Ina hata vijana wa 1980's na 2000's wanavyotofautiana kwa urefu, hii ni kwa sababu ya kubadilka kwa mazingira ya lishe, siku hizi blueband kwa wingi..
Hicho kitu kinaitwa ADAPTATION tofautisha ADAPTATION na EVOLUTION evolution ni permanent but adaptation ni temporary,na hii ni ili mwili uweze kuendana na mazingira.
 
Siamini kwenye vestigial organs nijuavyo kila kitu kwenye mwili wa kiumbe kina kazi hata kama si inayoonekana
"HATA KAMA SI INAYOONEKANA"
Ni unfalsifiable assumption
Yaani Hoja yako imejikita katika dhana ambayo Milele haiwezi kuthibitishwa
Na kwa mantiki hio...Mtu anaweza kusema chochote bila kupigwa
"Mimi Naamini Kati ya Sayari ya Mars na Dunia Kuna Kasri la Zamani ambalo hatuwezi kuliona Wala kulitambua kwa njia yoyote ile"
Utanipinga vipi?Huo ndio ubaya wa Unfalsifiable Assumption
Kwa ufupi....Hoja yako ni Utumbo mtupu
 
Sasa humu kuna wanasayansi wa Jamiiforums. Wajuaji wa kila kitu na wataalamu wa anatomy, genetics, na evolution.

Wengine hata hiyo "vestiges" hawajui maana yake lakini wamo humu wanashusha nondo zao za kisayansi.

Evolution yenyewe walifundishwa sekondari huko kwenye shule za vumbi zisizojulikana hata jina. Tandahimba huko ndani ndani maporini. Lakini nao wamo humu wanashusha madini ya kufa mtu.

Jamani, hii ndio Tanganyika!
 
Duh, mbona siku hz evolution haiendelei??
Watu wanaivolve.Huoni wachina brain yao ime evolve kutoka watu wanaotengeneza penseli na vichongeo mpaka satellite.Waafrika Tupo njiani bado akili zetu zipo njiani kuelekea huko kwa wachina na wazungu,tusitumie nguvu sana akili yenyewe itabadirika tu,tume evolve ktk physiki ya mwili bado ubongo.Mzungu hajaivolve ktk fiziki bali akil.Misuli yetu ipo vizuri
 
Hicho kitu kinaitwa ADAPTATION tofautisha ADAPTATION na EVOLUTION evolution ni permanent but adaptation ni temporary,na hii ni ili mwili uweze kuendana na mazingira.
Ndio nikasema adaptation ni changes za muda mfupi na haziwi invluded kwenye genome, hizo adaption / changes kama zitakuja as a result of chance mutation na kisha zikawa naturally selected over thousands+ of years basi hapo evolution inatokea, angalia tembo wenye pembe ndogo wanavyoongezeka.
 
"HATA KAMA SI INAYOONEKANA"
Ni unfalsifiable assumption
Yaani Hoja yako imejikita katika dhana ambayo Milele haiwezi kuthibitishwa
Na kwa mantiki hio...Mtu anaweza kusema chochote bila kupigwa
"Mimi Naamini Kati ya Sayari ya Mars na Dunia Kuna Kasri la Zamani ambalo hatuwezi kuliona Wala kulitambua kwa njia yoyote ile"
Utanipinga vipi?Huo ndio ubaya wa Unfalsifiable Assumption
Kwa ufupi....Hoja yako ni Utumbo mtupu
Excellently handled...!!😅😅😅😂😂😂
 
Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
Hii mpya kwangu kwenye elimu ya sayansi ya viumbe. Naweza kupata ufafanuzi wa kina wa kisayansi juu ya hili?
 
Sasa humu kuna wanasayansi wa Jamiiforums. Wajuaji wa kila kitu na wataalamu wa anatomy, genetics, na evolution.

Wengine hata hiyo "vestiges" hawajui maana yake lakini wamo humu wanashusha nondo zao za kisayansi.

Evolution yenyewe walifundishwa sekondari huko kwenye shule za vumbi zisizojulikana hata jina. Tandahimba huko ndani ndani maporini. Lakini nao wamo humu wanashusha madini ya kufa mtu.

Jamani, hii ndio Tanganyika!
Hata kama mtu alisoma mavumbini.Kama amesoma vitabu atajua tu sawa na aliesoma kwenye sofa.Tomas Edson hata mavumbini hakusoma lakini ndio mwanasayandi mbunifu mkubwa sana.Katika dunia ya Leo huituitaji sana kuka saana darasani.simu ya mchina tu inatosha kuwa sawa na profesa wa miaka ya 90.Kuna mabilioni ya vitabu,maelfu ya lecture,simulation,jf,quora,websites,facebooks,blogs,picture,documentary,articles yaani mi utashi wa mtu kuamu ajue niini na asijue nini.Zamani ukitaka kuwa mjuaji mpaka uende maktaba,sasa hivi maktaba zote duniani zipo google.
WEWE bado unawaza ktk mifumo ya miaka mitano,kumi iliopita sasa hivi kuna evolution of knowlogde.
 
Hoja yako haiondoi uumbaji,ila inafafanua uumbaji kwamba ni process ambayo ni endelevu
😂😂😂
"Don't move the goal post Bro"
Evolution na Uumbaji ni vitu viwili tofauti
Evolution inatengeneza species through trials and Errors....Aina ya specie itakayo withstand hayo Mabadiliko ndio itakua naturally selected kwenda Kizazi kingine
So haipo perfect Mara zote....Ukipata mda Soma kuhusu 'Poor design in nature'
Je Mungu mkamilifu anaweza vipi kutumia Mchakato wa bahati nasibu Kama Evolution?
Nadharia ya Uumbaji inadai kila kitu kiliumbwa kikiwa kamili Kama ilivyo Sasa...Kugundulika kwa ushahidi Tena Mwingi tu unaothibitisha vinginevyo ni ushahidi tosha kuwa hatukuumbwa na Mungu Hana Nafasi katika Evolution

Na hio ndio Hoja ya Msingi wa Mtoa Mada
 
Sasa humu kuna wanasayansi wa Jamiiforums. Wajuaji wa kila kitu na wataalamu wa anatomy, genetics, na evolution.
Wengine hata hiyo "vestiges" hawajui maana yake lakini wamo humu wanashusha nondo zao za kisayansi.
Evolution yenyewe walifundishwa sekondari huko kwenye shule za vumbi zisizojulikana hata jina. Tandahimba huko ndani ndani maporini. Lakini nao wamo humu wanashusha madini ya kufa mtu.
Jamani, hii ndio Tanganyika!
Wewe yawezekana kabisa ni Mzee wa Miaka ya 60
Kipindi ambapo Msomi pekee wa kumuamini ni yule Aliyepata shahada yake Ughaibuni au Mtoto wa Chief Aliyepata Nafasi kusoma shule ya Seminary
Au ndio mnao amini kuwa kuna Shule za kata na wenye Vipaji
Dunia imebadilika.....Elimu yoyote utayohitaji unaipata kwenye keyboard ya Simu janja yako
Ni Wewe tu na Mda wako
Evolution ni ile ile hata ukifundishwa chini ya Ardhi
au ya Mti.... Science ni Universal
Haitegemei ulipo au unafundishwa na nani au Unajifunza kwa njia ipi
Mijitu Kama nyie Inayo amini kwenye huo mfumo unaoitwa rasmi wa Elimu,wa Mtu kusoma Miaka 16 ndio aitwe Msomi ndio chanzo kikubwa Cha kuwa na Wasomi wa hovyo vyuo kikuu
 
Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom