'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
35,845
40,433
Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.

Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.

Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!

=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================

Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
=============================

=================================
Update: 27/08/2021
Mifupa ya nyangumi mwenye miguu ‘dating millions of years ago’ yapatikana.

4B937FF1-DA23-45FB-9A71-39FE5C3725EA.jpeg

_______________________________
WaChina ni WaAfrika waliohama na kubadilika kutokana na mazingira

Kwahiyo wamaanisha pia miaka ijayo,tutakuja kuwa viumbe tofauti na tulivyo sasa?...
Acha miaka, wewe nenda gym kwa miezi miwili tu, mwili wako utabadilika kulingana na mazingira mapya ya mazoezi magumu, misuli ya mwili itaimarika, ila kuna changes za muda mrefu ambazo hutumia hata miaka milioni 200 na kuendelea, mfano kuna samaki wanaotembea ardhini kisha wanarudi majini, yaani yale mapezi yao wanayatumia kama miguu. Ina hata vijana wa 1980's na 2000's wanavyotofautiana kwa urefu, hii ni kwa sababu ya kubadilika kwa mazingira ya lishe, siku hizi blueband kwa wingi..
 
Acha miaka, wewe nenda gym kwa miezi miwili tu, mwiki wako utabadilika kukingana na mazingira mapya ya mazoezi magumu, misuli ya mwili itaimarika.., ila kuna changes za muda mrefu ambazo hutumia hata miaka milioni 200 na kuendelea.., mfano kuna samaki wanaotembea ardhini kisha wanarudi majini, yaani yale mapezi yao wanayatumia kama miguu..
Wazani io ya gym mabadiliko yake yanahusiana chochote na kilichoong3lewa kwenye mada ya thead?

Kwahiyo mfano binadamu wa sasa na yule wa miaka ilee unaemsema alikua na mkia,genetically do you think they were related or are they still in the same specie?
 
Nimekutolea mfano kukuonyesha adaptive capabilities za viumbe, lakini ili mabadiliko yaweze kufikia hadi kwenye ngazi ya vinasaba huwa inachukua hadi miaka milioni 200 na kuendea..
 
Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
 
Huko kujiburudisha kwa mijusi,ndio kazi yenyewe,ya hivyo viungo.
Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
 
Acha miaka, wewe nenda gym kwa miezi miwili tu, mwili wako utabadilika kulingana na mazingira mapya ya mazoezi magumu, misuli ya mwili itaimarika.., ila kuna changes za muda mrefu ambazo hutumia hata miaka milioni 200 na kuendelea.., mfano kuna samaki wanaotembea ardhini kisha wanarudi majini, yaani yale mapezi yao wanayatumia kama miguu. Ina hata vijana wa 1980's na 2000's wanavyotofautiana kwa urefu, hii ni kwa sababu ya kubadilka kwa mazingira ya lishe, siku hizi blueband kwa wingi..
kwahyo kwasababu miili ya watu inatanuka wakifanya mazoezi....na samaki wanatembea ardhini kisha wanarudi majini....na vijana wa 2000's wana maumbile madogo kuliko wazee wa 1980's na lishe nyingi pamoja na matumizi ya blueband n.k je wamekuwa viumbe wengine wapya?!

huyo mtu anaekwenda gym ana mabadiliko gani kutoka kwenye ubinadamu wake zaidi ya kuwa mfano wa funguo ya tri-cycle?!.
huyo samaki amebadilika nini kutoka kwenye usamaki wake...?!..

huyo kijana wa 2000's ana nini kipya zaidi ya kuwa ni offspring ya haohao wazee wa 1980's....

kabla ya kwenda kusoma ombeni sana ufahamu mzuri na si kukariri takataka nyingi kichwani.....kulima kungekuwa bora kwenu kuliko kusoma.
 
Nimekutolea mfano kukuonyesha adaptive capabilities za viumbe, lakini ili mabadiliko yaweze kufikia hadi kwenye ngazi ya vinasaba huwa inachukua hadi miaka milioni 200 na kuendea..
huyo mwanadamu existence yake hapa duniani wala haina miaka elfu 40 bado....hiyo elfu 25 yenyewe kuna walakini.....sasa hizi milioni 200 n.k sijui huwa mnazitoa wapi..
 
Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom