'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Umesema kuwa Kama kiungo hakitumiki hupotea chenyewe.
Swali: Ni vipi Hawa masista na mapadre ambao hawajamiiani/hawazai. Je mfumo wao wa uzazi unapotea mwilini mwao? Yaani nyeti zao hubaki kwaajili ya kukojoa na kunya tu?
maswali haya ni mazuri sana ila akijibu uniite
 
Umesema kuwa Kama kiungo hakitumiki hupotea chenyewe.
Swali: Ni vipi Hawa masista na mapadre ambao hawajamiiani/hawazai. Je mfumo wao wa uzazi unapotea mwilini mwao? Yaani nyeti zao hubaki kwaajili ya kukojoa na kunya tu?
Mabadiliko ya kiwango cha vinasaba vinachukua millions of years, hao masista mapadre sio tu kwamba viungo vyao vitapotea, ni kwamba genetics zao hazitakuwa passed on kwa vizazi vijavyo, kwahiyo wanapokufa na wao na kizazi chao na vinasaba vyao vyote ndio vinakwenda na maji
 
Sasa hao wanyama walokuwepo mwanzo walitokana vipi?
Viumbe wote inavyoonekana tulikuwa na ancestor mmoja ambae alikuwa ni single celled organism, na aka-develop into more complex forms na viumbe vika branch out kutokea hapo. Itakuwa Mungu aliumba huyo kiumbe wa kwanza na akaacha evokution iendelee tokea hapo.
 
Mabadiliko ya kiwango cha vinasaba vinachukua millions of years, hao masista mapadre sio tu kwamba viungo vyao vitapotea, ni kwamba genetics zao hazitakuwa passed on kwa vizazi vijavyo, kwahiyo wanapokufa na wao na kizazi chao na vinasaba vyao vyote ndio vinakwenda na maji
google helper Jibu hili hapa
 
Wew umesoma biology baada ya kumaliza chapter zako unajiona bonge la mjanja.mimi nakukushauri hivyo vidole vya mikono uwe unajipiga midole matakon labda ndio kazi yake ili uwe unajiburudisha ,kwa sababu zamani watu walitumia vidole vya mikono kuchimbia ,kulimia nk View attachment 1200467
Viungo vya uzazi kazi yake ni uzazi, ila kwakuwa hao mijusi wamegundua namna mpya ya kuzaliana (wame-evolve) kwa kuweza kujiclone naturally basi hizo zana za kuzaliana zikawa zimebaki kama 'vestiges', yaani kwao hazifanyi tena ile kazi ambayo kwa wengine walivyonavyo inafanya, na hawa mijusi wote wanakuwa ni majike sababu wote hutaga mayai yenye clone ya vinasaba vyao, sasa kwakuwa bado kuna conditioned reflex za kujamiiana ambazo bado hazijapotea moja kwa moja, kuna wakati jike mmoj anajifanya kama dume na wanajiburudisha kwa namna hiyo, ila haina any results kwamba anarutubisha mayai or anything else for that matter.
 
Hiyo simu au computer unayotumia kuandika kuna aliyeitengeneza au nayo imeibuka yenyewe?
Wapi nimesema kiumbe cha kwanza hakijaumbwa, ninachosema ni kwamba viumbe hai vilikuwa na ancestry moja (ambayo iliumbwa ofcourse), ila aka evolve na kubranch out kuwa viunbe vingi vilivyopo leo.
 
Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.
Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.
Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!
=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================
Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
Hata wewe mwenyewe "as a whole" ni "vestige".
 
Mimi naamini viungo vyote niloumbwa navyo vina kazi na umuhimu, anayehisi ana viungo visivyokuwa na kazi avitoe tu, atapata practical evidence ya hoja zake.
Madaktari huwa wanakata appendix wagonjwa wa appendicitis kila siku
 
evolution theory...haina nafasi katika mizani ya kielimu achilia mbali akili na utambuzi makini....mbwa aliumbwa akiwa mbwa.....paka,kuku,dagaa n.k...lakini wazungu wanawaingiza mjini kwamba ninyi waafrika ndo mlibadilika kutoka kwenye jamii ya nyani kuwa mlivyo leo....na bila soni mnashangilia...
Niambie, mifupa ya miguu inafanya nini ndani ya mwili wa nyangumi asiye na miguu?
 
mkuu ww elimu inakupa uchizi maana hata kujiuliza swali dogo tu kwamba hiyo origin( mwanzo wa yote) kabla ya kuanza kubadilika ilitokea wapi ??. ukivuta bangi ujue kujicontroll utawehuka
Probably Mungu aliumba kiumbe cha kwanza ambacho kilikuwa single celled na kika-evolve na kubranch out kuwa viumbe vyote tunavyovijua leo.
 
mkuu ww elimu inakupa uchizi maana hata kujiuliza swali dogo tu kwamba hiyo origin( mwanzo wa yote) kabla ya kuanza kubadilika ilitokea wapi ??. ukivuta bangi ujue kujicontroll utawehuka
Probably Mungu aliumba kiumbe cha kwanza ambacho kilikuwa single celled na kika-evolve na kubranch out kuwa viumbe vyote tunavyovijua leo.
hata kama babu yake ni sokwe ajibu sokwe alitokea wapi ??? mbona leo sokwe hawageuki binadamu ?
Pia mabadiliko ya kiwango cha vinasaba huweza kuchukua mamiliini ya miaka, kwahiyo usitegemee kuona sokwe akibadilika ndani ya uhai wako, wanaweza kuja kuwa the next super species na wao wakatuona sisi ndio kama manyani..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom