'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Kila kiumbe kimeumbwa kwa namna yake.Kwaiyo kila kiumbe kilivyo ndivyo kilivyotakiwa kuwa.Na Mungu ndiye dizaina na injinia wa hivyo vyote.Zaidi ya hapo ni porojo tu za watu.
Hakuna aliyebisha, ila si uumbaji wa kila kitu kwa muda huo huo, bali viumbe vili-branch out toka kwenye aina moja ya kiymbe na kuwa vingi tofauti. Niambie kwa mfano, mifupa ya miguu inafanya nini kwenye mwili wa nyangumi asiye na miguu?
 
Umesema kuwa Kama kiungo hakitumiki hupotea chenyewe.
Swali: Ni vipi Hawa masista na mapadre ambao hawajamiiani/hawazai. Je mfumo wao wa uzazi unapotea mwilini mwao? Yaani nyeti zao hubaki kwaajili ya kukojoa na kunya tu?
 
Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.
Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.
Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!
=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================
Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
Sasa hao wanyama walokuwepo mwanzo walitokana vipi?
 
Mimi naamini viungo vyote niloumbwa navyo vina kazi na umuhimu, anayehisi ana viungo visivyokuwa na kazi avitoe tu, atapata practical evidence ya hoja zake.
 
Ofcourse binadamu hana miaka milioni 200,ila ancestry iliyokuja kuevolve na kuwa viumbe vingi including binadamu ilikuwepo..
Evolution theory...haina nafasi katika mizani ya kielimu achilia mbali akili na utambuzi makini....mbwa aliumbwa akiwa mbwa.....paka,kuku,dagaa n.k...lakini wazungu wanawaingiza mjini kwamba ninyi waafrika ndo mlibadilika kutoka kwenye jamii ya nyani kuwa mlivyo leo....na bila soni mnashangilia.
 
Mkuu wewe elimu inakupa uchizi maana hata kujiuliza swali dogo tu kwamba hiyo origin( mwanzo wa yote) kabla ya kuanza kubadilika ilitokea wapi? Ukivuta bangi ujue kujicontroll utawehuka
 
ushauri mzuri sana kwake ebu print alafu kabandike mlangoni kwake nakuja kulipa gharama.
Kwahyo kwasababu miili ya watu inatanuka wakifanya mazoezi....na samaki wanatembea ardhini kisha wanarudi majini....na vijana wa 2000's wana maumbile madogo kuliko wazee wa 1980's na lishe nyingi pamoja na matumizi ya blueband n.k je wamekuwa viumbe wengine wapya?!..
huyo mtu anaekwenda gym ana mabadiliko gani kutoka kwenye ubinadamu wake zaidi ya kuwa mfano wa funguo ya tri-cyle?!..
huyo samaki amebadilika nini kutoka kwenye usamaki wake...?!..
huyo kijana wa 2000's ana nini kipya zaidi ya kuwa ni offspring ya haohao wazee wa 1980's....
kabla ya kwenda kusoma ombeni sana ufahamu mzuri na si kukariri takataka nyingi kichwani.....kulima kungekuwa bora kwenu kuliko kusoma..
 
Hakuna aliyebisha, ila si uumbaji wa kila kitu kwa muda huo huo, bali viumbe vili-branch out toka kwenye aina moja ya kiymbe na kuwa vingi tofauti. Niambie kwa mfano, mifupa ya miguu inafanya nini kwenye mwili wa nyangumi asiye na miguu?
kwa hiyo haina kazi inamuumiza tu eenh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom