Very soon, Tanzania is going to face political instability and great transformation

Hyo siku yaja. Wakaiba uchaguzi wamekalia viti wakijineemesha kweli kweli huku maisha ya wananchi yakiwa hoi taabani. Juu ya yote ajira,zikiwa hamna na wale waliokula mema ya nchi wakirudshwa kwenye vyeo. Wasomi wakijibiwa wajiajili huku watawala wakiwapa kazi watoto wao na jamaa zao.
Huku mitaani wakiongeza kodi za bidhaa ama tozo hali vipato vya wananchi vikinyong,onyeaa chini kabsaaa. Hali si hali, Hakika siku yaja, siku hyoo ardhi itawapasukia waingie ndani but hawatakua na nguvu za kipenya nyufa wajifiche. Nyakati zao zaja!!
 
Kama unga ulifika kilo 2200 hatukuandamana, kama ajira zilistop na biashara zikadorora hatukuandamana, vifaa vya ujenzi mfano cement ikatoka 8000 mpaka 15000 hatukuandamana, sukari ikatoka 1600 mpaka 2500 hatukuandamana, tozo zimewekwa kwenye miamala hatukuandamana, local channel hazionekani baadhi ya ving'amuzi hatukuandamana. Mbowe na Lissu wamefanyiwa yao hatujaandamana ni kipi kipya kitatufanya tuandamane?
Ni hayo hayo yatatufanya tuandamane. Unapochokoza mara ya kwanza unaweza kusamehewa, mara ya pili pia au hata ya tatu na nne, lakini mtu akishachoka basi atafanya chochote tu. Nakubali kwamba watanzania wanaweza kuchoka na kufanya maajabu na huo ukawa ndio mwanzo wa watu kuheshimiana nchi hii. Mara nyingi watu huheshimiana baada ya tifu.
 
Wanalijua hilo fika na ili kuwa Pro-active ama kuokoa jambo hilo wanaona threat ni CDM, sasa mpango ni kumfunga Mbowe na kuifuta CDM hii itakuwa ndiyo dawa ya kudumu.

Sasa hatujui if this will work out.
 
Sio kwamba nasapoti serikali au kwamba naridhishwa na hali ilivyo, LAKINI KWA WATZ WALIVYO WAOGA, TUSAHAU KUHUSU HILO ANALOSEMA MLETA UZI
 
Wabongo tu waoga kinyama, tunasubiri Roma au Ney wa mitego waimbe wimbo wa kiharakati ndo tuanze kusema AISEE JAMAA KAWACHANA KINOMA!!!
 
Nayaona mabadiliko makubwa ya kidemokrasia nchini yatakayoambatana na vurugu zitakazosabsbishwa na watu waliochoka kunyanyaswa,kutishiwa, kubambikiwa kesi na kupigwa. Kuna vuguvugu kubwa linakuja siku za usoni, watu hawajakasirika bado lakini muda siyo mrefu watalazimika kukasirika.

Hili halihitaji utabiri wa kinyota lakini kuna kitu ndugu zangu wanausalama wanaita situational analysis, Kama kweli wana situational awareness watazame tu uhalisia wenye watapata majibu. Ukiona taifa limefikia hatua ya watu kutishwa mabomu ya polisi hawaogopi, wanaharakati hawaogopi kulala mahabusu na hata kufungwa jela kwa yale wanayoyaamini basi mamlaka zinapaswa kusoma alama za nyakati na kukubali tu likae kwenye mstari na kuwasikiliza wananchi. Hakuna dola iliyowahi kushinda wananchi walio na hasira duniani, hakuna hicho kitu.

Kama unaamini kwamba hapa naandika kwa kujifurahisha basi waswahili husema kua muda ni mwalimu mzuri.

Hili taifa lilishaanza kujengwa katika misingi ya kidemokrasia muda mrefu huwezi kufananisha na Uganda na Zimbabwe ya Mugabe. Sidi kwetu tofauti ya kiitikadi ni kubwa na ndiyo iliyozaa tofauti kubwa ya kimawazo.

Watawala wetu wasizibe masikio kwa kutamani kuendelea kutawala.
Mkuu umenana vyema, ngoja machokoraa ya UVCCM yatakavyokuja mbio humu kukushambulia
 
ukapige mswaki sasa
 
Wananchi hao waliochoka walikuwa wapi miaka yote? Au unazungumzia Tanzania ya ndotoni?
Mkuu angalia Eswatin utawala wa kifalme ulikuwa hauguswi wala kuhojiwa kwa miaka mingi.Leo hii maandamano ni makubwa hadi watawala hawaamini kinachotokea.

Unajua kama SADC wanatuma ujumbe wao nchini Eswatin kuzungumzia hali ya mambo?
 
Kama unga ulifika kilo 2200 hatukuandamana, kama ajira zilistop na biashara zikadorora hatukuandamana, vifaa vya ujenzi mfano cement ikatoka 8000 mpaka 15000 hatukuandamana, sukari ikatoka 1600 mpaka 2500 hatukuandamana, tozo zimewekwa kwenye miamala hatukuandamana, local channel hazionekani baadhi ya ving'amuzi hatukuandamana. Mbowe na Lissu wamefanyiwa yao hatujaandamana ni kipi kipya kitatufanya tuandamane?
Waoga huwa hawaandamani Wala kusema. Siku ikifika wao hufanya tu.
 
Mleta uzi anajipa matumaini hewa tu
Kama unga ulifika kilo 2200 hatukuandamana, kama ajira zilistop na biashara zikadorora hatukuandamana, vifaa vya ujenzi mfano cement ikatoka 8000 mpaka 15000 hatukuandamana, sukari ikatoka 1600 mpaka 2500 hatukuandamana, tozo zimewekwa kwenye miamala hatukuandamana, local channel hazionekani baadhi ya ving'amuzi hatukuandamana. Mbowe na Lissu wamefanyiwa yao hatujaandamana ni kipi kipya kitatufanya tuandamane?
 
Mkuu angalia Eswatin utawala wa kifalme ulikuwa hauguswi wala kuhojiwa kwa miaka mingi.Leo hii maandamano ni makubwa hadi watawala hawaamini kinachotokea.

Unajua kama SADC wanatuma ujumbe wao nchini Eswatin kuzungumzia hali ya mambo?
Mkuu nikuhakikishie tu kwamba Watanzania wamelala usingizi wa pono. Wao hawaelewi chochote zaidi ya amani hata ikiwa watakanyagwa na kupondwapondwa kichwani wao kwao ni hewalla tu. Labda unazungumzia Watanzania wa Kusadikika.
 
Back
Top Bottom