Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 987
Nayaona mabadiliko makubwa ya kidemokrasia nchini yatakayoambatana na vurugu zitakazosabsbishwa na watu waliochoka kunyanyaswa,kutishiwa, kubambikiwa kesi na kupigwa. Kuna vuguvugu kubwa linakuja siku za usoni, watu hawajakasirika bado lakini muda siyo mrefu watalazimika kukasirika.
Hili halihitaji utabiri wa kinyota lakini kuna kitu ndugu zangu wanausalama wanaita situational analysis, Kama kweli wana situational awareness watazame tu uhalisia wenye watapata majibu. Ukiona taifa limefikia hatua ya watu kutishwa mabomu ya polisi hawaogopi, wanaharakati hawaogopi kulala mahabusu na hata kufungwa jela kwa yale wanayoyaamini basi mamlaka zinapaswa kusoma alama za nyakati na kukubali tu likae kwenye mstari na kuwasikiliza wananchi. Hakuna dola iliyowahi kushinda wananchi walio na hasira duniani, hakuna hicho kitu.
Kama unaamini kwamba hapa naandika kwa kujifurahisha basi waswahili husema kua muda ni mwalimu mzuri.
Hili taifa lilishaanza kujengwa katika misingi ya kidemokrasia muda mrefu huwezi kufananisha na Uganda na Zimbabwe ya Mugabe. Sidi kwetu tofauti ya kiitikadi ni kubwa na ndiyo iliyozaa tofauti kubwa ya kimawazo.
Watawala wetu wasizibe masikio kwa kutamani kuendelea kutawala.