VENGU (Joseph Shamba) anaumwa, kalazwa Muhimbili tumuombee na kumjulia hali

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,985
2,770
Nawasalimu wote hasa wale wenye moyo wa huruma na upendo kwa wenzetu wahitaji. Nimekwenda Muhimbili Jana kwenye Wodi ya Mwaisela namba 1. Lengo langu lilikuwa kumjulia hali Msanii wa Komedi VENGU baada ya kutokumuona kwenye kipindi muda mrefu na kusikia amelazwa Muhimbili.

Niliwakuta Ndugu zake ambao walinikaribisha kwa upendo katika kumjulia hali Ndugu yao. Jamani kusema ukweli Yule kijana anaumwa na anahitaji Sala na Maombi yetu. Hatambui mtu wala hawezi kuongea. Waliniambia kwa sasa wanashukuru mungu ana nafuu baada ya kukaa ICU muda mrefu tangu Masanja alivyokuwa anasema Jembe lake linaumwa bila kufafanua.

Nawaombeni mwenye nafasi , hali na mali akamjulie hali Kijana huyu. Alituburudisha wengi kwa USANII wake wa KOMEDI tulicheka alipokuwa Mzima. Na sasa tukamuone hospitali kwani ni jambo la dhawabu kumuona mgonjwa. Wengi labda walikuwa hawajui kalazwa wapi ni MUHIMBILI, Mwaisela WARD 1.

Labda tunaweza kuomba serikali iingilie kati Ugonjwa wake naye wampeleke INDIA ili arudi Chuoni na Kazini kwake. Mungu amnyoshee mkono wake wa uponyaji Josef Shamba.

Amen.
 
Siyo hayo ndugu zangu anakula kwa mpira mwenzetu anaonekana hana fahamu labda amepata Meningitis kwa sababu nilishaona mgonjwa kama huyo. Unajua tena siyo rahisi kuambiwa Ugonjwa wa mtu kama huna mahusiano naye ya karibu na tena kwa ridhaa yake. Ila kwa macho anatumia mipira puani na shingoni na hatambui mtu.

Ahaaa hayo ya MACHI MACHI NA MAANDE KINONDONI mbona wanaDUNDA TU mitaani wazima na wana vitambi na MASABURI yanatoka kama ya mchina? Mhurumieni mwenzenu. Hujafa Hujaumbika.
 
Itabidi tuanzishe move apelekwe India. Wale wanne walioko India kwa hivi sasa wameenda kwa kodi zetu na wanaendesha maisha yao ya kila siku kwa kodi zetu, na ni wakwepaji wakubwa wa kodi.

Huyu kijana alikuwa mlipaji mzuri sana wa kodi, hasa ile indirect taxi kupitia kilaji, anayo haki ya msingi ya kupelekwa India. Manji yuko wapi, aliwahi kuwapeleka hawa vijana UK wakale maisha sasa tunamuomba amjali kijana wakati huu wa shida.

POLE SANA BW MDOGO VENGU
 
1dzfcm.jpg
 
pole yake lakini akipona aache kuwafagilia ccm kwenye kipindi chake cha komedi tbc.ile ni tv ya taifa sio ya chama.
 
jaman wengine sie tuko mikoani huku hata idea anaumwa nin hatuna hata uwezo wa kuja na kumcheki huko muhi2 , mkienda mcheki huko mtuwakilishe na mtufikishie salamu zetu za pole pia. ila get well soon kwake na Mungu amsaidie apone haraka, ni majaribu tu hayo jaman

GET WELL SOON VENGU n GOD BE WITH YU ALL THE TIME
 
pole vengu, upone haraka mungu apende aridhie maombi yetu, AMEN
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom