Venezuela: Juan Guaido rejects talks proposal

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Mpinzani wa Maduro aliye jipa urais nchini Venezuela bwana Guaoido amekata ofa iliyotolewa na rais Maduro ya kukutana kwao na kuzungumzia hatma ya Venezuela.
Guaoido anadai yeye ni rais wa Venezuela huku Maduro nae akisema yeye ndio rais halali kwa mujibu wa katiba ya Venezuela.

Marekani na baadhi ya washirika wake wamemtambua mpinzani huyo kuwa ndiye rais wa Venezuela. Mpinzani huyo amevitaka vyombo vya dola kumtambua na kumpa ushirikiano.
Inaonekana Maduro anaelekea kukubali yaishe maana mpaka anaomba majadiliano si mchezo.
Kwa kibri cha Maduro na misimamo yake inaonekana kaishiwa nguvu za kuitawala Venezuela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka mwanzo maduro alishasema mambo ya Venezuela yatamalizwa na wavenezuela wenyewe maana ndiyo wanaoface difficulties.
 
Maduro asepe na madola yake tu, mbona sehemu za kuishi ni nyingi tu, na huyu Juan Guaoido ajipe muda tu, siku akienda vingine na hao wanaompa support yatamtokea puani kama Maduro..
 
Huyu anaefikiri ataweza kua rais kwakujitangaza ni rais mbele ya maandamano haramu..atasubiri sana
Kama anautaka huo urais aende huko marekani akatawale huko..

Mambo ya Venezuela yatamalizwa na wao wenyewe..sio na hawa wanafikii
 
Duh n Hatar sana
Screenshot_20190202-192014.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati Mbaya Afrika hapa hatuchambui pumba na mchele kila tunachokiona tunakimbia naccho
 
Back
Top Bottom