Vazi la Taifa: Nchi yetu imepata fursa nyingine ya matumizi mabaya ya rasilimali

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,744
Na Ndesumbuka Merinyo

Mbunifu wa Mavazi Afrika Sana

Kwa mara ingine hivi karibuni tumetangaziwa na Waziri mwenye dhamana na utamaduni wa taifa kwamba imeundwa kamati ya "kutafuta" vazi la taifa.

Hii ni mara ya tatu kwa serikali kufanya jambo hili. Mara ya kwanza ilikuwa miaka ya 2003-4 wakati ilipoandaa mashindano ya kupata vazi la taifa. Binafsi nilishiriki mashindano yale na nilikuwa mshindi wa jumla mkoani Kilimanjaro, na kitaifa moja ya mavazi niliyosanifu liliteuliwa kuwemo kama vazi la taifa upande wa wanaume.

Matokeo haya hayakutokea hivihivi, bali usanifu wangu uliegemea sana matokeo ya utafiti nilioshiriki wa mavazi ya asili ya makabila 9 maeneo kadhaa ya nchi yetu. Pale Dodoma kwenye mashindano kitaifa Vazi moja la kike lililobuniwa na maanii kutoka Kigoma lilishinda upande wa nguo za wanawake. Baada ya zoezi lile hapana chochote kilichofanywa na serikali kuhusu "matokeo" hayo.

Ukapita karibu muongo mmoja, na 2012 serikali ikatangaza "kutafuta" upya vazi la taifa. Ikaundwa kamati ya kitaifa, ambamo nilikuwa mjumbe. Safari ile kamati ikatembelea kanda sita nchi nzima na kupata maoni ya wananchi. Baada ya kukusanya maoni, kamati ikakaa na wataalam wa nguo - wasanifu vitambaa, watengeneza nguo viwandani na wasanii wachoraji.

Matokeo ya mchakato yakakusanywa katika kabrasha kubwa lenye maelezo ya kina na picha anuai. Ripoti rasmi ikakabidhiwa kwa Waziri mwenye dhamana. Kwa bahati nzuri niliikabidhi kwa mkono wangu kwa Waziri husika kwa niaba ya Mwenyekiti wa kamati aliyekuwa safarini. Kutoka hapo kikatokea kimya kizito cha muda mrefu kuhusu jambo la vazi la taifa.

Baadae, kwenye Awamu ya Tano ya uongozi wa nchi, Waziri mwenye dhamana na utamaduni, baada ya kubanwa kwa maswali kutoka kwa wadau na wabunge, akatamka kuwa serikali imefuta wazo hilo na kila Mtanzania atajishonea aonavyo inafaa kujiwakilisha kama Mtanzania.

Kabla maji yaliyomwagika hayajanyaushwa vema na joto la muda, tumeshtushwa tena kuona kwamba serikali ya Awamu ya Sita nayo imeamua kutengeneza fursa ingine ambayo bila kigugumizi naiita fursa ya kutumia vibaya rasimali za nchi.

Baada ya kushiriki mchakato wa mashindano ya kutafuta vazi ya mwaka 2003-4 na mchakato wa kamati wa 2012, niliona nina wajibu wa kushauri taifa letu kuhusu jambo hili. Niliandika makala iliyochapishwa kwenye magazeti ya Mwananchi na Nipashe ambayo kimsingi nilishauri kwamba mitindo iliyokuwa inatumiwa na serikali, ima kwa mashindano au kwa kamati, hayana tija na hayataleta matokeo yanayotarajiwa. Nilishauri kuwa serikali iangalie zaidi masuala ya sera zake zinazohusiana kwa namna moja au ingine na tasnia ya nguo nchini ili kutengeneza mazingira ambayo mavazi ya kitaifa yangeibuka bila matumizi ya kamati wala mashindano.

Mwaka jana nilirejea kufanya itafiti wa mavazi ya jadi ya jamii zetu za kikabila kwa undani zaidi nikiitumia mikoa mitatu ya Tanga, Arusha na Manyara. Utafiti wangu, pamoja na kuangazia uasili, malighafi, matumizi na maadili ya uvaaji, ulijaribu pia kuangalia manufaa na athari za utengenezaji wa mavazi ya jadi kwa tasnia ya usanifu mavazi kwa nyakati hizi nchini Tanzania. Niliwasilisha matokeo ya utafiti wangu serikalini kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) tarehe 7 Machi, 2022 pale ofisi za BASATA.

Tarehe 29 Julai, 2022 nitaendesha warsha jijini Arusha ambayo itakutanisha washiriki wa utafiti huo (wakiwemo maafisa utamaduni wa maemeo husika walioshiriki na BASATA wenyewe) kwa ajili ya kupata ithibati ya washiriki ili niweze kuhifadhi matokeo ya utafiti huu katika makavazi ya kidijitali kwa matumizi ya yeyote kwa vizazi vijavyo.

Baada ya maelezo haya, ni imani yangu kuwa viongoi wetu wanaopewa dhamana za ofisi mbalimbali ni watu weledi ambao wanaweza kuzingatia historian, uzoefu na tajiriba badala ya kufanya mambo kwa kufiata njia rahisi ambazo zimeshadhihirika kutoleta tija kwa taifa.

Ushauri wangu ni kwamba zoezi hili lisitishwe kabla hatujapoteza tena pesa za walipa kodi wa Tanzania kwa jambo ambalo lina muhali.

Screenshot_20220722-091642_Google.jpg
59499b079dbc2b007cfd5e146a2ebc9a.jpg
 
Na Ndesumbuka Merinyo

Mbunifu wa Mavazi Afrika Sana

Kwa mara ingine hivi karibuni tumetangaziwa na Waziri mwenye dhamana na utamaduni wa taifa kwamba imeundwa kamati ya "kutafuta" vazi la taifa...
Wote wana vitambi vya kula mabumunda na kunywa wanzuki, walikosa vi model au slim wakapiga hizo picha??? Nachukia minyama uzembe
 
Kuna mawaziri ambao hawana mafaili mezani kwao kabisa. Kuna mawaziri wiki inapita hajatia sahihi hata moja.
Waziri Kama huyo ambaye haangalii mafaili ya watangulizi wake hua anajiona yeye ndio muasisi wa wizara.
 
Kuna mawaziri ambao hawana mafaili mezani kwao kabisa. Kuna mawaziri wiki inapita hajatia sahihi hata moja.
Waziri Kama huyo ambaye haangalii mafaili ya watangulizi wake hua anajiona yeye ndio muasisi wa wizara.
Nahisi anadanganywa sana
 
Vazi la taifa?.

Yaani hata sielewi mpaka leo mnapambana kutaka muwe ma vazi la taifa, siku hazigandi kila kukicha kaunda suite imekuwa vazi la taifa yaani wanawake kwa wanaume, kwenye mikutano, sherehe, misiba, imekuwa kaunda kaunda mpaka watoto, walinzi nk.

Ukienda kwa vitenge hata wanaijeria nao wanavaa vitenge yaani mambo ni mpwitompwito.

Kinachotakiwa tengenezeni njia muandae kongamano mmuite wadau ili mle pesa na maposho tu basi.
 
Hata jana Mbunifu wa mavazi Mustaffa Hasanali alihijiwa na BBC alisema kitu hihiki kwamba vazi lilipatikana wakati wa Kikwete na walikabidhi kwa waziri ila baada ya hapo ikawa kimya
 
Kuna matapeli wengi ndani ya Sekta ya sanaa ambao hata Waziri hajaweza kuwastukia.

Watu wa Utawala Bora nao hawalijui hili kwa sababu wamezama kwenye kufuatilia wanasiasa tishio kwa maslahi ya chama
 
Back
Top Bottom