Vatikan Kuruhusu Mapadri Kuoa na Masista Kuolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vatikan Kuruhusu Mapadri Kuoa na Masista Kuolewa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Oct 26, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Siyo siri kuwa Kanisa la Kirumi la Kikatoliki linaanza kuuona mwanga na ukweli. Kama mizengwe na unyanyasaji na urushi havitarudiwa, kuna haja ya kulipa shime na heko kwa kuachana na unafiki na ukale visivyo na ulazima.

  Kanisa la Vatikan chini ya Rais wake, Papa Benedicto XVI linafanya mashauriano na baadhi ya wanamapinduzi ya kiroho juu ya sakramenti takatifu ya ndoa. Harakati hizi kwa upande mwingine zinaongozwa na Askofu mwenye mke, Emmanuel Milingo toka Zambia.

  Ulimwengu unakumbuka jinsi gwiji huyu wa theolojia na uponyaji alivyolitia kanisa msambweni pale alipoamua kuachana na ukapela na kumuoa Daktari Maria Sung (48), toka Korea ya Kusini. Ndoa hii iliyofana ilibarikiwa na Mchungaji Sung Myung Moon wa kanisa la Unification mwaka 2001.

  Kanisa kwa nguvu zake zote lilifanikiwa kumrubuni na kumrejesha Milingo kwenye kundi. Katika hatua hii mwezi Augusti 2001 alimkana mkewe na kurejea Vatikan alikofanya maombi na kufunga kabla ya kupelekwa uhamishoni nchini Argentina.

  Kwa mara ya kwanza wakati huo, kanisa na Bi Milingo waliingia mvutano usio wa kawaida hasa pale Mke wa Miliongo Daktari Maria Milingo alipodai kuwa kanisa lilikuwa limemteka mumewe.

  Kwa kitambo kidogo kanisa liliona kama limeshinda kumbe wapi. Maana baadaye Milingo alimrudia mkewe na kuendelea na kazi yake ya uponyaji na kuishi maisha ya ndoa.

  Mlingo mwanamapinduzi na mwanatheolojia asiyeshindwa na anayejua anachofanya, ameibuka upya jijini New-York akiwa na mkewe. Amekwenda maili moja mbele kwa kuanzisha jumuia inayoitwa "Married Priests Now".

  Kanisa limemtimua tena mwezi Oktoba baada ya kuwapa daraja la uaskofu mapadre wanne waliooa nchini Marekani.
  Anatarajia kuitangaza jumuia yake atakapokutana na mapadre wapatao 1,000.

  Jambo hili limelifanya kanisa la Roma kuanza harakati za kujadili suala zima la useja na ukasisi.

  Wale wanaopinga useja kwa makasisi wanadai kuwa hata Papa wa Kwanza kama kanisa linavyotuaminisha, Petro alikuwa ni mtu aliyeoa. Vile vile ukisoma Biblia hakuna sehemu hata moja Mungu anapozuia Mapadre kuoa wala Masista kutoolewa.

  Kitu kingine kinachofanya wanaopinga useja wa kulazimishwa kwenye kanisa la Roma ambao umekuwapo kwa takribani miaka 1,000, ni kuongezeka kwa kashfa za uzinzi na ulawiti miongoni mwa Mapadre na uzinzi kwa Masista.

  Soma 1 Timotheo 3:1-12 anasema ukiitaka kazi ya uaskofu umetaka kazi njema.

  Askofu awe mume wa mke mmoja,mtu wa makamo,asiwe mpenda mvinyo na pesa na mtu anayeweza kuitiisha familia yake. Je maaskofu wa Kikatoliki wanazo sifa hizo?

  1 Timotheo 4:1-4 roho asema wazi kuwa kutakuja wakati wengi wataanguka wakizitii roho chafu na itikadi za kishetani.
  Kwa kutumia unafiki wa waongo tena kwa ugumu wa chuma. Wanaozuia ndoa na kutetea kuacha kula baadhi ya vyakula....

  1 Timotheo 5: 9-11 kwa watawa au masista awe na umri si chini ya miaka 60 kwani chini ya hapo bado anahitaji kuolewa na kuzaa watoto.


  Historia.
  Papa Paulo V (1605-1621) Alipotaka madanguro yote ya Roma iliyokuwa na watu 100,000 na madanguro 6,000, waumini walikuja juu wakisema kuwa kufanya hivyo kutafanya mapadri wawatongoze wake zao.

  Papa Grigori XV (1621-1623) Alipoamru kisima karibu na nyumba ya watawa kikaushwe, alishtuka kukuta mafuvu ya vichanga zaidi ya 6,000.
  Kardinali Peter D'Ailly aliwahi kusema kuwa kuvaa joho la usista ni sawa na kutangaza kuwa u kahaba wa jamii.

  Albert The Magnificient wa Humburg Ujerumani, mnamo mwaka 1477 alipigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa wanawake wapatao 11,000 kwenye jimbo lake walikuwa wamewekwa kinyumba na watawa. Msemo kuwa Padre ni kuwa mume wa wanawake wote.

  Akiwaonya Mapadre wake Albert alisema "Si non caste,tamen caute" yaani kama huuwezi utaua basi uwe mwangalifu. Yaani ufanye mambo yako kwa usiri.

  Hivyo basi ni wakati muafaka wa kulirudisha kanisa kwenye ukweli kwa kuruhusu Mapadri waoe na Masista waolewe. Tena itakuwa rahisi maana wawili hawa wanajuana vilivyo ni suala la kutangaza kuachana na usiri na unafiki vinginevyo tendo lipo na halina ubishi.

  Kufanya hivyo kutarejesha hata imani ya waumini kwa watumishi wa Mungu ambao kusema ukweli kwa sasa ni hatari na uzembe kuwaamini hasa katika masuala ya ndoa.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Kuoa mke mmoja si dhambi. Hivyo kama wanataka kuamend sheria kwa manufaa ya dini yao, hakuna kosa hapo.

  Mapadri ni binadamu wa kawaida na hakuna dhambi yeyote wao kuoa kama sheria itabadirishwa katika dini yao, vivyo hivyo Masister wa Kiroma.

   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndg X-pathta kabla ya kukuuliza maswali mengine, samahani naomba nijue ilmu yako na profession yako, hii ni ktk kuepusha 'kumwonesha mtu asiyeona' wakti hana uwezo wa kuona.


  Nitashukuru kwa mwitikio.


  Asante.

  Nadhani umenielewa..
   
 4. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Tetesi, udaku ama habari ya uhakika? Nipatie chanzo cha hii habari tafadhali.
   
 5. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mpendwa X-Paster,
  Ungetupa chanzo cha hii habari kingetusaidia sana.
  Au kama chanzo ni 'wewe mwenyewe' ingependeza pia tujue.
  Asante.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wandugu,

  Sidhani kama anacho kithibitisho chochote, si unajua watu kujifanya walimu wakti wana ilmu ndogo kuliko 'wanafunzi' wao? Kumtajia References ni kumwonea.. Hebu angalia hata 'nature' ya posting yake ilivyokaakaa inatia mashaka kama ana idea ya mnachomuuliza!

  Na ndo maana nikamwomba animegee kidogo background yake ili tuangalie tuanze vipi kumsaidia.
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2008
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wana macho lakini hawataki kuona,wanamasikio lakini hawataki kusikia... Tumieni akili zenu Mtamwelewa hapahitaji torch hapo vinginevyo ni kujitia pambani tu,
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tutumie akili ktk nini haswa?
   
 9. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mhhhhhhhhhhhhhhhh???????
   
 10. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Akili kwa mujibu wa 'akili' yako ni nini?
   
 11. R

  Resie Member

  #11
  Nov 24, 2008
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari hii ina ukweli ndani yake! na hawa watumishi wa Mungu wa Kikatoliki huwa wanaenda kinyume na utauwa wao! swala la mapenzi haliwezi kuepukika, na ndio maana Mungu kamuumba mwanamke na mwanamume. Hivyo, sio vibaya wakiruhusiwa kuoa na kuolewa, watakuwa wamewapunguzia dhambi nyingi sana!
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Max, mapadre na maaskofu wote wanaongozwa na kitu kinachoitwa BIBLIA TAKATIFU. Wanaamend kitu gani kama hakuna mahali popote pale palipoandikwa wasioe! Kama kuna mahali pameandikwa basi waweke wazi hapa ni kitabu cha fulani. Nguzo ya Kanisa Petro alikuwa ndiye Baba Mtakatifu wa kwanza na alikuwa na mke. Tena kuna waliooa zaidi ya mke mmoja na bado walikuwa na cheo hicho. Paulo hakuwaambia Mapadre na watawa wasioe ila alimalizia kwa kusema " na kama mkishindwa basi mkae kama mimi" maana yeye Paulo hakuwa na mke, soma Wakorintho 7:1-7 endelea 8 kama una nafasi. Je tunaichukulia kauli ya Paulo kama Amri ya Mapadre kuto oa?
  Tukija kwenye uhasilia wa mambo, ni kuwa Mapadre wengi na Baadhi ya Masista kwa sasa ama wana vimada ama wake za watu ama wake wao kabisa. Ni ukweli usiopingika kuwa watu hawa wamekuwa msitari wa mbele kuipotosha jamii yetu kwa kigezo kuwa " Msifate niyafanyao bali nikwambiayo"
  Unaweza kusimama hadharani na kumwambia mtoto wangu usivute sigara ni mbaya wakati wewe una mche wa sigara unavuta kwa madaha kabisa? Baadhi ya mapadre ni wazinzi wakubwa tena kupita hata sisi ambao hatufungwi na dhana yao. Hawa tunakutana nao huku kwenye ma-guest na wake za watu, watoto wa shule nk, halafu kesho yake yuko madhabahuni anakwambia usizini? Kwa mtizamo wangu, mimi kama mimi nasema hapana hata kidogo. Siwezi kuongozewa ibada na mzinzi, na sitosali, nitakuwa nimepoteza muda wangu kwenda kanisani bure, ni bora nilale angalao. Waulize wale wasemao ukweli, watakwambia kuwa baadhi wanaacha wasichana wao vyumbani mwao wanaenda kwenye ibada ya asubuhi na akirudi wanaendelea? Mara ngapi wanawake wanamgombania Padre fulani? Kwa kuwa sio ndoa rasmi, basi wanaugulia maumivu tu! Wako wengi, tunawajua na jamii pia inawajua. Na huyu Mungu asiyefichwa kitu amewafunulia yale wayafanyayo (Kimaro), tena siyo kwa mwanamke! Kwa mtoto wa kiume! Aah! Inatishaje kumtumia mwanamke kinyume na maumbile halafu mtu kama huyu, kiongozi anayeheshimika na jamii anadiriki kumwambia mtoto wa kiume tufanye hivi! Jamani! Mapadre someni Wakorintho 6:15-20! Ni wangapi wana majeraha ya kujeruhiwa na HAWA watu. Ni wengi, ila kwa sababu ni tendo la aibu wasi wanuguza majeraha yao polepole na bado wanaugua mpaka leo.
  Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuripoti suala la uzinzi wa padre fulani hapa Tanzania, yaliyompata anayajua, kama siyo nyumba yake kuwa na mlango wa nyuma saa hizi angekuwa marehemu.
  Sio kwamba zamani Mapadre hawakufanya uzinzi, la hasha, walifanya sana lakini kwa siri kubwa sana. Masista walikuwa wakifanya hayo pia, na kwa sababu ndio wabebao mimba walihamishwa na kupelekwa mahali wasipofahamika, wanakaa, wanajifungua na baadae wanapelekwa kwenye parokia fulani kuendelea na kazi za utawa. Mtoto anapelekwa kulelewa kwenye vituo vya watoto yatima. Ndo maana hata saa nyingine masista wanakuwa na roho nzito sana kusaidia watoto maana nao wanajiuliza "watoto wao huko waliko wanalelewa vipi?"
  Mtu akijua uchungu wa mke/mume hawezi kufanya haya yafanywayo na hawa ndugu zetu. Unakuta kiongozi huyu anajua kuwa fulani saa hizi hayuko nyumbani lakini anaenda nyumbani kwake na kujidai anamtafuta mzee mwenye nyumba kumbe nia ni kutongoza mke ama mtoto wa nyumba hiyo.
  Waachiwe waoe, wawe na uchungu wa mke/mume na watoto. Hapo ndopo nao wataona ni jinsi gani inavyouma kutendewa.
  Mimi nafikiri Kanisa Katoliki wamechelea kukubali Mapadre na masista kuoa/kuolewa. Ni wakati sasa umefika wa kubadili mtizamo huu.
  Naona naanza kuhubiri, tuyaachie hapo,,,,,
  Mungu awabariki sana
   
 13. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  X-Paster
  Kama unataka kujenga harakati ni lazima uwe kati ya kondoo...usikimbie ukasema ukiwa nje mkuu..Kwani useja si mtu anajipangia? Kama padri/sista anataka kuoana ruksa na anakuwa X-Paster X-Priest X-Baba Paroko X-Mama Mkuu X-Sista MariaGoreta.... X-Sista Consolata!
  Ila baada ya hapo mgawanyo wa sadaka na zaka lazima ujulikane!
   
 14. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Acha uongo wako! Ni kweli "hawa watumishi wakikatoliki huwa wanaenda kinyume na utawa wao?" Nionyeshe wasioenda na kinyume na wito wao katika dini yoyote (hasa ya kwako).

  Ni heri useme baadhi kwa vile hata hao unaowasema sidhani kama unawafahamu kama siyo namba ya kichwani tu. Kwani ukioa huwezi kwenda kinyume na wito wako?

  Mara ngapi tunasikia skendo za watu waliooa pia: wanalawiti watoto wao wa kuzaa na kubaka. Au hawa wote huwa ni watawa unaowasema?

  Kuwa na uelewa mzuri na kitu unachokisema.
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Eka Mangi umesema ukweli na hakuna wa kubisha hapa. Tamati ni kwa mapadre na masista kuwa na wenzi wa maisha. Hakuna popote katika bibilia imekataza. Nafikiri hapa Vatican ilikuwa inataka kukwepa mzigo wa kutunza familia za mapadre!!! Kumbe basi kutokuwa na familia rasmi za mapadre kumesababisha kuwe na several of them na ambazo zinagharimiwa na makanisa indirectly. Mapadre wengine kwa sasa wamemeamua kujiingiza katika biashara, kujenga guest houses, hotels, maduka , n.k na hii ni kupata fedha kwa ajili ya kugharimia watoto au tuseme familia zao zisizotambulika na kanisa. Kwa wale waliosoma au ni waalimu wa Kibosho Girls, Kiraeni Secondary, Mazinde Juu, Kifungilo, you name a few watakubaliana nami kuwa watoto wa mapadre wanasoma shule hizo (wa kike). Wale wa kiume wanasoma hasa Kilimanjaro boys!!!!

  Hili fumbo la mapadre kutoa limeleta mtafaruku mkubwa sana hata katika nyumba za familia watokazo mapadre hawa. Kwa kawaida (generally) familia zinazotoa mapadre huwa ni nyenyekevu sana na washika dini (Katoliki) na huwa huonekana za heshima mbele ya jamii inayowazunguka. Hivyo wazazi au familia hizi wanaposikia mtoto wao padre amejiingiza katika tabia ya uasherati au uzinzi inawaumiza sana. Kuna mfano mmoja padre alizaa watoto wanne (wanaojulikana ni zaidi ya hapo) na akawa anaendekeza uzinifu ndani ya kanisa kiasi kwamba jimbo lake lilimpa adhabu ya kutoa huduma parokiani alikozaliwa ili pengine angejirekebisha lakini haikusaidia. Kilichofuata ni wale watoto kukusanywa na kuletwa kuishi nyumbani kwa babu yao. Kitendo hiki kilimuumiza sana yule mzee wa (baba mzazi wa padre huyo) na alipata shinikizo la damu kabisa. Sasa basi ili yote hayo yasitokee naona mapadre waruhusiwe kuoa, vinginevyo kanisa la Katoliki linazidi kuporomoka.

  Yaani gilrfriends ndo usiseme, kila kona. Huwezi kuniambia eti mwanaume anakula vizuri tena highly in protein halafu unamwambia eti ishi towashi, ni kitu ambacho hakiwezekani, ni sawa na ndoto za abunuasi na alinacha.
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Na siku za hivi karibuni walianzisha michango inayoitwa VIPAJI! Kwa mgongo huu wakawa manapelekewa sukari, majani, sabuni, kuku, mayai, karanga, na vyote ambavyo waumini waliona vinamfaa paroko wao. Akaangiwe na sista pale parokiani ama amteue mke wa jirani, mzurimzuri hivi ampikie, halafu amwache? Na virutubisho vyote hivi? Lol. Nachoka kweli kweli!
   
 17. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Eeka Mangi hapa nakunyooshea mikono...nilikuwa sijapambanua vipaji thing na ngoma za kuvipeleka madhabauni kama Selemani vile
   
 18. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kifupi; Kutooa kwa mapadre /maaskofu wa kikatoliki si agano la Kibiblia....Huu ni utaratibu ambao kanisa katoliki lilijiwekea kupitia Mtaguso wa nane(not sure with 8)...na kwa taarifa yenu....hata baada ya Petro, mapadre waliofuata walikuwa wanaoa (ni huo mtaguso ulikuja kubadili hili) angalia Orthodox (katoliki wa mashariki) wanaendelea kuoa hadi leo!

  Hivyo kuoa kwa mapadre wa kikatoliki si dhambi ila ni kukiuka taratibu za kanisa tu!. Na taratibi hizi zaweza kabadilishwa wakati wowote kama itakubalika na kanisa (World catholics) vinginevyo wakienda pupa wanaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa sana katika kanisa la kikatoliki!

  For more mtafuteni Askofu M. Kilaini....mtaalam wa Historia ya Kanisa Katoliki na atawapa in detail maisha ya USEJA KWA MAPADRE WA KIKATOLIKI
   
 19. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bwana mmoja wakati najadili hapa amenidokeza kuwa kuna jamaa alipata taarifa kuwa mkewe ana mahusiano na padre wao, jamaa akaamua kumpa kichapo mkewe, mke akaenda kushitaki kwa padre yuleyule anayetuhumiwa, padre akamwita mume wa yule mwanamke,,,, akamuuliza:-
  Padre: Ni kweli umempiga mkeo
  Mume: Si kweli padre
  Padre: Unasema kweli
  Mume: Ndio padre
  Padre: Nikuapize na huu msalaba
  Mumu: uumh,,, aaaaah, lakini padre nakubali uniapize lakini kabla mimi sijaapa na mimi ushike msalaba uape kama hujafanya ngono na mke wangu!
  Padre akawaacha sakriste mtu na mkewe akaondoka zake.
  Kaaaaazi kweli kweli!
   
 20. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Well nakubaliana na wewe ila ni kitu gani kinachowafanya Kanisa Katoliki kuwa ni shingo ngumu ni kitu gani? Hata Yesu alisema hakuja kuibadilisha tourati bali kuiendeleza. Mtaguso wa nane una nini usiuhishwe ili uende na wakati tuliokuwa nao? Askofu Kilaini ama anapitaga mitaa hii ama vijana wake, watoe hoja huku, je uzinifu wanasingiziwa? Kwa nini wasibadilike? Hawawaoni baadhi ya mapadre na ndoa zao ambazo sio rasmi? Hawajui ni kwa nini wanakuwa na watoto wanaoitwa wa mapadre? Sisi tunachjiuliza mtaguso ni tourati?
  ni wakati sasa wa kubadilika maana hata sasa kuna Biblia ya kiswahili cha kisasa! Tuhuishe mtaguso huo
   
Loading...