VAT katika mbuga zetu na hadithi na mizengwe ya Prof Maghembe

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
19,931
34,408
Heshima sana wanajamvi,

Wakati Waziri wa Fedha akiwasilisha bajeti ya wizara ya fedha aliainisha pamoja na mambo mengine juu ya kodi mbali mbali ambazo Tanzania iliwajibika kutoza kwakuwa tayari kulikuwa na maridhiano na mawaziri wenzake wa fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kati ya kodi hizo tozo ya VAT kwa wageni watakaotembela hifadhi zetu za taifa zilitangazwa katika bunge hili la bajeti.

Baadhi ya taasisi zinazojihusisha na utalii Tanzania hasa TATO zilitoa taadhali juu ya kodi kwamba majirani zetu Kenya ambao ni washindani wetu wakubwa hawajaweka tozo ya VAT katika utalii na hili pekee yake yaweza kuiweka Tanzania katika nafasi ngumu ya kushindana na majirani zetu.Katika hali ya kukatisha tamaa angalizo hili halikuzingatiwa na pengine bajeti ya mwaka huu sehemu kubwa haikujadiliwa kwa kina kwakuwa mazingira hayakuwa rafiki sana.

Majuzi tumemsikia Prof Maghembe akitetea jambo kwa nguvu (si kwa hoja nzito) eti Tanzania si koloni la Kenya na haifanyi mambo yake kwa kuitegemea au kuitazama Kenya ?.Kasahahu Waziri wa fedha wakati wa bajeti alisema wazi kodi hiyo ni maridhiano na mawaziri wenzake wa Afrka Mashariki Kenya ikiwemo.Imekuwa ni kawaida watawala wetu wa ngazi mbali kutoa majibu ya hovyo kwakuwa wanafikiri waTanzania si watu wa kufuatilia mambo yao kwa karibu.Ifike wakati mawaziri na viongozi wengine waelewe kauli zao zitakuja kuwaumbua muda si mrefu.Ni vyema wakawa na akiba ya maneno badala ya kupayuka payuka pasipo kushirikisha akili.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom