Vasectomy imeniponza: Mke wangu ana mimba ya wajanja, nifanyeje!

Fidel80 nakuunga mkono, kuondoa hii kadhia mwambie salama yake muende akatoe hii mimba, ni adhabu tosha kwake. Halafu na yeye atoe kizazi. Sema uwe makini anaweza sasa kuuza mechi balaa maana nyavu hazitingishwi utajuaje?

Akitoa kizazi jamaa watakuwa wanapewa kila kukicha.......ndio mambo ya kwenye ndoa jamani
 
Kwa mtizamo wa haraka:
  1. Huo mfululizo wa watoto wengine si wako,
  2. Ulipokuwa umeshamtia mimba wewe akizaa
  3. Mwanaume mwingine naye anatia baada ya muda kidogo kwa hiyo
  4. Unakuta mlikuwa wanaume wawili ndiyo maana ukajikuta mkeo anazaa ovyo ovyo, ushauri
  5. Pima hao watoto DNA ufahamu, then uchukue maamuzi kwani usipofanya hivyo,
  6. Hapo baadaye akina mama huwa hawana siri kwa watoto wao watakuja
  7. Waeleza haswa unapokuwa umekosana na hao watoto, ndiyo mama atakaposema
  8. Mwanangu huyu siyo baba yako, kwa hiyo badala ya kusubiri aibu
  9. Iepuke sasa kwa kujiweka sawa!
 
Mpe muda ajifungue huyo mtoto kisha babaye amlee kisha akurejee. Mbona mwanaume anaoa wake zaidi ya mmoja basi pia wewe kubali kuwa mkeo anawanaume zaidi ya mmoja life goes on!!!!
 
ndo maana sasa naona hata kupima DNA inaweza ikaja kuwa yaleyale ya kujimaliza kabla ya wakati..............sijui itakuwaje ntapojua kuwa hata hawa wengine kati yao sio wangu. presha inaweza kuniondoa duniani

Polle sana mkuu......ushauri wangu kama huna kifua achana na mambo ya DNA, endelea kulea hao malaika wasio na makosa. Cha msingi kabla hujaanza kumuhukumu mkeo hakikisha umeenda hospital sio chini ya tatu kupata uhakika kuwa your sperm count is zero!! Kinachonichosha ni kuwa umefanya hiyo surgery 10months ago(weird)......najitahidi kutoamini kuwa unasaidiwa mpaka mimba!!! Kama kweli kazi unayo,poleee maana na gonjwa hili mmmhhh!!!!
 
Miezi 10 iliyopita niliamua kufanyiwa uzazi wa mpango kwa kutumia ile njia ijulikanayo kwa jina la VASECTOMY. Hii ni baada ya kuona mwenzangu 'hesabu' zimemshinda kabisa. Nikaona ili kuepuka uwezekanao wa kuwa na familia yenye idadi ya timu ya mpira-maana watoto 8 ktk ndoa ya miaka10 sio mchezo-nikaona acha jukumu la uzazi wa mpango nilichukue mwenyewe. Nikaamua kufanyiwa vasectomy.

Miezi miwili imepita sasa, nimegundua mke wangu ni mjamzito, tena wa miezi 3. Hii ni baada ya kuona dalili zile zinazoambatana na mimba changa. Nilipohisi nikaamua kumpeleka hosp lakini bila yeye kujua, nikaongea na daktari ampime mimba na anipe majibu privately. Mungu si Athumani, vipimo vikaonyesha mke wangu ana mimba ya miezi miwili. Sikuonyesha kushangaa mbele ya dr kwani sikutaka ajue mshangao wangu ktk hilo. Hata hivyo wife ameshaanza kuhisi kuwa amenasa, na amekosa amani ghafla.

Awali nilidhani huenda hiyo operesheni haikufanywa vizuri, lakini nilipoenda kuangaliwa upya mtaalamu iko sawa na nisingeweza kumtia ujauzito my wife. Hivyo ni wazi mimba hii ni ya mwanaume mwingine.

Wajemeni naomba mnishauri nifanyeje. Na kama ni adhabu, nimpatie adhabu gani..........nimchinje, nimpe talaka, au niendelee kulea 'kiumbe cha mwanaume mwingine?

pole sana mkuu, hapo inabidi utumie busara ku-handle hili suala ikiwa ni pamoja na kujua ukweli kwa DNA japo namuonea huruma next born anaweza akakosa kabisa father love.

Samahani mkuu nauliza, hivi ukifanyiwa hiyo procedure bado gun inaendelea ku-fire ila risasi zinakuwa zile za mpira (haziui) au hata risasi zinakuwa hakuna kunakuwa labda na mlio tu??? Maana wanasema pia ile kani ya risasi inavyomrusha adui ina changia morali ya vita..
 
Hapa chukua watoto wote pima DNA unaweza kukuta kwamba hata
kwenye aho waliobaki wapo ambao sio wa kwako kisha timua na mama
yao acha uzandiki

hata simba wa porini hatunzi watoto wa mume mwenzie kama ni wadogo
sana huua ili aweze kupata uzao wake
............kwa heri

Kweli. Lakini kwa ukweli zaidi ni kwamba, simba jike anapokua ananyonyesha hawezi kuingia katika "heat"; hivyo simba dume (dume ambalo halimzalisha huyo jike) likitaka kumfanya huyo jike aingie kwenye "heat", litavila/litaviua hivyo vi lion cubs ili mama aingie kwenye heat tayari kabisa kufanya shughuli nzima ya kupass genes.
 
Miezi 10 iliyopita niliamua kufanyiwa uzazi wa mpango kwa kutumia ile njia ijulikanayo kwa jina la VASECTOMY. Hii ni baada ya kuona mwenzangu 'hesabu' zimemshinda kabisa. Nikaona ili kuepuka uwezekanao wa kuwa na familia yenye idadi ya timu ya mpira-maana watoto 8 ktk ndoa ya miaka10 sio mchezo-nikaona acha jukumu la uzazi wa mpango nilichukue mwenyewe. Nikaamua kufanyiwa vasectomy.

Miezi miwili imepita sasa, nimegundua mke wangu ni mjamzito, tena wa miezi 3. Hii ni baada ya kuona dalili zile zinazoambatana na mimba changa. Nilipohisi nikaamua kumpeleka hosp lakini bila yeye kujua, nikaongea na daktari ampime mimba na anipe majibu privately. Mungu si Athumani, vipimo vikaonyesha mke wangu ana mimba ya miezi miwili. Sikuonyesha kushangaa mbele ya dr kwani sikutaka ajue mshangao wangu ktk hilo. Hata hivyo wife ameshaanza kuhisi kuwa amenasa, na amekosa amani ghafla.

Awali nilidhani huenda hiyo operesheni haikufanywa vizuri, lakini nilipoenda kuangaliwa upya mtaalamu iko sawa na nisingeweza kumtia ujauzito my wife. Hivyo ni wazi mimba hii ni ya mwanaume mwingine.

Wajemeni naomba mnishauri nifanyeje. Na kama ni adhabu, nimpatie adhabu gani..........nimchinje, nimpe talaka, au niendelee kulea 'kiumbe cha mwanaume mwingine?

Kinachoniuma ni kwamba nilipochukua uamuzi wa kufanya vasectomy, alifurahi sana na kuwaeleza watu jinsi alivyoona kuwa mimi ni responsible husband. manesi pia walinisifia sana. sasa ghafla wife ana mimba, ntauweka wapi mimi uso wangu jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiii! si afadhali angetumia kinga, walau angenisitiri utu wangu?

Duh! Kama ni kweli haya yote basi hakika ulioa bovu. Yaani pamoja na mkeo kujua kwamba umefunga kizazi chako bado hakathubutu, kujaribu na kusonga mbele katika uzinzi na hatimae kunasa!!!!?!?!
 
Mpe muda ajifungue huyo mtoto kisha babaye amlee kisha akurejee. Mbona mwanaume anaoa wake zaidi ya mmoja basi pia wewe kubali kuwa mkeo anawanaume zaidi ya mmoja life goes on!!!!

hiyo nayo ni busara pia!
 
Acha kujitia pressure wewe lea mtoto..anaweza kukufaa kupita wengine wote..

Kulea mtot moja nini bana wakati unao nane??
 
Couple Sues After Failed Vasectomy

Posted by Hannah Tennant-Moore

What would your first assumption be if your wife got pregnant after you’d had a vasectomy? Would you suspect her of being unfaithful—or your sperm of outsmarting your sterilization surgery?

Well, unless your marriage is on the rocks or you’re swingers (and, hey, I don’t judge!), the latter is the more likely. At least 1 percent of vasectomies fail to prevent pregnancy—just as condoms break and women on the pill get pregnant.

Mindy and Brady Hill of Arkansas found out what it was like to be that one percent (as, presumably, have thousands of other couples), and they didn’t like it one bit. They claim that doctors suggested that Mindy had been unfaithful, which put stress on their marriage. After Mindy miscarried, a paternity test showed that there was a 99.999 percent chance that the baby was Brady’s. No doubt this whole ordeal was highly stressful and unpleasant.

Still, one would hope that Brady trusted Mindy enough that a paternity test wasn’t necessary to make him believe that the baby was his. But, of course, a paternity test will come in handy in court.

Mindy and Brady are suing for negligence and defamation. Should they win?
Yes, Without any doubt.

sheria gani unayozungumzia inamlinda mke aliepata mimba nje ya ndoa? kuna sheria inalinda adultery? ground za mahakama kukubali kutoa talaka mojawapo ni adultery ukiwa na ushahidi kwa huyu bwana anao
labda useme sheria ya ndoa ya 1971 imefanyiwa mabadiliko kuruhusu adultery.
kwa ushauri wangu tayari una watoto 8 ukimtimua mama watoto watateseka
bora umkamate akueleze ukweli yawezekana hao wengine pia sio wako lkn kwa vile wanakuita baba na ushawatunza endelea kuvumilia 'kweli ndoa kaka ni ngumu
msamehe tu alijisahau kama ulifanyiwa hiyo kitu si unajua mpenda asali huchonga mzinga kabisa.yahitaji moyo

Pole mkuu.

Ila sheria ya Ndoa ya Tanzania inamlinda mkeo. Hata kama ukichukua vipimo vya DNA na kugundua kuwa mimba si yako kabisa, KITANDA HAKIZAI HARAMU (kwa sheria ya Tanzania). Unaweza kuuchuna na kumwonya, for the best interest of your other children.

Jikaze mzee.
 
Miezi 10 iliyopita niliamua kufanyiwa uzazi wa mpango kwa kutumia ile njia ijulikanayo kwa jina la VASECTOMY. Hii ni baada ya kuona mwenzangu 'hesabu' zimemshinda kabisa. Nikaona ili kuepuka uwezekanao wa kuwa na familia yenye idadi ya timu ya mpira-maana watoto 8 ktk ndoa ya miaka10 sio mchezo-nikaona acha jukumu la uzazi wa mpango nilichukue mwenyewe. Nikaamua kufanyiwa vasectomy.

Miezi miwili imepita sasa, nimegundua mke wangu ni mjamzito, tena wa miezi 3. Hii ni baada ya kuona dalili zile zinazoambatana na mimba changa. Nilipohisi nikaamua kumpeleka hosp lakini bila yeye kujua, nikaongea na daktari ampime mimba na anipe majibu privately. Mungu si Athumani, vipimo vikaonyesha mke wangu ana mimba ya miezi miwili. Sikuonyesha kushangaa mbele ya dr kwani sikutaka ajue mshangao wangu ktk hilo. Hata hivyo wife ameshaanza kuhisi kuwa amenasa, na amekosa amani ghafla.

Awali nilidhani huenda hiyo operesheni haikufanywa vizuri, lakini nilipoenda kuangaliwa upya mtaalamu iko sawa na nisingeweza kumtia ujauzito my wife. Hivyo ni wazi mimba hii ni ya mwanaume mwingine.

Wajemeni naomba mnishauri nifanyeje. Na kama ni adhabu, nimpatie adhabu gani..........nimchinje, nimpe talaka, au niendelee kulea 'kiumbe cha mwanaume mwingine?

Kasome vasectomy kwenye internet halafu tafuta kipengele kinachogusia uwezekano wa kumpa mtu mimba after vasectomy....kama nakumbuka shule yangu vizuri it takes about 6 months for the sperms to clear....hiyo mimba inaweza ikawa yako
 
Swali la kizushi , Kabla ya ndoa ulikaa naye muda gani kumjua tabia zake ? inawezekana hakuwa mwaminifu toka mko wachumba tabia huwa ngumu kubadilika baadae huyo anonekana alizoea kucheat !
 
hii ni mbaya sana mkuu( only if didn't ever/ don't cheat on her) and it's not too late kuchukua maamuzi magumu.Why they said za mwizi 40? kimsingi binadamu anaweza kujizuia kwa muda flani lakini hana uwezo wa kuzuia nature baada ya muda flani,siri zinafichuka baada ya wahusika kuwa less careful kuhusiana na matukio baada ya time kupita & nature ku-take its place which means there's high possibility kua alianza michongo hiyo kitambo,inawezekana pia katika hao 8 wa kwako ni 2 au 1 au whatever,shtuka mkuu.
 
kwa hiyo unanishauri na shule nimpeleke na gharama nyingine nitoe as if ni mwanangu huku nikijua sio wangu? Hata kama limbwata hii sasa itakuwa imezidi, loooooooh!

Makosa yashafanyika!!!!, Tahadhari kabla hujafanya utakayo jutia baadae, vumilia ndugu. Huyo mtoto wala usimchukulie kwa ubaya hana makosa hata kwa mungu....Amini, Usiamini...kati ya hao watoto 8, anaweza kuja kukufaa ni huyoooo!!!, tushayaona haya.
 
Dah pole mkuu..maneno makali sana umeyatumia hapa na yanaleta hali fulani ya huzuni.
Kikubwa hapa jaribu kuongea nae taratibu usikie nae anajitetea vipi. huenda anapata mimba kwa miugiza...Je nyendo/tabia zake wewe huwa zinakutia mashaka? kabla ya kuchukua maamuvi yeyote magumu pata ukweli ili umjue kabisa nani mharibifu wa hii ndoa yako.
Kinachoniuma ni kwamba nilipochukua uamuzi wa kufanya vasectomy, alifurahi sana na kuwaeleza watu jinsi alivyoona kuwa mimi ni responsible husaband. manesi pia walinisifia sana. sasa ghafla wife ana mimba, ntauweka wapi mimi uso wangu jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiii! si afadhali angetumia kinga, walau angenisitiri utu wangu?
 
Back
Top Bottom