Vanessa Mdee akamatwa na Polisi Dar kwa tuhuma za Madawa ya Kulevya

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
Msanii wa kizazi kipya, Vanessa mdee amekamatwa na polisi leo mchana, hata hivyo sababu ya kukamatwa kwake bado haijajulikana.

=====

MSANII VANESSA MDEE AKAMATWA NA POLISI JIJINI DAR
IMG-20170308-WA0000.jpg

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita.

Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa chini ya Lebo B'hitts.
 
Mkuu sababu haijulikani kweli? Au ile kuwa kwenye majina ya makonda?
 
Na alivyojichokea si wangempa methadone tu, kule wataenda kukaua tu jamani
Warumi kwani unaona ni sawa kuwakamata hawa watumiaji na kuwaweka ndani, badala ya kuwatumia kama link ya information kwa wale mapapa wakubwa wanaowauzia. . ?
 
Warumi kwani unaona ni sawa kuwakamata hawa watumiaji na kuwaweka ndani, badala ya kuwatumia kama link ya information kwa wale mapapa wakubwa wanaowauzia. . ?
Hiyo link wataitaja wakiwekwa ndani, ndio maana wamawekwa ndani coz wanahoji then wanawaachia kama hawana hatia
 
Msanii wa kizazi kipya, Vanessa mdee amekamatwa na polisi leo mchana, hata hivyo sababu ya kukamatwa kwake bado haijajulikana
Vanessa should immediately be subjected to methadone for withdrawal effect on heroin she has been.
 
Back
Top Bottom