Van Dame(Sinza), Yesu (Mbeya) kati ya Wababe waliowahi tikisa Tanzania

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,321
11,410
Nilikuwa na jamaa yangu ananipa visa na mikasa mbali mbali ya Jiji la Mbeya miaka ya 1980s mpaka 1990s. Alianza kuniambia jinsi ambavyo miaka hiyo vijana wengi jijini mbeya ilikuwa lazima waende GYM, wajifunze Karate/Kung fu au Tae kwon do na michezo mingine mbalimbali ya mapigano.

Mwenyeji wangu ananitajia mmoja ya watu anaowakumbuka miaka ile alikuwepo Daud. Huyu kwa watu wengi wa Mbeya miaka ile wanamkumbuka jamaa likuwa amejenga mwili na kujichora tattoo kadhaa mwilini mara nyingi akitembea amevaa singlet kuonesha tattoo zake na misuli yake iliyokuwa imejaa vyema kabisa.

Huyu alikuwa mbabe, ngumi jiwe miaka hiyo akipiga ngumi uliyepigwa unaona kama umepigwa na jiwe zito sana kutokana na kuwa na nakozi kwenye mikono. Wengi walikuwa wakizimia kutokana na ngumi alizokuwa akipiga watu. Akaendelea kunipa historia ya wababe wengine waliowahi kutokea jijini humo miaka ya kale.

Anasema miaka hiyo alitokea jamaa mmoja alikuwa anaitwa Shetani. Jamaa alikuwa ana uwezo mzuri sana wa kutembeza kipigo kwa raia na askari kiasi kwamba askari wenyewe walikuwa wakimgwaya sana. Alikuwa kwa Mbeya mjini yeye ndiye mtemi anayefahamika na kama hukukubaliana naye ilikuwa ni jambo rahisi tu mnakubaliana siku ya weekend mnaenda kukutana eneo flani kwa ajili ya kutembezeana mkono mpaka apatikane mshindi.

Utawala wa huyu bwana ulikuja kukomeshwa na jamaa mmoja ambaye alikuja kupewa jina la yesu. Huyu aliitwa Yesu baada ya yeye kuja kumtembezea kipigo kikubwa sana huyo shetani. Huyu Yesu inasemwa kuwa yeye alitokea Zambia. Kufika Mbeya mjini akawa amesikia habari hizo za uwepo wa shetani kuwa ndiye mbabe ile kinyama na ikatokea siku moja wakakutana katika mizunguko ya maisha katika kutunishiana misuli ikaamuliwa zichapwe.

Msimualiaji anasema miaka hiyo walipata nafasi ya kushuhudia ngumi kama za kwenye movie live kabisa bila chenga, zilipigwa ile kinyama. Mapigo na ufundi mbalimbali mpaka dakika za mwisho shetani alikuwa hoi vibaya sana na kuamua ku surrender. Ndipo yule mbabe mpya alipopewa jina la Yesu. Tofauti na shetani wanasema huyu Yesu alikuwa ni mstaarabu hakuwa akionea watu au kufanya mambo kibabe.

Hayo ni mambo ya Jiji la Mbeya miaka hiyo. pamoja na kuwepo pia wababe wengi maeneo mbalimbali jijini humo hasa akisema maeneo kama Machinjion, Sisimba, Sinde, Meta, Soko Matola, Mwanjelwa n.k

Nikakumbuka miaka ya 200s Dar es Salaam alikuwepo jamaa mmoja naye shababy sana al maarufu kwa jina la Van Dame wa Sinza. Huyu jamaa nilishasikia sana habari zake miaka hiyo na kwa bahati mbaya mimi umri wangu ulikuwa umeshasogea sogea sikuwa naendelea tena na mchezo nliokuwa nikiupenda wa MMA. Maana nlijifunza kung fu, nilikuwa mzuri kwenye Katare na kiasi judo. Hii ilinipelekea pia nicheze michezo mingi kama Kick Boxing n.k miaka hiyo ya nyuma.

Van Dame alikuwa anasifika sana kwa uwezo mzuri aliokuwa nao wa kurusha mateke na wepesi katika kuruka na kukimbia inapohitajika. Polisi wengi walikuwa wakimgwaya na hata hawakuwa wakitamani kwenda mkamata maana alikuwa na uwezo wa kuwatembezea kipigo kikubwa sana hata wakarudi kituoni wakiwa hoi na wenye hali mbaya kimwili.

Tatizo kubwa la Van Dame lilikuwa nasikia ni usela choo mwingi sana. Alikuwa akikaba watu au kupora vitu vya thamani na alikuwa akikufanyi hivyo huna cha kumfanya. Maana ukimpeleka polisi wataishia tu kuandika maelezo na kuanzia hapo wao ndo wanaanza kumkwepa ili wasije wakajikuta wapo katika mazingira ambayo walipaswa kumshika halafu ikawa ngumu.

Hivyo polisi wenyewe ikawa ukiwaambia Van Dame nimemwona Mwenge au Kijitonyama basi siku hiyo polisi hawakanyagi kabisa maeneo ya huko. Hali ilikuwa ikizidi sana wanaenda kumwomba aende kituoni naye atawaambia basi haina shida ntakuja baadaye au kesho.

Van Dame wanasema alikuwa mbabe kinyama, sifahamu mwishowe aliishia wapi lakini ni mmoja ya watu ambao walikuwa na sifa lukuki katika sanaa za mapigano.

JE MKOANI MWAKO ALIKUWEPO NANI MBABE NA SASA YUPO WAPI? TUENDELEE KUJULISHANA HAYA MAMBO YA KIBABE... KWA SASA UTU UZIMA NA KAZI ZETU HIZI ZINATUZUIA SISI WENGIE TUSIISHI MAISHA HAYA. LAKINI KIUKWELI NI MAISHA AMBAYO MIMI HUWA NAYAMISS SANA. NA ILIKUWA NGUMU KUSIKIA WANAKUWEPO AKINA JUMA LOKOLE... sababu wanaume ilikuwa ni kugangamaa toka ukiwa mdogo. unakua kiume hasa. siku hizi watoto wanavaa mlegezo?

zamani ungevaa mlegezo kuna mbabe mmoja angekuita na kukwambia asikuone tena unakanyaga mtaani KWAKE ukiwa umevaa hivyo sababu next time atakugonga makwenzi kinyama mpaka akili yako ikae sawa. au akuone unatembea kishoga shoga... angekucharaza viboko na kukwambia asikuone tena mtaani unachafua hali ya hewa.


GuDume Bujibuji Mshana Jr Chizi Maarifa @ na wadau wengi wenyeji wa dar na mikoa mingine. Hasa Arusha Macharliee mtupe habari za wababe waliowah kuwepo na walipo mpaka sasa.
 
Naona amekusimulia sehemu nyingine anekuchanganya Daud Masonke wa Mafiati alijichora tatuu moja kwenye bega D...na pia alivuliwa ukuu kwa kupigwa na jamaa mmoja wa Isanga akiitwa Brigadier Mwakayugu huyu jamaa alikua hana mwili ila alikomaa mbaya na akipigwa havimbi siku wapo Mount Living stone disco kila mtu akawa anatangaza yeye mbabe walitoka Nje walipigana mpaka maeneo ya Rift Valley hotel baadae wakaanza kitupiana Mawe ikawa vita kati ya wababe wa Isanga na Mafiati huko maguruweni ilifikia mpaka vijana wa Mafiati hawaruhusiwi kukatiza Isanga kwenda kuzika makaburi ya huko wazee wa pande zote mbili waliingilia kati huku kuna kijana mdogo Marehemu Atu Mwaijande ilikua ni hatari...kuhusu Shetani na Yesu walikua washkaji sikumbuki kama walishawahi kupigana nachokumbuka walizima disco lililofanyika Iyunga sec na Chuo cha MTC wao wakitaka kuondoka walikua wanataka disco liishe hao ndio wababe wa Zamani Mbeya miaka hiyo Mbeya usipokua Nunda unaonewa sana...Disco tunaenda kwa mguu popote pale na kurudi usiku muda mwingine hata peke yako....
 
unaweza tu kuongezea nyama maana mimi nimesimuliwa na fasihi simulizi inakuwa na mambo yake kadhaa wa kadhaa hivyo kama kuna sehemu unaweza ongeza nyama ongeza tu lengo hawa wabbe tuweze kuwa enzi angalau hata mara moja kwa mwaka.

Naona amekusimulia sehemu nyingine anekuchanganya Daud Masonke wa Mafiati alijichora tatuu moja kwenye bega D...na pia alivuliwa ukuu kwa kupigwa na jamaa mmoja wa Isanga akiitwa Brigadier Mwakayugu huyu jamaa alikua hana mwili ila alikomaa mbaya na akipigwa havimbi siku wapo Mount Living stone disco kila mtu akawa anatangaza yeye mbabe walitoka Nje walipigana mpaka maeneo ya Rift Valley hotel baadae wakaanza kitupiana Mawe ikawa vita kati ya wababe wa Isanga na Mafiati huko maguruweni ilifikia mpaka vijana wa Mafiati hawaruhusiwi kukatiza Isanga kwenda kuzika makaburi ya huko wazee wa pande zote mbili waliingilia kati huku kuna kijana mdogo Marehemu Atu Mwaijande ilikua ni hatari...kuhusu Shetani na Yesu walikua washkaji sikumbuki kama walishawahi kupigana nachokumbuka walizima disco lililofanyika Iyunga sec na Chuo cha MTC wao wakitaka kuondoka walikua wanataka disco liishe hao ndio wababe wa Zamani Mbeya miaka hiyo Mbeya usipokua Nunda unaonewa sana...Disco tunaenda kwa mguu popote pale na kurudi usiku muda mwingine hata peke yako....
 
unaweza tu kuongezea nyama maana mimi nimesimuliwa na fasihi simulizi inakuwa na mambo yake kadhaa wa kadhaa hivyo kama kuna sehemu unaweza ongeza nyama ongeza tu lengo hawa wabbe tuweze kuwa enzi angalau hata mara moja kwa mwaka.
Sio ubabe tuu walikua watundu sana pia walikua wanatengeneza Tiketi feki za sehemu yeyote iwe Sokoine uwanjani walikua na Tiketi zao walikua wanatambulika kama FAT ya Isanga... huko kwenye disco wanaenda na muhuri watu wakianza kutoka tuu wanagonga kama ule ule na anagongwa mtu anatoa hela anazama ndani...Baunsa mbabe wa Living stone kuna siku aliyakanyaga alivutiwa Nje jamaa walikua wakorofi sana alipigwa aisee bila sababu na mademu kama huna kundi lenye nguvu hutoki nae hata akiwa wako baadae wakaibuka wakina Kambasonic wa Sangu na kundi lake na Wababe wa Nonde huko walikua wanashindana kuangusha ng'ombe mtu mmoja hapo machinjioni...Ila pamoja na maugomvi yao yote vijana wengi darasani walikua wanaweza hiyo ndio Mbeya enzi za Docks Mwanjelwa kabla soko halijaungua...
 
Mwanza kuna mmoja simkumbuki vzr jina alikua anafunga mtaa, watu wanaenda kulala hata kama ni saa 8 mchana, mwaka jana kalazwa Sekou Toure (hospital ya mkoa mwanza) hawezi hata kunyanyua kijiko cha uji.
Maisha yapo kasi sana
Wasukuma walivyo na miili mikubwa na mwonekano wa mabavu kweli wa kulazwa saa 8 na mtu mmoja?


Huyo jamaa shida nini ilipelekea kulazwa?
 
weweeee hujui wababe walivyo.... nyie miaka yenu hii mna enjoy sana life.. sisi miaka yetu bila kuwa na nguvu utakufa mapema kwa sonono sababu hata demu wanakuchukulia.

Wasukuma walivyo na miili mikubwa na mwonekano wa mabavu kweli wa kulazwa saa 8 na mtu mmoja?


Huyo jamaa shida nini ilipelekea kulazwa?
 
mwaka flani nlienda kumsalimia bibi mkoa flan nyanda za juu kusini.nlikuwa nmeenda na mpira GOZI. mpira huo ilikuwa ni nadra sna kuukuta mikoani.mimi mzee alikuwa anatununulia na wadogo zangu kila mar. nikaenda nao. kule nilikuta wanatengeneza mipira flani hivi kwa kutumia paketi za maziwa wanajaza upepo zinafungwa mbili then zinazungushiwa mpira vizuri zinaka round. inatengeneza mpira wenye sifa kiasi kama za gozi maana nao unaweza kudunda n.k

wakaliona gozi langu wakaniomba nishiriki nao mechi... basi wakachukua ule mpira nami nikapewa namba. shida ikaja nikawa ni mwoga jamaa walikuwa wamekomaa sana.... so nikawa siwezi pambana nao nacheza kwa. kapteni akaamua kunitoa. nikagoma... nikakamata mpira wangu tayari kwa kuondoka. jama alikuja akaupiga mikononi mwangu ukaanguka akaukamata akautia msumari.

wallah nilipandisha mori.. jamaa alikuwa mkubwa kwangu... nilitizama pembeni na kuliona jiwe kuna mawe flani hivi yanakuwa very sharp rangi kama ya kijivu iliyokolea huku dar sijawahi yaona. mikoani yapo. nilimpiga na lile jiwe lilimpasua sentimita chache chini ya jicho.alianguka ... watu kumfuata kumwangalia mimi nlitoka mbio kuelekea home kwa kasi ya ajabu sana.. jamaa waliposhtuka kuanza kunikimbiza it was too late.haraka nliingia ndani na kufunga geti. jamaa walikomea getini. walinambia "dogo tusije tukakuona nje.... utapata shida sana" week mbili nilikuwa sitoki nje ya geti. ilibidi bibi aende kusawazisha yale mambo kwa wazazi wa yule jamaa.

yule jamaa kama jiwe lingeenda juu sentimita chache sana angekuwa kipofu kwa lile jicho milele.... alishukuru Mungu halikufika ile sehemu kwa gap ya sentimita chache sana. nliporusha lile jiwe sikulenga kipige wapi.ila nililenga lipige yule jamaa mhusika.kikafanyika kikao na bibi alilipia matibabu nusu maana aliwaambia nao walipe ule mpira wa GOZI hawakuweza. basi likasuruhishwa hilo suala. mimi baadaye likizo ikaisha nikarudi dar.

kulikuwa na wababe ile mbaya .. kiasi ilikuwa shida sana kusurvive kama umnyonge.
 
Nyokaaa ni habari nyingine huku Arusha...RIP





 
Miaka ya kuanzia 2004 au 2005 km sikosei nikiwa primary alitokea jamaa mmoja maarufu Mbeya aliitwa zebedayo huyu jamaa alikuwa ni balaa kwenye kufukuza upepo achana na ubabe wa kupigana

Kuna mbwa aliiba samaki kwake bwana huyu alimfukuza mbwa yule na hakutaka kumkamata ni swala la kwenda nae sambamba tu. Mbwa yule alikufa kwa kukosa pumzi ligi ilikuwa kubwa

Bwana huyu pia alishawahi kukimbia kutoka town mpaka tukuyu kwenye msiba na wale walipanda magari kutoka town walishangaa kumkuta zebedayo ameshafika eneo la msiba na gari hakupanda
 
Back
Top Bottom