Van Dame(Sinza), Yesu (Mbeya) kati ya Wababe waliowahi tikisa Tanzania

nlikuwa na jamaa yangu ananipa visa na mikasa mbali mbali ya Jiji la Mbeya miaka ya 1980s mpaka 1990s. alianza kunambia jinsi ambavyo miaka hiyo vijana wengi jijini mbeya ilikuwa lazima waende GYM, wajifunze Karate/Kung fu au Tae kwon do na michezo mingine mbalimbali ya mapigano.

mwenyeji wangu ananitajia mmoja ya watu anaowakumbuka miaka ile alikuwepo Daud. huyu kwa watu wengi wa Mbeya miaak ile wanamkumbuka jamaa likuwa amejenga mwili na kujichora tattoo kadhaa mwilini mara nyingi akitembea amevaa singlet kuonesha tattoo zake na misuli yake iliyokuwa imejaa vyema kabisa. huyu alikuwa mbabe,ngumi jiwe miaka hiyo akipiga ngumi uliyepigwa unaona kama umepigwa na jiwe zito sana kutokana na kuwa na nakozi kwenye mikono. wengi walikuwa wakizimia kutokana na ngumi alizokuwa akipiga watu.akaendelea kunipa historia ya wababe wengine waliowahi kutokea jijini humo miaka ya kale.

anasema miaka hiyo alitokea jamaa mmoja alikuwa anaitwa Shetani. jamaa alikuwa ana uwezo mzuri sana wa kutembeza kipigo kwa raia na askari kiasi kwamba askari wenyewe walikuwa wakimgwaya sana. alikuwa kwa mbeya mjini yeye ndiye mtemi anayefahamika. na kama hukukubaliana naye ilikuwa ni jambo rahisi tu mnakubaliana siku ya weekend mnaenda kukutana eneo flani kwa ajili ya kutembezeana mkono mpaka apatikane mshindi.

utawala wa huyu bwana ulikuja kukomeshwa na jamaa mmoja ambaye alikuja kupewa jina la yesu. huyu aliitwa yesu baada ya yeye kuja kumtembezea kipigo kikubwa sana huyo shetani. huyu yesu inasemwa kuwa yeye alitokea Zambia. kufika Mbeya mjini akawa amesikia habari hizo za uwepo wa shetani kuwa ndiye mbabe ile kinyama. na ikatokea siku moja wakakutana katika mizunguko ya maisha katika kutunishiana misuli ikaamuliwa zichapwe.

msimualiaji anasema miaka hiyo walipata nafasi ya kushuhudia ngumi kama za kwenye movie live kabisa bila chenga. zilipigwa ile kinyama. mapigo na ufundi mbalimbali mpaka dakika za mwisho shetani alikuwa hoi vibaya sana na kuamua ku surrender. ndipo yule mbabe mpya alipopewa jina la yesu.tofauti na shetani wanasema huyu yesu alikuwa ni mstaarabu hakuwa akionea watu au kufanya mambo kibabe.

hayo ni mambo ya Jiji la Mbeya miaka hiyo. pamoja na kuwepo pia wababe wengi maeneo mbalimbali jijini humo hasa akisema maeneo kama machinjion,sisimba,sinde,meta,soko matola,mwanjelwa n.k

nikakumbuka miaka ya 200s dar es salaam alikuwepo jamaa mmoja naye shababy sana al maarufu kwa jina la van dame wa sinza. huyu jamaa nilishasikia sana habari zake miaka hiyo na kwa bahati mbaya mimi umri wangu ulikuwa umeshasogea sogea sikuwa naendelea tena na mchezo nliokuwa nikiupenda wa MMA. maana nlijifunza kung fu, nilikuwa mzuri kwenye Katare na kiasi judo. hii ilinipelekea pia nicheze michezo mingi kama Kick Boxing n.k miaka hiyo ya nyuma.

Van Dame alikuwa anasifika sana kwa uwezo mzuri aliokuwa nao wa kurusha mateke. na wepesi katika kuruka na kukimbia inapohitajika. polisi wengi walikuwa wakimgwaya na hata hawakuwa wakitamani kwenda mkamata maana alikuwa na uwezo wa kuwatembezea kipigo kikubwa sana hata wakarudi kituoni wakiwa hoi na wenye hali mbaya kimwili.

tatizo kubwa la Van Dame lilikuwa nasikia ni usela choo mwingi sana. alikuwa akikaba watu au kupora vitu vya thamani na ilikuwa akikufanyi hivyo huna cha kumfanya . ukimpeleka polisi wataishia tu kuandika maelezo na kuanzia hapo wao ndo wanaanza kumkwepa ili wasije wakajikuta wapo katika mazingira ambayo walipaswa kumshika halafu ikawa ngumu.

hivyo polisi wenyewe ikawa ukiwaambia vn dame nimemwona mwenye .... au kijitonyama.. basi siku hiyo polisi hawakanyagi kabisa maeneo ya huko. hali ilikuwa ikizidi sana wanaenda kumwomba aende kituoni naye atawaambia basi haina shida ntakuja baadaye au kesho.

van dame wanasema alikuwa mbabe kinyama.... sifahamu mwishowe aliishia wapi lakini ni mmoja ya watu ambao walikuwa na sifa lukuki katika sanaa za mapigano.

JE MKOANI MWAKO ALIKUWEPO NANI MBABE NA SASA YUPO WAPI? TUENDELEE KUJULISHANA HAYA MAMBO YA KIBABE... KWA SASA UTU UZIMA NA KAZI ZETU HIZI ZINATUZUIA SISI WENGIE TUSIISHI MAISHA HAYA. LAKINI KIUKWELI NI MAISHA AMBAYO MIMI HUWA NAYAMISS SANA. NA ILIKUWA NGUMU KUSIKIA WANAKUWEPO AKINA JUMA LOKOLE... sababu wanaume ilikuwa ni kugangamaa toka ukiwa mdogo. unakua kiume hasa. siku hizi watoto wanavaa mlegezo?

zamani ungevaa mlegezo kuna mbabe mmoja angekuita na kukwambia asikuone tena unakanyaga mtaani KWAKE ukiwa umevaa hivyo sababu next time atakugonga makwenzi kinyama mpaka akili yako ikae sawa. au akuone unatembea kishoga shoga... angekucharaza viboko na kukwambia asikuone tena mtaani unachafua hali ya hewa.


GuDume Bujibuji Mshana Jr Chizi Maarifa @ na wadau wengi wenyeji wa dar na mikoa mingine. Hasa Arusha Macharliee mtupe habari za wababe waliowah kuwepo na walipo mpaka sasa.

hahaaaa hiyo ni zamani mzee baba, sasa hivi...'' ANGEPATA TABU SANA''.......''ANGEPIGWA KIPIGO CHA MBWA KOKO''

1113557
1113559
 
Huyo Van Dame Biscuit tu,enzi zetu dar kulikuwa na wababe Kweli Kweli e.g. Santana,Mwamba Josia,Bob Chura,ukikutana nai disco mbowe hotel au YMCA kama una demu mzuri lazima wakupore
 
Miaka ya kuanzia 2004 au 2005 km sikosei nikiwa primary alitokea jamaa mmoja maarufu Mbeya aliitwa zebedayo huyu jamaa alikuwa ni balaa kwenye kufukuza upepo achana na ubabe wa kupigana

Kuna mbwa aliiba samaki kwake bwana huyu alimfukuza mbwa yule na hakutaka kumkamata ni swala la kwenda nae sambamba tu. Mbwa yule alikufa kwa kukosa pumzi ligi ilikuwa kubwa

Bwana huyu pia alishawahi kukimbia kutoka town mpaka tukuyu kwenye msiba na wale walipanda magari kutoka town walishangaa kumkuta zebedayo ameshafika eneo la msiba na gari hakupanda
Nilijua kuwa itakuwa ni vigumu mno kukosa chai katika huu uzi..!
 
Kuna mbabe mmoja jijini Mbeya alimbaka mwanamke sokoni,watu walikuwa wanaangalia tu,walishindwa kumtetea yule mwanamke kwasababu tu jamaa alikuwa ni mbabe..!
Yule mwanamke aliyebakwa alikuja kujiua...
Hivi ni ubabe au ujinga wa wanakijiji/wanamtaa,mtu mmoja anawezaje kufunga kijiji/mtaa na kufanya anachotaka..!?
 
Kipindi niko shule ya msingi huku mtaani kwetu tulikuwa na mbabe mmoja aliyejulikana kwa jina la Terry Butcher, nakumbuka alikuwa na mwili mdogo tu, lakini jambo la ajabu mtaa kama sio kata nzima walikuwa wanamgwaya..!
Alikujaga kufa kijinga sana baada ya wahuni wenzake kumchoka,jamaa alikuwa hana rafiki wa kudumu..!
 
Hivi mwakayugu yuko wapi?. Nakumbuka mara mwisho enzi hizo aliwaporaga wasukuma karibu milioni 100
Alipopata nadhani hiyo hela alikodi taxi ambayo akawa anazunguka nayo tuu kuna siku Trafiki mwanamke alisimamisha gari aliyopanda Mwakayugu walichofanya akasimama kushuka akatoa kisu na kumpora saa rado na simu na hela maeneo ya Sinde ya magaereza kichotokea baada ya kuisha hela zote walimdaka kirahisi sana kwa kesi hiyo na Ingine aliiba hela hotel moja hivi akahukumiwa miaka mitano nadhani alipotoka akaenda South Africa alikua anaishi Hill brow akaja kutulia kabisa maana kaka yake walikua watu wa kwanza kufanya biashara za Magari kutoa South na S.H.Amon alipewa jembe yupo Dar katulia kabisaa kama sio yeye watu wanabadilika...yeye kwenda dar alikua anazamia train kule kabla halijafika kituoni ashashuka zamani na kurudi hivyo hivyo...
 
Jambazi JoMbi ndio mwisho wamaneno mbeya..
Jombi aliwahi tulizwa na kuibiwa na hilo kundi nae akiwa ametoka kuiba Chunya huko alifanya msako Isanga bila police alivyoenda na gari hakukuta tairi hata moja akakimbilia police kutoa taarifa ya kuibiwa matairi tu na siyo alivyokabwa huko njiani maana hela zilikua za kuiba walikamatwa vijana kadhaa kwa kesi ya matairi ila baadae walitoka...
 
Kipindi niko shule ya msingi huku mtaani kwetu tulikuwa na mbabe mmoja aliyejulikana kwa jina la Terry Butcher, nakumbuka alikuwa na mwili mdogo tu, lakini jambo la ajabu mtaa kama sio kata nzima walikuwa wanamgwaya..!
Alikujaga kufa kijinga sana baada ya wahuni wenzake kumchoka,jamaa alikuwa hana rafiki wa kudumu..!
Hahahahahaha utawala utawala au sio mikono juu na nyinyi apo azimio na maputo yote mlikuwa wazembe tu na mpaka leo mnavumilia upuuzi wa kina mabungo hahajhaha.
 
Ndo utupatie simulizi zake huyo Rodar. Sijawahi msikia.

Alichofanya yesu huyo ili kumpata shetani alimchukua demu wa shetani na shetani akapewa taarifa kuwa wapo bar ya mwasa pale mabatini na ngumi zilipigiwa hapo na yesu akaondoka na demu wake baada ya kumuadhibu shetani lakini hakukupa habari ya demu anaitwa rodar waulize oss kwa nini walikuwa hawakanyagi mbeya wanaogopa rodar demu hatari huyo ukipata simulizi zake
 
Kweli zama zile zimepitwa na wakati,mimi namkumbuka jamaa wa mitaa tuliokuwa tunaishi alikuwa anaitwa Sadru,yeye muda wetu wa kutoka shule ukifika alikuwa anakaa barabarani anakusanya hela na ukipita bila kutoa unachezea kichapo,ilifikia wakati mkijua leo yupo mnapita njia za maporini mpaka mkutane na njia za kufika makwenu,cha kushangaza ni kuwa polisi walikuwepo lakini walikuwa hawachukui hatua...
 
Mwanza kuna mmoja simkumbuki vzr jina alikua anafunga mtaa, watu wanaenda kulala hata kama ni saa 8 mchana, mwaka jana kalazwa Sekou Toure (hospital ya mkoa mwanza) hawezi hata kunyanyua kijiko cha uji.
Maisha yapo kasi sana
Kuna jamaa alikuwa anaitwa Guimo mitaa ya bugando. Mkongwe wa lake sekondari enzi hizo. Nakumbuka fainali moja ya ligi ya kuku. Mitaa ya Nera tulifungwa tukakosa ushindi. Ile tunarudi tukakutana nae akasema haiwezekani twendeni. Mtiti wake mbona tulipewa kombe la kuku.
 
Aisee hizo habar ni kwel.Nakumbuka huyo jamaa shetan baadae alikuja kuishi iringa na peak yake ikawa inaishia ishia akawaga mlevi tu komoni na mbege plus ulanzi.Jamaa akawaga jambazi tu iringa.

Ila hapo iringa alikutanaga na wababe wengine namkumbuka mmoja alikua akiitwa COOL 9 (nine).Hii team ilikua balaa sana

Mbali na mambo yao ya kutembeza vichapo, matukio mengine pendwa pale iringa ikikua fujo zao kwa polis kipind cha mechi za mpira pale uwanja wa Samora.Wanyonge wasiolipa wakawa wanaponea kuingia bure.

Zamani tamu sanaaa
 
mwaka flani nlienda kumsalimia bibi mkoa flan nyanda za juu kusini.nlikuwa nmeenda na mpira GOZI. mpira huo ilikuwa ni nadra sna kuukuta mikoani.mimi mzee alikuwa anatununulia na wadogo zangu kila mar. nikaenda nao. kule nilikuta wanatengeneza mipira flani hivi kwa kutumia paketi za maziwa wanajaza upepo zinafungwa mbili then zinazungushiwa mpira vizuri zinaka round. inatengeneza mpira wenye sifa kiasi kama za gozi maana nao unaweza kudunda n.k

wakaliona gozi langu wakaniomba nishiriki nao mechi... basi wakachukua ule mpira nami nikapewa namba. shida ikaja nikawa ni mwoga jamaa walikuwa wamekomaa sana.... so nikawa siwezi pambana nao nacheza kwa. kapteni akaamua kunitoa. nikagoma... nikakamata mpira wangu tayari kwa kuondoka. jama alikuja akaupiga mikononi mwangu ukaanguka akaukamata akautia msumari.

wallah nilipandisha mori.. jamaa alikuwa mkubwa kwangu... nilitizama pembeni na kuliona jiwe kuna mawe flani hivi yanakuwa very sharp rangi kama ya kijivu iliyokolea huku dar sijawahi yaona. mikoani yapo. nilimpiga na lile jiwe lilimpasua sentimita chache chini ya jicho.alianguka ... watu kumfuata kumwangalia mimi nlitoka mbio kuelekea home kwa kasi ya ajabu sana.. jamaa waliposhtuka kuanza kunikimbiza it was too late.haraka nliingia ndani na kufunga geti. jamaa walikomea getini. walinambia "dogo tusije tukakuona nje.... utapata shida sana" week mbili nilikuwa sitoki nje ya geti. ilibidi bibi aende kusawazisha yale mambo kwa wazazi wa yule jamaa.

yule jamaa kama jiwe lingeenda juu sentimita chache sana angekuwa kipofu kwa lile jicho milele.... alishukuru Mungu halikufika ile sehemu kwa gap ya sentimita chache sana. nliporusha lile jiwe sikulenga kipige wapi.ila nililenga lipige yule jamaa mhusika.kikafanyika kikao na bibi alilipia matibabu nusu maana aliwaambia nao walipe ule mpira wa GOZI hawakuweza. basi likasuruhishwa hilo suala. mimi baadaye likizo ikaisha nikarudi dar.

kulikuwa na wababe ile mbaya .. kiasi ilikuwa shida sana kusurvive kama umnyonge.
Ahahahahahah....kaka umenikumbusha mbali sana.Zaman kukikua na mind set flan kwa watoto wa darcwakija mikoan likizo walikuwa hawa cope kucheza na sisi et wanasema sisi wa mikoan tumekomaaa sanaa
 
Back
Top Bottom