Value Retention ya bodi ya mikopo ni msiba kwa watoto wa watanzania maskini

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,774
2,297
wadau kwa masikitiko makubwa nasema value retension ya 6% ya kila salio baada ya makato ni shida kubwa sana

kwanza wanufaika walilazimishwa kulipa asilimia kumi na tano wakakubali bado haitoshi wamewekewa 6% kila baada ya mwaka wa fedha kweli haki iko wapi.

watu wa sheria wanajua makubaliano ya mwaka jana wakati sheria haijabalika yatabaki yale yale hayataingiliwa lakini awamu hii wakavunja makubaliano hayo na kulazimisha watu wote walipe fifteen percent.

serikali hii inajinasibu serikali ya wanyonge wanyonge gani inawajali?

je msalaba huu kuwatwisha watoto wa maskini na kuwapaka kwa mgongo wa chupa eti serikali ya wanyonge ni sentensi nzuri kweli?

Ebu tujadiliane haya tunapoelekea serikali ya chama kimoja ccm hapo octoba itatokea nini.
 
Kipindi cha nyuma wizara ilikuwa inatoa fungu kufadhili wanafunzi kwenye vyuo vikuu vya umma pekee, mfano UDSM, SUA, Mzumbe na kulikuwa hakuna ujinga kama huu wa bodi ya mikopo. Baadaye mapiga dili yakaleta sheria ya bodi ya mikopo ambapo ufadhili ukatolewa hadi vyuo binafsi wakaanza kufungua vyuo hadi vichochoroni. Hapa suluhisho ni kufuta hili dude linaitwa loan board na kurudisha ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu vya umma pekee...
 
CCM na Magufuli hawajawahi kuweka utaratibu wowote wa utoaji huduma au mpango wowote wa kuwaendeleza wananchi kwa maslahi ya hao wananchi isipokuwa kuwanyonya kupitia mikataba ambayo wanayoipitisha kibabe kule bungeni.
 
Wakati nasoma chuo kikuu..kozi yangu ada ilikuwa milioni moja kwa mwaka .. kwa miaka mitatu total fees ilikuwa milioni 3..

Kwa sasa hivi wanaosoma kozi kama yangu chuo nilichosoma mimi wanalipa milioni moja na nusu kwa mwaka, mwanafunzi wa sasa hivi anatumia total fees ya milioni 4 na nusu kwa miaka mitatu.

Nashangaa wanasema pesa imepungua thamani.m na kutubambikia deni la milioni 20

Ilipaswa wanidai hela ambayo inatosha kumsomesha mwanafunzi wa leo .. maana ndio dhumuni la kulipa deni.. sio sahihi kunidai deni kubwa la kulipia ada wanafunzi wa nne wa sasa wakati mimi walinisomesha mmoja tu
 
Hili la bodi ya mikopo ni kilio cha wengi. Bahati mbaya kila mmoja anapambana na hali yake. Nilikuwa nadaiwa 8m lakini baada ya mabadiliko ya sharia yao limebakia kwenye 4m haliishi.
 
Vyuo vikuu siku hizi zimekuwa kama shule za sekondari hili suala ilitakiwa wanafunzi waliopo vyuo vikuu kupitia serikali zao za wanafunzi na wanafunzi wapinge hii kitu tena kwa nguvu zote maana itawakuta uku watapambana NATO

Ukisema watumishi ni vigumu kukusanyika unatakiwa wanafunzi elimu ya huu wafanye mandamano ya Amani kusema hii value retention free ifutwe
 
Wakati nasoma chuo kikuu..kozi yangu ada ilikuwa milioni moja kwa mwaka .. kwa miaka mitatu total fees ilikuwa milioni 3..

Kwa sasa hivi wanaosoma kozi kama yangu chuo nilichosoma mimi wanalipa milioni moja na nusu kwa mwaka, mwanafunzi wa sasa hivi anatumia total fees ya milioni 4 na nusu kwa miaka mitatu.

Nashangaa wanasema pesa imepungua thamani.m na kutubambikia deni la milioni 20

Ilipaswa wanidai hela ambayo inatosha kumsomesha mwanafunzi wa leo .. maana ndio dhumuni la kulipa deni.. sio sahihi kunidai deni kubwa la kulipia ada wanafunzi wa nne wa sasa wakati mimi walinisomesha mmoja tu
M4 na boom mbona hujaongelea mkuu. Ambalo ndio huwa kubwa zaid kuliko school fee .

Mimi nilitafuna takribani 15m za loan body nimejiajiri sasa sijui hyo pesa yao kama ntakuja kuwalipa , labda inarudi indirect kwa kodi nayolipa
 
Bumu sijaongelea ili summary iwe rahisi.. ndio maana nimeongelea tution fees tu... pia wakati sisi tunasoma bumu ilikuwa 5000 kwa siku.. ambayo hata nikiiweka bumu + ada + field bado haifiki 10m... hivyo loan bodi kudai milioni 20 ama 30 sio sahihi...

Maana hata mwanafunzi wa leo hatumii milioni 20 kusoma kozi niliyosoma mimi
 
Kipindi cha nyuma wizara ilikuwa inatoa fungu kufadhili wanafunzi kwenye vyuo vikuu vya umma pekee, mfano UDSM, SUA, Mzumbe na kulikuwa hakuna ujinga kama huu wa bodi ya mikopo. Baadaye mapiga dili yakaleta sheria ya bodi ya mikopo ambapo ufadhili ukatolewa hadi vyuo binafsi wakaanza kufungua vyuo hadi vichochoroni. Hapa suluhisho ni kufuta hili dude linaitwa loan board na kurudisha ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu vya umma pekee...
Mkuu utaratibu wa kufadhili hadi vyuo binafsi umetoa nafasi kwa wengi na kusaidia serikali tatizo la uhaba wa vyuo.
Utaratibu huu ni mzuri naunga mkono ingawa mimi nimesoma chuo kikuu cha umma na kupata ufadhili 100%.

Hapo shida hayo makato yao na makorokocho mengine ni janga kubwa sana kwa vijana wanao anza maisha.
 
Ndio maana kuna wadau wakimaliza hilo deni wanafanya sherehe.
 
Kipindi cha nyuma wizara ilikuwa inatoa fungu kufadhili wanafunzi kwenye vyuo vikuu vya umma pekee, mfano UDSM, SUA, Mzumbe na kulikuwa hakuna ujinga kama huu wa bodi ya mikopo. Baadaye mapiga dili yakaleta sheria ya bodi ya mikopo ambapo ufadhili ukatolewa hadi vyuo binafsi wakaanza kufungua vyuo hadi vichochoroni. Hapa suluhisho ni kufuta hili dude linaitwa loan board na kurudisha ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu vya umma pekee...
Chuki hii na ubaguzi huu unatoka wapi-hawa wote ni watanzania na wanastahili kupata mikopo. Na vyuo vya umma havitoshelezi uhitaji wa elimu kwa wote Tanzania. Tafakari tena mawazo yako. Nilimpinga sana Kitila Mkumbo alipokuja na wazo kama hili ili tu kuwakomesha Maaskofu walipo andika ujumbe wao wa Easter huko nyuma.
 
Your argument makes a lot of sense.
Wakati nasoma chuo kikuu..kozi yangu ada ilikuwa milioni moja kwa mwaka .. kwa miaka mitatu total fees ilikuwa milioni 3..

Kwa sasa hivi wanaosoma kozi kama yangu chuo nilichosoma mimi wanalipa milioni moja na nusu kwa mwaka, mwanafunzi wa sasa hivi anatumia total fees ya milioni 4 na nusu kwa miaka mitatu.

Nashangaa wanasema pesa imepungua thamani.m na kutubambikia deni la milioni 20

Ilipaswa wanidai hela ambayo inatosha kumsomesha mwanafunzi wa leo .. maana ndio dhumuni la kulipa deni.. sio sahihi kunidai deni kubwa la kulipia ada wanafunzi wa nne wa sasa wakati mimi walinisomesha mmoja tu
 
Chuki hii na ubaguzi huu unatoka wapi-hawa wote ni watanzania na wanastahili kupata mikopo. Na vyuo vya umma havitoshelezi uhitaji wa elimu kwa wote Tanzania. Tafakari tena mawazo yako. Nilimpinga sana Kitila Mkumbo alipokuja na wazo kama hili ili tu kuwakomesha Maaskofu walipo andika ujumbe wao wa Easter huko nyuma.
Mkuu waliokuwa wanasoma vyuo binafsi walikuwa wanajilipia na hilo walikuwa wanalijua, na hata kwenye shule za msingi na sekondari za binafsi serikali huwa haitoi elimu bure huko bali wazazi wanajua wanatakiwa kuingia mfukoni. Sasa uamuzi wa kutoa ufadhili kwa wanachuo wa private lilichukuliwa kwa kukurupuka na kukatokea shida ya bajeti kuweza kuhimili wingi wa wanaohitaji hii mikopo kwa sababu vyuo vilifunguliwa kama njugu. Kwa hiyo suluhisho ni kutoa ufadhili wa masomo kwa wanachuo wanaopata nafasi vyuo vikuu vya umma pekee na kufutilia mbali hiyo bodi ya mikopo.
 
Hiyo imewekwa makusudi ili deni lisiishe.
Yaani ukukuruke kadri uwezavyo lakini deni haliishi kirahisirahisi

Mpaka unamaliza kulipa mkopo, utakuwa umeshasomesha Watanzania kama Watatu hivi bila wewe kujijua!
 
Back
Top Bottom