hassan kisabya
Senior Member
- Jun 14, 2014
- 165
- 109
Habari kwenu,
Kweli moyo kichaka!
Nimepokea kwa masikitiko maelezo yenu na misimamo yenu ya tarehe ya leo toka kwenu wote, naamini hisia hizo ndio ukweli mliobeba mioyoni mwenu.
Nimegundua kumbe siku zote tuliishi pamoja na kushirikiana pamoja kinafiki.
Nimekosa amani, matumaini na kwa kweli sina tena uaminifu na nyie wote hapa. Nakumbuka siku zote tumekuwa tukionyeshana upendo, kuhurumiana na hatimaye kusaidiana, kumbe ilikuwa hila tu, leo nimegundua kuwa mema yoote yalikuwa uongo, unafiki, uzandiki na ulaghai, je kuna tofauti gani na uchawi?
Kumbe hamkuwa na upendo,upendo wenu upo siku moja tu, hii ni aibu kwenu woote, maana hali hii mnaitenda katika majumba yenu na kwa familia zenu ni jambo na hatari kuwa katika mwaka mzima umekuwa unawaongopea watoto wako, mke/mume wako, baba/mama, bibi/babu, shangazi/wajomba na marafiki zako kuwa unao upendo kwao kumbe sio kweli, ukweli ni kuwa siku zote hizo ulikuwa unawasimanga. Eti ila leo tarehe 14/2 ndio siku ya upendo kwako? Unadhani tutaupona moto? Je, hili tumejifunza katika kitabu gani cha Mungu? Kwa maana hiyo baada ya leo unarejea katika unafiki wako.
Mungu anawaona nyie mjue !
Hakika najuta kuwafahamu!