Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,887
Kwakweli walokole wanaume hainifurahisha sana vaa yao.
Hupenda mashati ya kung'aa na rangi za kung'aa. Unakuta shati rangi ya zambarau au njano linang'aa na kola pana. Suruali zao nyingi huwa za kushonesha za kitambaa cha kung'aa. Zamani walikuwa wanashona suruali pana kupitiliza chini. Akivaa tai basi katakua kafupi kanene na kakung'aa vilevile.
Viatu wanapenda vyeupe, cheusi au vya rangi mbili. Kiatu kimechongoka kina rangi nyeupe na nyeusi.
Makoti wana ya aina nyingi. Kuna yale makubwa siku hizi hawavai sana, linakuwa linafika magotini. Unakuta nalo upande mmoja jekundu na ungine jeupe au jeusi. Kuna yale yanakuwa na viraka kwenye viwiko na mengine ya kawaida tu ila yanakuwa yanang'aa kama bati.
Ila jamaa huwa wacheshi sana