Vaa ya walokole hunifurahisha sana

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,886
Kwakweli walokole wanaume hainifurahisha sana vaa yao.

Hupenda mashati ya kung'aa na rangi za kung'aa. Unakuta shati rangi ya zambarau au njano linang'aa na kola pana. Suruali zao nyingi huwa za kushonesha za kitambaa cha kung'aa. Zamani walikuwa wanashona suruali pana kupitiliza chini. Akivaa tai basi katakua kafupi kanene na kakung'aa vilevile.

Viatu wanapenda vyeupe, cheusi au vya rangi mbili. Kiatu kimechongoka kina rangi nyeupe na nyeusi.

Makoti wana ya aina nyingi. Kuna yale makubwa siku hizi hawavai sana, linakuwa linafika magotini. Unakuta nalo upande mmoja jekundu na ungine jeupe au jeusi. Kuna yale yanakuwa na viraka kwenye viwiko na mengine ya kawaida tu ila yanakuwa yanang'aa kama bati.
Ila jamaa huwa wacheshi sana
 
.
images-3.jpeg
 
😂😂😂😂mm nimeishi nao miaka dahari unaweza jiuliza hv huyu mzima?😂😂😂 hao bado wapo iringa na mbeya utacheka ufe..trauza ukiangalia haraka ova sketi !panaaa...alafu kitambaa kinang'aa zaman nilikua na picha kbs dah 😂😂😂sinazo...
 
Hahaha nimecheka sana. Kuna uhusiano gani kati ya ulokole na nguo za kung'aa?
Kuna kitu kinaitwa haiba inajumuisha mwonekano, uongeaji wa MTU, fikra za mtu, uvaaji na yote yanayohusu mtu has a kwa nje na kidogo sana kwa ndani.

Walokole kutokana na mapokeo yao na haiba yao wengi wamejikuta wakivaa namna hiyo.
Hata ukaaji wao kanisani ni wa kipekee bila kusahau uswahili na utapeli.
Nitaongeza nyama muda si mrefu
 
Back
Top Bottom