Uzushi kuwa Kamuzu Banda alikuwa Daktari wa Malkia Elizabeth ulienezwa na nani?

Labda itakuwa Ni Mabeberu tu ndio walizusha au vibaraka wao. Niko kwenye Siti ya mbele kusubiri Jibu la wajuzi. Wewe kaa Cha nyuma hapo
 
Kuna huu uzushi kuwa Rais wa zamani wa Malawi aliwahi kuwa Daktari wa Malkia wa Uingereza na alihasiwa ili asije tembea na Malkia na wakazaa. Eti ndiyo kisa alikufa bila mtoto.

Huu uzushi ulienezwa na nani?

Nchi ambako kiongozi mkuu ni mwongo wa wazi Unategemea vijiweni kuweje mkuu?
 
Kwani hamkusikia kiongozi wa nchi ya kusadikika ni kiongozi wa malaika huko mbinguni?

Tena kabla ya hapo alianza kama mfagizi wa huko mwisho akapanda cheo

Kwani bado hamjui tu mtukufu jiwe wa chattle anavyojinasibu sisi ni dona kantri hata huyo kamuzu alikua hivyo hivyo!

Nadanganya wadau?
 
Kuna huu uzushi kuwa Rais wa zamani wa Malawi aliwahi kuwa Daktari wa Malkia wa Uingereza na alihasiwa ili asije tembea na Malkia na wakazaa. Eti ndiyo kisa alikufa bila mtoto.

Huu uzushi ulienezwa na nani?
Mkuu kipindi kile mataifa yetu ya Kiafrika yalipokuwa katika vuguvugu la kujitawala kulikuwa na euphoria na rumours zilikuwa nyingi.
 
Mkuu kipindi kile mataifa yetu ya kiafrika yalipokuwa katika vuguvugu la kujitawala kulikuwa na euphoria na rumours zilikuwa nyingi
Hapo nakupata, Jamaa waliongoza harakati za uhuru walikuwa wanaaminisha watu wao ni kama demigods. Jamaa kweli alikuwa daktari na amepractice huko uingereza. Pengine walikuza/alikuza kuwa alimtibu malkia ili aonekane babkubwa.
 
Tuliambiwa fimbo ya Baba wa Taifa ilikuwa na uwezo wa ajabu akiiweka Chini hakuna mtu anayeweza kuinyanyua

Sasa sijui kama ilikuwa ni kweli kwasababu alipoaga Dunia tulikuwa tukiambiana kuwa nani atakaeweza kuitoa fimbo ya Taifa Uingereza
 
🎵🎶🎶Nafichaa..nanaa!!🎶🎶..nafichaaa!!nanaa!!!...naogopa isije ikawa noma..nafichaa.. nanaaa!!!...🎶🎶🎶
🚶🚶🚶🚶🚶
 
Mayunga alikua anageuka mti mkavu kwny vita vya Kagera.

Gaidi carlos alikua anapita kwny bomba la maji machafu anatokea bafuni kwa queen elizabeth akiwa anaoga anapiga nae story baadae anasema kimya kimya.

Bongo kwa mapicha picha ni noma sana,No wonder tuliambiwa Idd Amin anakula nyama za watu.
 
Tuliambiwa fimbo ya Baba wa Taifa ilikuwa na uwezo wa ajabu akiiweka Chini hakuna mtu anayeweza kuinyanyua

Sasa sijui kama ilikuwa ni kweli kwasababu alipoaga Dunia tulikuwa tukiambiana kuwa nani atakaeweza kuitoa fimbo ya Taifa Uingereza
Ilibebwa na cranes tatu za tani miatano miatano
 
Kuna huu uzushi kuwa Rais wa zamani wa Malawi aliwahi kuwa Daktari wa Malkia wa Uingereza na alihasiwa ili asije tembea na Malkia na wakazaa. Eti ndiyo kisa alikufa bila mtoto.

Huu uzushi ulienezwa na nani?

Ukweli ni upi?
Yule alikuwa towashi kama yule wa Ethiopia.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuchukiwa na mswahili, yani linaulizwa swali kumuhusu Kamuzu Banda majibu yanakuja kwamba Magufuli ni muongo sana

Mpaka nikaanza kuwaza, pengine sijaelewa mada iliyoko mezani.
Shukrani imhotep kwa ufafanuzi.
Pia nilichogundua, wengi wa watoto hawa wa sikuhizi hawajui Hastings President Omuyaya.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom