Uzuri wa kitu kwa nje si usalama wa ndani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzuri wa kitu kwa nje si usalama wa ndani

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Anyisile Obheli, Mar 17, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Papai jama papai, lanipendeza machoni,
  Kwa yake rangi papai, halinitoki usoni,
  Hata nikifunga tai, nalisogeza mdomoni.
  Nikilikata papai, kumbe lishaaoza ndani

  Ukiliona ni zuri, machoni linavutia,
  Ni kwa yake rangi nzuri, mikononi ukilitia,
  Njano na kijani nzuri, na umbole vyavutia,
  Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani

  Yapo mapapai mengi, kwa zake rangi tofauti,
  Na mitaani kwa wingi, na hayahitaji suti,
  Pia sokoni ni mengi, tena hayana masharti,
  Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani.

  Ni mazuri sana kwa nje, shida yake kule ndani,
  Ukiyaona yalivyo nje, huna swali na ndani,
  Yanavutia sana nje, yanachefua kwa ndani,
  Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani
   
 2. Bavuvi

  Bavuvi Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Papai la Afrika, vitamini limesheneni,
  Ukilikosa hakika, unyafuzi ndani mwilini,
  Kiswahili kimepunguka, peni naweka kabatini,
  Uozo tukiukwepa, unyafuzi utatuua.
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  pole sana ndugu pole, upendaye vya kuoza,
  tumbo kupiga kelele, kitandani lakulaza,
  na njaa isikukele, hata kula vya kuoza,
  kweli ongeza bidii, unyafuzi kuukwepa.
   
 4. M

  Mundu JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  anyisile wa obheli, mbona kwikwi kulikoni?
  umeipata asali, kuila waitamani
  sasa mbona wakejeli, kisa imeoza ndani
  ukimchunguza bata, huwezi kumla ndugu

  vile vinavyopendeza, wenzako wavisifia
  kwafujo wanavikuza, ndo mana vina mikia
  sasa wewe wavibeza, kisa vimejivundia
  ukimchunguza bata, huwezi kumla ndugu

  hata noti za thamani, bidhaa twanunulia
  zimepita pande gani, nawewe kukufikia
  hauziachi kwanini, bidhaa kujipatia
  ukimchunguza bata, huwezi kumla ndugu

  papai ni tunda tamu, lenye ladha maridhawa
  wenzako hatwishi hamu, tulilapo twapagawa
  twala hatujilaumu, hatuhitaji kunawa
  ukimchunguza bata, huwezi kumla ndugu

  kuna njia nyingi mno, za kutafuna papai
  hata ushike kiuno, utaona haifai
  kula utoe miguno, papai hutakinai
  ukimchunguza bata, huwezi kumla ndugu

  kula umechuchumaa, papai litaingia
  au kula umekaa, kitako kujikalia
  papai tunda balaa, utamu wa asilia
  ukimchunguza bata, huwezi kumla ndugu

  papai kama nanasi, twayala kila wakati
  kula kwataka nafasi, na kupanga mikakati
  vinginevyo hutapasi, utaja pigwa kibuti
  papai tunda adhimu, ukisusa sisi twala.
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni ya kweli bwana Mundu, usichunguze ya bata,
  Hata kule kishumundu, wanajivunia bata,
  Wala hana ya utundu, kama ya mbuzi matata,
  Wa muhimu umakini, ili kuboresha afya.

  Mundu uwe na makini, papai na lake umbo.
  Usijesema maskini, na yamenikuta mambo,
  Likioza jalalani, usiliweke kwa tumbo,
  Wa muhimu umakini, ili kuboresha afya.

  Halifanani na bata, lenyewe mwili halina,
  Uchafu akila hata, matatizo ni hakuna,
  Ni halali kumla bata, papai kutofanana,
  Wa muhimu umakini ili kuboresha afya.

  Papai likishaoza, halifai kwa chakula,
  Ni heri kulichunguza, hata kabla hujalila,
  Maamuzi kugeuza, uozo usije kula,
  Wa muhimu umakini, ili kuboresha afya.

  Mimi bado naosia, uzuri wa kitu si nje,
  Tusipende kukisia, tena wala tusionje
  Na bomba twavisifia, tukishaviona kwa nje
  Wa muhimu umakini, ili kuboresha afya.
   
 6. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mi hapo sina changu,papai kulichambua,
  nililipata kitangu,mbolea iliumua,
  pozi papa lipo kwangu,wambea huwaumbua,
  kama lako bovu papa,i njoo uone langu,

  kwa nje linachanua,usukumani patia,
  kwa ndani pia ubua,kufunzwa ndiko papai,
  mkuu hili tambua,asili mia patia,
  kama lako bovu papa,i njoo uone langu,
   
Loading...