Uzuri wa kitimoto dhidi ya nyama zingine

Azarel

Azarel

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Messages
14,129
Points
2,000
Azarel

Azarel

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2016
14,129 2,000
Asalaam Aleikum

Salaam ziwafikie, ama baada ya salaam mimi ni bukheri wa afya.

Leo ninapenda kuandika kwa ufupi umuhimu wa kutumia nyama ya nguruwe maarufu kama Kitimoto. Faida za kutumia kama kitoweo nyama hii ni nyingi sana kama ifuatavyo:-

1) Kwanza Kitimoto ni tamu sana:

Ladha ya Kitimoto ni nzuri sana na humfurahisha kila alaye. Ni tamu kwangu, kwako na kwa yule. Mfano wake walingana ama la wauzidi nyama ya Kuku.

2) Kitimoto ni nyama salama isiyo na Cholestral:

Nyama ya nguruwe ni white meat isiyo na vimelea vya kuleta magonjwa tofauti na nyama ya Ng'ombe, Mbuzi au Kondoo n.k
Ni kama ilivyo samaki na Kuku.

3) Kitimoto inakupatia ULINZI:

Unaweza kujiuliza ni ulinzi kwa vipi? Unajua kuwa walaji wa Kitimoto wengi hawalogeki?

Fanya hivi: chukua mafuta mabichi ya Kitimoto kisha paka kidogo tu katikati ya nyayo za miguu pale palaini kisha ingia katika nyumba yoyote ya mchawi, mfuga majini au mganga wa kienyeji ama kwa yeyote anayetaka kukuroga. Hakika hataweza.

AMA, chukua mfupa wa nguruwe wowote ulioungua kwa kuchomwa au kupikwa kisha uing'inize juu ya paa au mlango wa kuingilia nyumba unayoishi bila hata kunuia chochote. Hakika hakuna kigaragosi wa kichawi au jini atakayekusumbua.

Hongera nyingi ziwaendee ndugu Waislam ambao yamkini wamegundua umuhimu wa nyama hii na kuanza kutumia kwa faida na usalama wao na familia zao, hasa wa mtaa wa Mbagala Zakhem, chamanzi, Kariakoo mwisho na Buguruni pia.


Wabillah Tawfiq
 

Forum statistics

Threads 1,334,524
Members 512,012
Posts 32,479,082
Top