Uzoefu wangu kuhusu maisha ya kijiweni

DMmasi

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
421
648
Leo ningependa kutumia muda huu kushiriki nanyi sehemu ya uzoefu wangu nilio nao juu ya maisha ya kijiweni kwa kuyapitia na kuyaona nitaongelea upande wa vijana wakiume ambao ndio wengi hukaa katika maeneo hayo, kijiwe ninachokiongelea apa siyo kijiwe cha kazi bali ni sehemu ambayo vijana hupendelea kukaa kumaliza siku yao ambapo ni kama majengo ambayo hayajakamilika, mashule(viwanja vya michezo) kwenye mawe n.k

UMRI: Kwa kipindi hiki vijiweni au paite maskani vijana wengi wanaokaa maeneo hayo ni wa umri kwanzia 13_30+ hutegemeana na eneo lenyewe yanii namba ya watu wa eneo ilo imekaaje kiumri

KAZI: Kazi kubwa wanazo fanya vijana wanao tulia maeneo haya ni kazi za kutwa (daywork) kama zile za saidia fundi kutwa unaweka 7,000 _10,000Tzs mfukoni wenyewe hupenda kuziita kazi ng'ombe, wachache wao ni wakusoma na baadhi wameajiriwa na kujiajiri kwenye biashara ndogondogo kama usafirishaji wa njia ya bodaboda

MATUMIZI: Dinari wanazovuna kwenye miangaiko yao mara nyingi huja kukandamiziwa maeneo haya baada ya kulipia kodi ya kulinda penzi kwa dada zetu na kucheza kamari sasa fainali inakuja kuchezekea apa nikumenya kile tulichokipata.

Matumizi makubwa yanayofanyika apa ni kujidunga tu kila mtuu hutumia kile atakachobarikiwa kukishika kwa wakati uliopo aipeleke akili yake masafa ya mbali. Vitu vinavyotumiwa ni kama mirungi, sigara, bangi, pombe zote kienyeji & kiwandani, maji na vinywaji laini.
IMG_20210430_135854.jpg
View attachment 1868269
Nitaongelea upande mmoja wa Mirungi
View attachment 1868271
Mirungi/gomba/mkokaa huuzwa katika vifungashio vya mifuko midogo yenye kufanana naile yenye kubeba sukari ila hiyo huwa ni mizito kiasi na mfuko mmoja huuzwa 2,000_3,000+ kutegemeana na upatikanaji wa mzigo siku iyo
Ili uweze kuutumia mkokaa unaitaji bigG na kinywaji chakushushia , apa mtumiaji X tumpe (mkokaa,bigG na kinywa laini )
Mkokaa 3000
BigG 5@100=500
Kinywaj 2@500=1000
Jumla ni 4,500 kweye perDay yake kabakiwa na 5,500
Akiwa anakula mkokaa kuna kugusa na fegi(sigara)au kushabu(bangi) na kuwatoa na washkajii ili siku na wewe mfuko umetoboka ushikwe mkono na wewe jumla apo tufanye utatumia 1,500 unabakiwa na 4,000 maisha yaendelee
Kula tutaenda kula nyumbani au kama nigeto basi tutajua tukifika naapo niile salio ya 4,000 inaenda kuumia

STORI: Stori nyingi zinazoongelewa maeneo haya ni zilizopo kwenye mzunguko wa maisha ya kila siku yaani ; nini kina trend sana mtaani, stori za mapenzi, stori za mafanikio, muvi, soka, muziki, visa na mikasa kikubwa ni muda uwende tukalalee na stori hizi huwa na mzuka maana kila mmoja huelezea kwa upana wake na utumiaji wa lugha husimama pande zote (stara na matusi)

MAISHA PANDE MBILI

1. UPANDE WA KIJIWE
apa tunakaa wote kwa pamoja tunafurahi pamoja tunacheka na kuhuzunika pamoja "kifo cha wengi ni harusi" pia tunajifunza na kuyajua wanayojua wengine

2. UPANDE WA MWANAKIJIWE:
Hapa sasa kila mmoja husimama katika nafasi yake mwenyewe, nguvu ya kutafuta ni tofauti kama kila mmoja alivyo na alama za vidole zake peke yake, upeo waakili kila mmoja anawakwake uwezo wakujua muda wakuingia kipi chakushika kipi chakuacha na muda wa kuondoka kijiweni ukaishi maisha mengine

MWISHO: wimbi hili lina hasara sana kwa jamii kuliko faidaa maana humo huzaliwa wizi, familia zisizokuwa rasmi na dhaifu, vifo na magonjwa.

CHA KUJIFUNZA NI NINI
Kijiweni kwetu ni sehemu ambayo unaweza ukakaa ukajifunza maishaa au ukapotea kwa wakati (ukapindukia kwenye uraibu wa matumizi ya pombe na madawa), nisehemu yakujifunz na kupata hari ya maisha ujue jinsi ya kupambana kipi niguse na kipi nisiguse kwa kujifunza kwenye picha halisi "picha unaliona mubashara" kijiweni ndipo yalipo madili na ramani za kazi za kutwa ila ni muhimu kujichunga na kuijua nafasi yako katika kuyatengeneza maisha yako na jamii yako yaani familia unapotoka CHEZA KIAKILI CHEZA KWA USALAMA
 
Back
Top Bottom