Uzoefu wangu kuhusu faida za Tembo Card VISA na MASTER CARD | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzoefu wangu kuhusu faida za Tembo Card VISA na MASTER CARD

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mtu Mzima, Jun 14, 2011.

 1. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 379
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mimi ni mteja wa benki inayotoa card za Tembo card VISA na Master Card.

  Nimekuwa mteja wa benki hiyo kwa kipindi kirefu tangu enzi hizo tukiwa tunatumia tembo card ya kawaida.

  Baada ya wateja wote kulazimishwa kuwa na tembo card ya VISA au MASTERCARD mimi pia nilibadilisha na kupata Tembocard Visa.

  Baada ya kusoma matangazo kwenye tovuti yao kuhusu matumizi ya kadi hizo mpya nikavutiwa kutumia huduma hasa ya online shopping.
  Huduma nyingine za kuvutia zilizoorodheshwa ni hizi.

  TemboCardMasterCard

  Features

  With TemboCardMasterCard you can have access to your account 24 hours a day whenever and wherever.

  Withdraw cash at more than 1 million ATM’s globally
  Make purchase at more than 30 million merchants where MasterCard is accepted
  Pay recurring bills
  Shop world wide
  You can track your expenses as your CRDB Bank account will have the list of all purchases made including date, time spent and name of a merchant.

  TemboCardVisa

  TemboCardVisa provides instant and safe access to your bank account from any place and at any time. TemboCardVisa is secured by the VISA Electron assurance and is globally accepted as a mode of paying electronically – through any VISA affiliated merchant outlet or VISA affiliated ATM worldwide.

  Features and Benefits

  Free TemboCardVisa
  Pay for your purchases conveniently using TemboCardVisa
  Pay for online shopping and transactions
  Worldwide acceptance

  Matumizi mengine lukuki yapo:
  TemboCard

  Baada ya kuvutiwa na huduma hizo nilkwenda benki nikajisajili ili niweze kupata huduma hizo hasa ya online shopping.

  Kwa mshangao bado nikawa siwezi kutumia kadi. Baada ya kufuatilia benki nikaambiwa jibu ambalo sikutegemea kupata.

  Jibu lilikuwa kwamba: Kadi yako pamoja na kuwa ina alama ya visa electron ni tembo card ya kawaida, haiwezi kutumika kwa shughuli niliyoomba.
  Nikashauriwa nibadilishiwe kadi.

  Pale benki nikaambiwa kadi nzuri itakayonifaa ni Tembocard master card.

  Mwezi mmoja baada ya kupewa kadi yangu ya Tembocard Master card nikaenda tena kuisajili kwa ajili ya online shopping.
  Siku mbili baadae nilipofuatilia nikaambiwa hizo kadi za Mastercard bado hazijaanza kutumika kwa ajili hiyo kwa hiyo siwezi kutumia kwa matumizi ninyoomba.

  Kuna mambo mawili hapa.

  Moja ni kwamba nimekuwa nikilipa Tsh 6,000 kwa mwaka kama ada ya kuwa na Tembo card Visa kwa takriban miaka 4 wakati kadi yangu ni (Sham au feki visa)

  Pili kwa maoni yangu naona walistahili kuwambia wateja ukweli kuhusu hizi kadi zao za Master card. Ingawa nina wasiwasi pia hata hizo za visa.

  Hayo ndio yaliyonikuta.

  Nimeona ni vema ku-share ili msije mkashtuka mambo haya yatakapowakuta.

  Yawezekana wapo wengi wanaotembea na tembo card za kawaida wakidhani ni visa au mastercard.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,045
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  nenda standard chartered au stanbinc

  upate kadi za kweli....

  nimesikia hata exim bank na diamond trust wanatoa visa card za ukweli.sina uhakika lakini

  crdb ni local zaidi
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 29,268
  Likes Received: 4,246
  Trophy Points: 280
  whaaat? Usiniambie
   
 4. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 891
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nimefanya crdb kwa muda mrefu sana tena department ya tembo card tatizo Crdb kuna staff pale wako sifuri kichwani pengne unabahati ya kuhudumiwa na wanafunzi wa fild, na pengne kama kachoka anaweza kukujibu simple mradi tu uondoke.
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe uliye na majibu tupatie mwenzetu!
   
 6. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 891
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  mbona majibu kayatoa mwanzo kabsa!
   
 7. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mbona mie nilishafanya online transaction kwa kutumia "TemboCard Visa"?, japokuwa haikuwa card yangu, ila niliomba kwa rafiki yangu akatumia card yake na ikakubali, ninachojua mimi ni kwamba inabidi Card iwe "activated" na unaingia mkataba wa kukubali itumike kwa matumizi hayo.
   
 8. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 379
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kama umesoma post yangu taratibu zote unazosema nilizifuata.

  Pengine wewe ulikuwa miongoni mwa wachache waliobahatika.

  Nimetoa tahadhari tu kwa watumiaji wa hizo kadi usije siku moja ukawa na shida ya kuzitumia halafu ukakwama.

  Kwa jumla imani yangu kwa sasa na hizo kadi imepungua sana.
   
Loading...