Uzoefu wangu katika maisha; niliyoyaona katika Mahakama za Mwanzo yanatisha

Mkuu...unapoambiwa kua uyaone ndiyo hayo sasa...Dunia hii unaweza wekwa kwenye kona ukakosa msaada kabisa...

Ukipata nafasi ya kusikiliza stori za wengi walio jela utajiona mwenye bahati sana dunia hii...watu wamepotezwa na life imprisonment zisizo halali ili tu wake zao waolewe huku nje....kusingekua na imani za maisha baada ya kifo watu wengi wangekua wamejiondoa duniani,hususan kwenye nchi zetu hizi ila wanaogopa tu adhabu baada ya kifo kutokana na imani zao.
 
Kiufupi ni mududu ni mengi, ndio maana kuna msemo wanasema mahakama za mwanzo hakuna sheria, serikali ijitahidi kuboresha hizi mahakama kwa kweli la sivyo haki za wengi zitakuwa zinapotea
Mkuu Pole kwa maswahibu lakini hongera sana kwa andiko hili lenye lengo la kuboresha huduma na kukemea ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi katika mahakama za mwanzo hapa nchini.

Mambo uliyozungumza ni mambo yanayofanyika karibu katika mahakama zote za mwanzo hapa nchini. Malalamiko yamefikishwa sana kwa viongozi wa Mahakama ikiwa ni pamoja na Mahakimu wa Wilaya wanaozisimamia mahakama hizo za mwanzo au hata Jaji Mkuu ambaye ndio kiongozi wa muhimili wa Mahakama, lakini utatuaji wa malalamiko umekuwa ni mdogo au usiokuwepo kabisa hivyo kufanya tatizo liendelee kuimarika.

Suluhu ya matatizo haya ni Mahakama kuwasilisha hoja zake kwa Serikali kuwa sheria irekebishwe ili mawakili waruhusiwe kuwawakilisha watu katika mahakama za mwanzo. Ukifuatilia, utagundua kuwa mahakimu wanayafanya yote haya kwa kuwa wanajua watu wengi hawajui sheria na hawana cha kuwafanya ikiwa watafanya watakavyo. Sheria iliyopo inazuia mawakili kuingia mahakama za mwanzo kuwawakilisha wateja wao, jambo hili sio sawa kwa kuwa lipo kinyume na katiba lakini pia limepitwa na wakati.

Kila mtu ana haki ya kuwakilishwa na wakili mahakamani, iwe wakili wa serikali au wa kujitegemea. Kuwazuia mawakili kuingia mahakama za mwanzo ni kwenda kinyume na katiba pamoja na misingi ya haki, mtu kupata uwakilishi wa kisheria. Zamani mahakimu wa mahakama za mwanzo walikuwa na cheti au Diploma ya Sheria, hivyo ikaonekana mawakili (wana digrii za sheria) kwenda mahakama hizo ni kuwanyima uhuru mahakimu sababu wanakuwa hawana uhakika na maamuzi yao kwa kuwa mawakili wamewazidi elimu (huenda wanajua mengi kuliko wao mahakimu. Kuanzia mwaka 2012, Mahakama ikaanza kuajiri mahakimu wenye digrii za sheria wakahudumu mahakama za mwanzo kama mahakimu wakazi, sasa kuna tatizo gani kuruhusu mawakili kwenda huko?? Maana kama ishu ni elimu, mahakimu karibu wote sasa hivi wana shahada za sheria.

Mahakama iruhusu mawakili kuingia mahakama za mwanzo kuwawakilisha wateja, itasaidia sana kupunguza ufedhuli huo unalalamikiwa humu.
 
Rushwa ni adui mkubwa wa haki, hupaswi kufumbia macho vitendo vya rushwa, tia taarifa mara moja TAKUKURU ili anaye kuomba rushwa adakwe.
hakuna aliye juu ya sheria, vitendo vya rushwa sio vya kuvumilia.
mimi nimewahi kutoa taarifa na nikaona faida yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku ukiwa mahakamani, kesi inahairishwa. Siku ukisahau tu kufika mahakamani, kesi inasomwa haraka na maamuzi yanafanyika hapohapo. Utakapostuka, kama wewe ni mlalamikaji basi kesi itakuwa imefutwa na kama wewe ni mshitakiwa basi unaletewa taarifa ya kuripoti lupango haraka sana.
 
Mahakama ni chanzo cha mapato na nguvu kazi (wafungwa) kwa serikali hii. Ukilijua hili wala huwezi kusumbuka kutafuta mchawi nani.
 
Wasalam,

Leo nimependa kushare nanyi baadhi ya mambo ya kusikitisha yanayoendelea katika mahakama za mwanzo na si kwamba yanafanywa na mahakimu wote la hasha bali wachache wenye nia ovu. Naandika haya si kuwa nimesimuliwa hapana ila ni mambo yaliyonitokea miaka ya nyuma kipindi biashara yangu imeyumba. Baada ya biashara kuyumba nikajikuta na madeni mengi yasiweza kulipika kwa wakati huo hiyvo wadeni wangu wakawa wanatumia mbinu mbalimbalia za kunibana, haya ndiyo niliyoyashuhudia.

1. Unaweza kusomewa hukumu imekaa namna hii ila siku ya kuchukua nakala ya hukumu ukakutana na kitu tofauti kabisa. Mfano unaweza kuambiwa unatakiwa kulipa laki moja ila kwenye hukumu ikaandikwa laki 6. Sasa kumbuka uliposomewa unalipa laki moja ulirelax hujujisumbua na rufaa kumbe huku kwenye makaratasi ngoma ni nyingine kabisa yaani.

2. Hakimu anaweza toa hati ya kukukamata kwa nguvu wakati unafahamika ulipo na wala si mtu wa shari l, hujaiba na kesi ni madai. Anayekudai anachonga na hakimu namna ya kukuharass anapewa hati ya kukukamata kwa nguvu anapeleka polisi msako unaanza. Ukidakwa unalala rumande wala hapo huwezi dhaminiwa polisi hadi mahakamani. Na siku ukipelekwa mahakamani hakimu husika anajifanya busy ili mradi tu ushuke magereza hapo kama unachochote lazima ujitikise.

3. Mdai anaweza kufungua kesi na usipewe summons ya kuitwa na ikaendeshwa upande mmoja. Siku moja niko mahakamani kwa kesi nyingine nikasikia jina langu linatajwa ile kuingia kule nikakuta ni kesi nyingine kabisa ambayo siijui na imeshafika mbali.

4. Inaweza kuwa ni madai ukafunguliwa jinai, japo una vielelezo au hata anayekudai akashindwa kuthibitisha jinai yake ila ukaambiwa ulipe faini au kifungo na siku ya pili ukatakiwa kulipa kiasi chote unachodaiwa.

Kiufupi ni mududu ni mengi, ndio maana kuna msemo wanasema mahakama za mwanzo hakuna sheria, serikali ijitahidi kuboresha hizi mahakama kwa kweli la sivyo haki za wengi zitakuwa zinapotea.
Tupe na mbinu ulizotumia kujinasua
 
Mkuu kama ulidharau kulipa deni kwa kugezo halifungi,nasema safi sana kwa kukomeshwa. Lakini kama ni hali ngumu kimaisha pole sana
 
Kama atakuwa amelalamika kuwa alikopesha lakini ametapeliwa yaani makubaliano yamekiukwa kuna uwezekano wa kesi kubadilika kuwa ya utapeli ( jinal )
Umenikumbusha,kuna watu wabishi sana,kuna jamaa anadaiwa kama 70m hivi,mdai kaenda mahakamani mdaiwa kakiri kuwa ni kweli anadaiwa ila kafilisika kwa sasa.kaulizwa so kama umefilisika then uwezo wako ni upi kulipa deni , akasema yeye uwezo wake ni kulipa elfu 50 kila mwezi.mahakama ikatoa hukumu jamaa kila mwezi awe analipa elfu 50.sasa imagine hiyo 70m itamalizika kulipwa mwaka gani?
 
Wasalam,

Leo nimependa kushare nanyi baadhi ya mambo ya kusikitisha yanayoendelea katika mahakama za mwanzo na si kwamba yanafanywa na mahakimu wote la hasha bali wachache wenye nia ovu. Naandika haya si kuwa nimesimuliwa hapana ila ni mambo yaliyonitokea miaka ya nyuma kipindi biashara yangu imeyumba. Baada ya biashara kuyumba nikajikuta na madeni mengi yasiweza kulipika kwa wakati huo hiyvo wadeni wangu wakawa wanatumia mbinu mbalimbalia za kunibana, haya ndiyo niliyoyashuhudia.

1. Unaweza kusomewa hukumu imekaa namna hii ila siku ya kuchukua nakala ya hukumu ukakutana na kitu tofauti kabisa. Mfano unaweza kuambiwa unatakiwa kulipa laki moja ila kwenye hukumu ikaandikwa laki 6. Sasa kumbuka uliposomewa unalipa laki moja ulirelax hujujisumbua na rufaa kumbe huku kwenye makaratasi ngoma ni nyingine kabisa yaani.

2. Hakimu anaweza toa hati ya kukukamata kwa nguvu wakati unafahamika ulipo na wala si mtu wa shari l, hujaiba na kesi ni madai. Anayekudai anachonga na hakimu namna ya kukuharass anapewa hati ya kukukamata kwa nguvu anapeleka polisi msako unaanza. Ukidakwa unalala rumande wala hapo huwezi dhaminiwa polisi hadi mahakamani. Na siku ukipelekwa mahakamani hakimu husika anajifanya busy ili mradi tu ushuke magereza hapo kama unachochote lazima ujitikise.

3. Mdai anaweza kufungua kesi na usipewe summons ya kuitwa na ikaendeshwa upande mmoja. Siku moja niko mahakamani kwa kesi nyingine nikasikia jina langu linatajwa ile kuingia kule nikakuta ni kesi nyingine kabisa ambayo siijui na imeshafika mbali.

4. Inaweza kuwa ni madai ukafunguliwa jinai, japo una vielelezo au hata anayekudai akashindwa kuthibitisha jinai yake ila ukaambiwa ulipe faini au kifungo na siku ya pili ukatakiwa kulipa kiasi chote unachodaiwa.

Kiufupi ni mududu ni mengi, ndio maana kuna msemo wanasema mahakama za mwanzo hakuna sheria, serikali ijitahidi kuboresha hizi mahakama kwa kweli la sivyo haki za wengi zitakuwa zinapotea.
Omba Mungu, ishi maisha ya uaminifu ndo suluhisho, ila inaonekana umekaa kijana haswa, una relax vipi na una Daiwa?
 
Rushwa ni adui mkubwa wa haki, hupaswi kufumbia macho vitendo vya rushwa, tia taarifa mara moja TAKUKURU ili anaye kuomba rushwa adakwe.
hakuna aliye juu ya sheria, vitendo vya rushwa sio vya kuvumilia.
mimi nimewahi kutoa taarifa na nikaona faida yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Takukuru ndio rushwa yenyewe
 
Back
Top Bottom