Uzoefu wangu: Changamoto za uchangiaji damu Tanzania

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,453
3,203
Nimedhamiria kuchangia damu kwa hiari kadiri ya uwezo nitakaojaliwa na Mungu. Nimechangia damu kwa hiari takribani mara nane tangu mwaka 2008. Mara ya kwanza ilikuwa Tegeta High School CTegeta, DSM), 2008, mara ya mwisho ni mwezi wa kumi mwaka huu Hosptali ya Mkoa - Iringa.

Nimefanya hivyo kwa kuwa: naamini hakuna masikini asiye na cha kutoa; hakuna kiwanda cha kuzalisha damu duniani; kwa kuwa nimetumia damu za watu wengi sana nyakati za utoto wangu pale KCMC na Mawenzi; uhitaji wa damu ni mkubwa sana (ikumbukwe damu chafu ni nyingi sana) kutokana na ongezeko la ajali, wagonjwa wa Anaemia n.k. Nimehamasisha ngugu, jamaa, na marafiki kuchangia damu kwa hiari.

Hizi ni baadhi ya changamoto nilizokumbana nazo:

- utaratibu mbovu wa kuhakiki damu salama. Benki ya damu kanda ya Mashariki wanatumia zaidi ya wiki mbili ili kutoa majibu;

- elimu duni juu ya ukusanyaji wa damu. Wauguzi, hususani wa Iringa, wametaka kunizuia nisishangie damu mara kadhaa kwa kigezo kwamba nimechangia damu mara nyingi, hivyo ni hatari kwa afya;

- ukosefu wa utaratibu unaoeleweka wa kukusanya damu. Kuna siku nilitumia zaidi ya masaa manne katika hosptali ya Mkoa - Iringa huku nikiambiwa nisubiri kwani siwezi kufika na kutolewa damu;

- uchaguzi wa makundi ya damu. Kila nikitaka kuchangia, hususani nje ya DSM, nikitaja kundi la damu (A+) wauguzi wanaguna na kusema labda ingekuwa kundi 0, hatimaye kunitoa kwa shingo upande;

- wauguzi nje ya DSM huniambia ninapaswa kuchangia damu mara moja tuu kwa mwaka, wahudumu wa benki ya damu Ilala wananiambia kila baada ya miezi mitatu (wanawake kila baada ya miezi minne);

- wahudumu wanachukulia kitendo cha kuchangia damu kwa hiari kama ni kujipendekeza. Wegi huniuliza "je una mgonjwa?", nikisema HAPANA wanaguna na kuniangalia tena;
- n.k.

Najua changamoto ni nyingi (ikiwemo kuwauzia wagonjwa damu niliyota kwa haiari yangu), na zitaongezeka ila kwa kuwa nimeamua kwa dhamira yangu mwenyewe, kwa kipindi chote nitakachajaliwa kuwa na damu salama, nitacgangia kwa moyo wangu wote. EE MUNGU NISAIDIE!!
 
Safi sana.Una moyo wa kibinadamu, na hata damu yako ni halali mtu kuongezewa pasipo kutozwa fedha. Umetoa kwa hiari itolewe kwa hiari pia
 
Back
Top Bottom