Uzoefu wako tafadhali, mpaka anaenda kufunga ndoa alikuwa na ujauzito wangu

indelible

JF-Expert Member
May 2, 2015
652
299
Salaam,

Miaka kadhaa iliyopita kabla sijaoa nilikuwa na mahusiano na binti mmoja ambaye alitokea kunipenda sana labda hata kuliko nilivyo kuwa najisikia kwake. Nakumbuka siku ya kwanza kumgegeda alilia kwa kwikwi huku akinishutumu kwanini nimemtoa usichana wake wakati alikuwa amepanga kumpatia zawadi mume wa maisha yake, ila ukiniuliza hiyo bikra niitoa saa ngapi kwa kweli mi sikuona chochote mzigo ulikuwa una lika tu na alionekana mtaalam kuliko nilivyo mdhania.


Kwa kweli alikuwa mtamu we was satisfied, baada ya miezi kadhaa alikolea ilikuwa ikipita sikutatu bila kuonana basi nijiandae kujibu maswali yasiyo na kichwa wala miguu,kesi kama hizo nilizimaliza kwa kumpa haki yake na amani ilikuwa inatawala tena.Uhusiano wetu pamoja na kwamba haukuwa rasmi ulidumu kwa mwaka hivi mpaka siku niliyoamua kuuvunja (ieleweke sikupenda kuuvunja makusudi).

Habari nzima inaanzia hapa. Siku hiyo ilikuwa mapema alfajiri kama saa 12 unusu nilisikia muungurumo wa gari ikifunga brake nje ya nyumba niliyokuwanaishi
ilikuwa sio kawaida huyu dada kuja uda huo maana kwao ni gate kali, ilimaanaisha kwamba aliaga kwao (aliagaje kwao mi sijui) aligonga mlango na kuingia ndani, nikamuuliza kuna tatizo gani mbona mapema sana? Akaniambia amemuomba driver wao ampitishe hapo kwa jambo moja tu muhimu.

Amekuja kuniuliza msimamo wangu kama niko radhi kumuoa nakuishi nae hata kama sina kitu, kauli hiyo ilinishitua kwa sababu sikuwa nimejiandaa kuoa na sababu kuu ilikuwa umri wangu mdogo na sikuwa na ajira ya maana. Hivyo nikamjibu kwa swali kwa nini ameniuliza hivyo? Akadai ni kwamba kuna wageni walikuja kwao jana kwa ajili ya kufanya posa kwa ajili yake. Lakini amewaomba wazazi wake wasijibu chochote kwenye posa hiyo mpaka atafakari kwanza, ndio atakapokuwa tayali kuwajibu ndiyo au hapana (kwa maana ya kuja kuniuliza mimi kwanza)

Nilimjibu kwamba mimi siwezi kumuoa na ikiwa anahitaji ndoa na amejitokeza mtu ambaye anaweza kufanya hivyo basi aendelee nae. Kwa kweli aliangua kilio sio cha kawaida huku akinisisitiza nimkubalie, nilimuonea huruma lakini sikuwa na jinsi ya kufanya. Nilimbembeleza mpaka akaonekana kunielewa,ila kabla ya kuondoka akaomba tuagane maana yeye atalazimika kuolewa na huyo bwana (Ingwa hawakuahi kuwa na mahusano kabla). Kama kawaida akapata kitu roho inapenda. Baada ya pale ndio ukawa mwisho wetu.

Sasa basi juzi hii kanitafuta kunieleza kwamba mpaka anaenda kufunga ndoa alikuwa na ujauzito wangu na inamaana kwamba kijana wake wa kwanza ni wangu. Ameshindwa kuendelea kumnyima mwanae haki yake ameona anitaarifu. Nimechanganyikiwa lakini pia ninafuraha maana huyu mke nilie nae kwa kweli tunaendelea kuhangaika sana hajapata mwana (Siwezikuelezea kwa undani kwanini hajapata mwana)


Sasa najiuliza nifanyeje, nitamwambiaje wife! Itakuwaje kwamumewe? Mtoto nae atanielewa? I am stillconfused, nifanyeje?.

Nawakilisha
 
mweleze tu huyo mkeo asipo kuelewa mpotezee mana wewe huwez kuitupa dam yako
Mmh naanzaje? Shida ni kwamba kijana kwa sasa anasoma standard six na sikuwahi mwambia wife habari yoyote ya mimi kuwa na mtoto kabla. Swala jingine ni huyo mume wa huyu dada atalichukuliaje hili au napaswa kukaa nae kitako?
 
Huyo dada anaweza kuhatarisha ndoa yake kama yule bwana hakuwahi kuambiwa kuhusu ujauzito
 
Huyo dada anaweza kuhatarisha ndoa yake kama yule bwana hakuwahi kuambiwa kuhusu ujauzito

Hajui ila mzazi mwenzangu anasema hiyo guilt conscious inamsumbua and she is ready to face all the consequences. Mi naona nina kibarua cha ziada sikuwa nimjiandaa kulikabili hili swala.
 
mweleze tu huyo mkeo asipo kuelewa mpotezee mana wewe huwez kuitupa dam yako
Inaniingia akilini lakini haikai...mkuu, kifupi wife ninamengi nae pamoja na kutopa mtoto lakini nakapenda haka kabint aisee.
 
Ukweli una kila haki ya kudhihirishwa, ukweli ni kama chafya ilikujia ghfla. Its a time to expose it out in the open.
Tofauti na hapo ni sawa na kuuficha/kuufutika moto uwakao katika nyasi kavu.
 
Kama yeye keshaolewa, na wewe tayari una mke kwa maana unajiweza sasa hivi. Mwambie ukweli mkeo na yeye kule kwa mume wake aseme ukweli. Acha na yeye aachike alafu muoe sasa.
 
Kama yeye keshaolewa, na wewe tayari una mke kwa maana unajiweza sasa hivi. Mwambie ukweli mkeo na yeye kule kwa mume wake aseme ukweli. Acha na yeye aachike alafu muoe sasa.
Ni maoni ushauri au mapendekezo?
 
Hajui ila mzazi mwenzangu anasema hiyo guilt conscious inamsumbua and she is ready to face all the consequences. Mi naona nina kibarua cha ziada sikuwa nimjiandaa kulikabili hili swala.

Wazee wazamani wakati mwingine walikuwa wanalea watoto sio wao na hii ilisaidia kudumisha ndoa zisivunjike
 
Unafikiri akimweleza mumewe ndoa yake itakuwa salama je nawe ndoa yako upo tayari kuipoteza
 
Ukweli una kila haki ya kudhihirishwa, ukweli ni kama chafya ilikujia ghfla. Its a time to expose it out in the open.
Tofauti na hapo ni sawa na kuuficha/kuufutika moto uwakao katika nyasi kavu.
is it real that sometime classified is essential or its depend on what are you trying to hide?
 
Back
Top Bottom