Uzoefu wako tafadhali, mpaka anaenda kufunga ndoa alikuwa na ujauzito wangu

Vitu kama hivyo huwa havisemwi.
Ili mradi wewe umeshajuwa imetosha.

................. ninayo mifano hai...........
 
Unamaanisha nipige kimya? What if mke wangu akilijua hili kupitia watu wengine?

hekima inahitajika hapa kumbuka yule bwana hajui chochote na sio kosa lake couse hakuambiwa toka mwanzo sasa fikiria amelea mimb hadi mwana leo anaambiwa sio wake unategemea nini kitatokea hapo...........wazee wetu nina mifano mingi tu katika familia ya watoto 5 mmoja sio wa baba huyo baadae wanakuja fahamu lakini kwa busara wanachukulia poa lakini sio kwa kizazi hiki aise
 
Achana na hiyo biashara ya kutaka mtoto wakati wazazi wake wapo hai..kwanini hakukwambia wakati bado ni mimba changa unafikiri alikuwa hajui kama mimba si ya mmewe wa ndoa??? Aliogopa kuachika sasa kwanini anataka kusema sasa???.tena wametunza for 12 years...ungejua jinsi mtoto anavyosumbua toka utunzaji wa mimba mpaka anatimiza five years ungekaa mbali na hiyo issue maana huyo mme anaweza toa uhai wako....
Unamaanisha nini kusema niachane na hiyo biashara ya kutaka mtoto wakati wazazi wake wapo hai! kumbuka i was blind till she come and confess on me she that the kid is mine. Nafahamu malezi yalivyo even though sina uzoefu sana wa kulea but nakuelewa. Ingekuwa ni mimi nimeenda kumdai that was another case lakini kaja mwenyewe anadai moyo unamuuma kuona anambambikia mumewe mtoto na si wake.
 
Vitu kama hivyo huwa havisemwi.
Ili mradi wewe umeshajuwa imetosha.

................. ninayo mifano hai...........

kweli unapiga kimya maisha yanakwenda.....huyu anapata pressure kwa vile kwa mkewe hakuna mtoto......najiuliza yule dada mwenye mtoto anataka nini wakati toka mwanzo alishindwa kumweleza mumewe mimba sio yake leo anataka kuharibu labda kashamchoka huyo mume anaamua liwalo na liwe.
 
I spoke to her this morning and asked the same question lakini anasema ameokoka si kwamba kamchoka mumewe ndio maana anahisi anaendelea kukaa katika kifungo cha dhambi ya uongo kwa mumewe anae mpenda kwa dhati.
 
mumewe naye ameokoka je atamwelewa kwa issue hii?...... asikurupuke kwanza nishasema inatakiwa hekima na busara swala zito hilo
 
Ni mimi nimekosea kusema au ni mzazi mwenzangu kakosea kuniambia!?

Wewe ndio unaonekana mmbea kuja kusema huku mambo ambayo unajua fika ni ngumu kuyaleta,yaan mtu miaka 12 anyamaze kimya leo akwambie kuwa mtoto wako baas wewe huyoooo JF kutoa dukuduku? Jiangalie ndugu na tumia hekima,huyo mama inawezekana ana personal/marriage conflicts na mumewe ndio maana kaona ayaseme hayo au wewe hali ya kukosa mtoto inakuweka hatiani. Fikirieni yule baba mwingine mtaumiza hisia zake kiasi gani,halafu huyo mtoto usidhani ataku-feel they way you expect him/her to!!

BE WISE!
 
Huyo mama ana watoto wangapi hadi sasa? naamini mumewe anajua kuwa watoto walionao wote ni wake, na pia huwezi jua ni kwa kiasi gani huyo baba anampenda mwanae wa kwanza, pia huwezi kujua uchungu atakaopata huyo baba baada ya kuambiwa na kuthibitisha kuwa kweli huyo mtoto si wake. Kuna hatari kubwa ya ndoa ya huyo mama (x wako), mwambie x wako, ajaribu kusoma uelekeo wa upepo kwanza kwa huyo mumeo; Anaweza kufanya vitu kama;

  • Kumpa stori inayofanana na hiyo halafu ktk maongezi baada ya stori hiyo akamuuliza kwa utani wenye ukweli ndani yake kama yangempata yeye angefanyaje?
  • Au akatafuta namna ya kuuliza ktk hali ya furaha na kimatani hivi, ili tu aweze kusoma mood ya mumewe hata kabla ya kuamua kupasua hilo bomu.

Pia kumbuka huyo mama ndiye anajua ni kwa jinsi gani mumewe anaupendo juu ya wanawake na watoto kwa baba pia. Maana mtoto ameshajidhihilishia kuwa huyo ndiye baba yake na ukute anampenda sana sana, leo mumgeuzie kibao gafla.

Pia nashauri kama itaonekana upepo unaelekea pabaya, mwambie huyo x wako asiseme atulie tu, na msubiri tena labda mtoto akue zaidi na awe na akili ya kiutu uzima, halafu aambiwe hapo badae kiutuuzima zaidi. (japo inategemea na mtu), lakini mimi naamini akiwa mtu mzima mkamwambia kiutuuzima itakaa vizuri na akapewa ushauri zaidi, atajua kuhandle baba zao, na inaweza isimuathiri sana kisaikolojia.
 
Ni kweli kabisa naweza kuwa mbea... but kwenye kizazi hiki social media ikitumika vizuri inaweza kuwa babu na bibi katika kupashana habari kupeana uzoefu na nk. Nadhani kuna ambayo siwezi kuyaleta hapa hasa ambayo ufumbuzi wake ninao au yanayo toa taswira ya kudhalilisha human dignity siwezi kamwe.

Kwa swala hili lililonikuta naweza kuwa nawagusa wengine ambao nao wangependa kujua maamuzi gani ni sahihi kuyafuata. Hata kama ushauri huu wa hapa ni pamoja na kuchanganya na akili zako. turudi kenye mada.

Hisia za mumewe nazijali lakini pia kwa umri wangu huu na sina mtoto na Mimi naona kama Mungu kanifungulia mlango na kuniondelea upweke nilionao wa kukosa mtoto sasa kaja lakini kwa njia ambayo ni ngumu sana kuitatua kwangu kwa sasa. conflict sijui sana kama zipo na kwa kiwango gani ila nilipo muuliza ndio kadai anataka kuivua dhambi ya uongo...hivi nikweli truth will set you free au kunabaadhi tu ya mambo!?
 
Mkuu nakuelewa vizuri sana umeniambia kitu kimenigusa..asante

Sijui huyu mumewe atalichukuliaje swala hili lakini ninamashaka sana na usalama wa kila mmoja.

Mkuu mimi nina wasi wasi isije ikatokea kama yaliyotokea juzi mabibo, ambapo mwanaume alimchinja mtoto baada mama kufumaniwa kisha kumweleza mmeww kwamba hata yule mtoto hakuwa wake!!!!
 
hekima inahitajika hapa kumbuka yule bwana hajui chochote na sio kosa lake couse hakuambiwa toka mwanzo sasa fikiria amelea mimb hadi mwana leo anaambiwa sio wake unategemea nini kitatokea hapo...........wazee wetu nina mifano mingi tu katika familia ya watoto 5 mmoja sio wa baba huyo baadae wanakuja fahamu lakini kwa busara wanachukulia poa lakini sio kwa kizazi hiki aise

Hakuna kitu kinachouma kama kupokonywa mtoto uliyemlea na kumsomesha mpaka anafikisha umri wa miaka 12. Mtoto unayemuita my first born, kama ni wa kike unamuita mama kama ni wa kiume unamuita baba, leo atokee mtu eti huyu ni mtoto wangu? Katika issue hii naiona hatari kubwa zaidi ya kunjika ndoa, kuna hatari ya kuondoka na uhai wa mtu. Cha msingi kabla hajaambiwa lolote huyo mwanaume ni vyema kukaa kitako na kuuongea kwa kina na kuangalia jinsi mtakavyotatua matatizo yatakayotokea mbeleni. Kingine, washirikishe wazazi wa mwanamke maana huyo mwanaume ndiyo anatambulika huko ukweni, pia kapime DNA.
 
Mkuu mimi nina wasi wasi isije ikatokea kama yaliyotokea juzi mabibo, ambapo mwanaume alimchinja mtoto baada mama kufumaniwa kisha kumweleza mmeww kwamba hata yule mtoto hakuwa wake!!!!

nimeona picha ulikuwa ni unyama wa hali ya juu, Mungu ampumzishe kwa amani yule mtoto. Kilikuwa kitendo kibaya sana sheria ifuate mkondo wake.
 
Kama kaokoka na hataki kumdanganya mume wake anayeita mpenzi urudishe kwanza bikra yake. Akiweza hilo amwambie mmewe ukweli kuwa mtoto sio wake. Akishindwa atulie maana naona kabisa uhai wa mtu/ watu ukipotea.
 
Ni kweli kabisa naweza kuwa mbea... but kwenye kizazi hiki social media ikitumika vizuri inaweza kuwa babu na bibi katika kupashana habari kupeana uzoefu na nk. Nadhani kuna ambayo siwezi kuyaleta hapa hasa ambayo ufumbuzi wake ninao au yanayo toa taswira ya kudhalilisha human dignity siwezi kamwe.

Kwa swala hili lililonikuta naweza kuwa nawagusa wengine ambao nao wangependa kujua maamuzi gani ni sahihi kuyafuata. Hata kama ushauri huu wa hapa ni pamoja na kuchanganya na akili zako. turudi kenye mada.

Hisia za mumewe nazijali lakini pia kwa umri wangu huu na sina mtoto na Mimi naona kama Mungu kanifungulia mlango na kuniondelea upweke nilionao wa kukosa mtoto sasa kaja lakini kwa njia ambayo ni ngumu sana kuitatua kwangu kwa sasa. conflict sijui sana kama zipo na kwa kiwango gani ila nilipo muuliza ndio kadai anataka kuivua dhambi ya uongo...hivi nikweli truth will set you free au kunabaadhi tu ya mambo!?

Truth will set u free its true ila angalia historia ya hilo tatizo na limetokea katika mazingira gani,wewe shukuru tu kuwa una damu yako somewhere that should be enough for you. Na iyo dhambi anayoiona huyo mama ya uongo aongee na mungu tu katika ibada zake hakuna kubwa wala dogo kwa mungu. Mengine mtakuja kuzua matafrani sana,mimi ni mmoja wapo ambao nimezaliwa katika situations kama hizo I know how it feels wala huna haja ya kuzua mapya.
 
Back
Top Bottom