Uzoefu na Mazingaombwe yaliyopo kwenye uchimbaji Madini/Migodini

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,265
23,029
Wadau, kumekuwa na habari nyingi za kutisha na pia visa na mikasa mbalimbali inayotokea wakati wa shughuli za kuchimba madini hasa dhahabu.

Jamaa mmoja alikuwa anasimulia hapa jinsi rafikiye alivyopata kichaa akiwa ndani ya shimo la dhahabu, anasema walikuwa wawili mstari wa mbele kabisa wanaelekea kuchimba sehemu ambayo ndio inaonekana dhahabu imelala pale, walionana na mwanamke mzuri sana wa Kiarabu ananukia ile haswa.

Yule rafikiye akaona yule dada analeta usiku wakati mentali ameenda kuzisaka ndalama, akamfuata na kumwambia aondoke ile sehemu asilete urembo.

Jamaa anasema issue nzima ilikuwa jamaa pia alishakula msuba so hata hakuwa na mshtuko. Wakabishana sana yule mwanamke anataka asisogelewe sababu jamaa ana madude kichwani(msuba)

Jamaa anasogea akifoka kuwa hajaenda kutafuta mademu Mwanza kaenda kupiga kazi asiwekewe usiku, ghafla alipigwa kumbo. Alipokuja amka jamaa alikuwa tayari kichaa.

Huyu mwenzie anasema hakuweza mwambia mtu kesho yake tu asubuhi alikuwa kwenye bus anarudi Muheza.akaendelee na maisha mengine.yule jamaa mpaka kesho ni kichaa.

Tuleteeni mikasa mingjne toka kwenye uchimbaji madini.
 
Mbona kisa hiki haujakimalizia vizuri?

Huyo aliyerudi Muheza alifanikisha kupata hayo madini, je huyo mwanamke wa kiarabu alipisha baadaye akafanikisha kuyapata?

Na kama siyo, ukanda huo ulijulikanaje kuwa ulisheheni madini?

Maswali yanskuwa ni mengi kutokana na ulivyoiseti simulizi yako kwa mapungufu.
 
Cha Arusha hakijawahi kumuacha mtu salama
 
Wa muheza hakuendelea tena na shughuli akaona bora arudi home kwao.

Wataalam wanasema kuna maeneo kunakuwa na dalili kabisa za uwepo wa madini na pia kuna viashiria.

Mbona kisa hiki haujakimalizia vizuri?

Huyo aliyerudi Muheza alifanikisha kupata hayo madini, je huyo mwanamke wa kiarabu alipisha baadaye akafanikisha kuyapata?

Na kama siyo, ukanda huo ulijulikanaje kuwa ulisheheni madini?

Maswali yanskuwa ni mengi kutokana na ulivyoiseti simulizi yako kwa mapungufu.
 
Ukiafuta kitu kwa haki utapata kwa haki,

Ngoja wa Apollo plus billionaire leizar aje aseme kama ni kweli maana zile Billion sio mchezo
 
Huyo mwanamke wa kiarabu naye alikuwa frontline, kabeba sululu kama masela....au aliingia tu kuuza sura na kuhanikiza manukato humo shimoni..
 
Huyo mwanamke wa kiarabu naye alikuwa frontline, kabeba sululu kama masela....au aliingia tu kuuza sura na kuhanikiza manukato humo shimoni..
jamaa yetu baada ya kuvuta mpepe,naona wazo lililomjia ni kama hili lako.

akaona huyu demu vipi,kashindwa kupaka mafuta juu huko anakuja kupakia chini humu,kumbe jini.
 
Kuna majaamaa wawili huku mtwara walienda kuchimba madini ya lubi huko msumbiji walipambana Sana Lakin hali ilikuwa mbaya wezao machimbo mengine waliokuwa wanatusua lubi wanarudi nyumbani Tanzania wanaanza maisha sasa nao wakaamua kujiongeza kwanini wezetu wanapata na sisi tunachezea njaa wakaamua kwenda kwa babu wa kimakonde huko msumbiji Wakamuelezea kila kitu akawajibu hayo ni mambo rahisi Sana akawambia nendeni mkachimbe chochote mtakachokiona uweni mkiona mjusi piga mende, nyoka, chochote kile wewe piga basi Bana watu wakaenda kupiga kazi wakaingia shimoni piga jembe piga sululu wakamuona mende wakapiga wakaendalea na mzigo mara akatokea mjusi jamaaa Kati yao anataka kupiga tu yule mjusi akageuka sura ya baba ake a Kasema aaaaah baba mwezie akawambia vipi akamwambia huyu baba umuoni. Mwezie mbona huyo mjusi piga bhana akitaka kupiga tu mjusi anageuka sura ya baba ake jamaa akata tupa jembe aka toka nje kutoka nje jamaa akawachizi bahati mzuri watu wakamkamata yule mwezie akawaelezea kwamba tulienda kwa babu fulani wakaenda kwa babu wakamuomba samahani babu akawa samehe.machimbo sio poa
Duu Aisee
 
Ayaa sasa hapo si walitakiwa waache warudi kwa Sangoma waeke nae maridhiano huyo muarabu kweli hao vilaza
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom