kaisa079
Member
- Nov 16, 2007
- 20
- 4
Kama unaishi katika nyumba iliyozungushiwa uzio ,tena na wengine wanaweka electrical security system na Mageti makubwa na walinzi milangoni hivi umewahi kufikiri ni kwa nini uliamua au mzazi wako aliamua kuweka uzio?.Waweza sema ni kwa ajiri ya ulinzi wako mwenyewe na usalama wa mali,hiyo ni mojawapo ya fikra,ila umewahi kufikiri kama mimi nnavyofikiri?
Ni kawaida kuona watu wako katika magari ya tintled wasionekane,acha hawa wenye uzio mrefu wa nyumba,hivi kweli imefikia hatua binadamu tunaogopana kiasi hiki?.Yaani watanzania ka watanzania tunaogopana? Why? Kwa nini? Jibu ni TOFAUTI KUBWA ZA KIMAISHA kati ya walionacho na wasionacho! Leo wenye nacho inabidi waweke uzio kuwazuia wezi au vibaka,vibaka na wezi ambaowameamua kuwa wezi kwa kuwa kuna mgawanyo usio sawasiwatetei kwa matendo yao,lakini sku moja nliwahi kuporwa nauli yangu katika mtaa wa kongo na kibaka,bahati mbaya kwake na nzuri kwangu nilimshika mkono wake alokuwa akupenyeza mfukoni mwangu,huweziamini niliuwa na 500 kama nauli ya kunifikisha uswahilini nilikoishi,nilimuangalia sana Yule kibaka,kasha nikagundua alionekana hajapata japo Break Fast mmh! Nikaamua kutafuta chenji nikamgawia 250 hii ni kwa sababu niligundua ni hali ngumu ya maisha ilimsukuma kunipora na hata kama angeenda kwa Matajiri waliozoea kujizolea misifa mikubwa kwa kutoa msaada kwa vikundi mbalimbali huku wakiambatana na waandishi wa habari wakawarushe katika news asingepewa hata sumuni.Na iwapo nisingempa fedha shida ilomfanya aibe bado ingebaki pale na labda victim mwingine angekwa ndugu yako!Jao sijui kama siku hiyo hakumuibia tena mwingine lakini jambo nialosisitiza hapa ni kuwa kwa kuwa hakuna mgawanyo sawa wa rasilimali ni lazima vibaka watakuwa wengi,majambazi watakuwa wengi na wenye nazo watazidi kuweka nyaya za umeme mpaka katika vioo vya magari ili kibaka akiguswa anaswe.
Hebu fikiria kama wote tungekuwa na mali kwa kiwango kinacholingana japo bado wangekuwapo akina Yuda Iskarioti wengi wenye tama,lakini angalau huku kuogopana kusingekuwepo,imefikia hatua hata ukimsimaisha bosi Fulani kumpa hi first impression yako kwake ni Kibaka
Hebu tusiogopane jama,kama hawa matawi ya juu wanajiwekea mageti bwana acha sisi tuendelee kusaidiana chumvi,maharage na moto wa kuwashia mkaa huku kwetu uswahilini,ila wananiudhi saa hawa watu siku hizi wameanza kutufuata nakujenga na kujiwekea mageti hukuhuku uswahilini kwetu.Mbona mwatufuatafuta? Kwanza mlituona vibaka tukawapisha huko kwenye majina ya kizungu..sijui nini nini .beach,sijui nini nini ..bay,sijui nini nini panga!
Tusichukiane wale iliowagusa hii ni haki yangu kusema ninachojisikia,uhurumaoni.Acha niishie hapa niwahi kibaruani bwana nsije nikaonwa nam Kibaka.Tajiri akinilipa kaujira nika save kidogo nitarudi tena hapa internet café nikupe mchapo mwingine.
Kwa maoni,Ushauri
Niandikie
Kaisa079@yahoo.com