Uzinzi wamsimamisha mchungaji madhabahuni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
MCHUNGAJI wa Kanisa Anglikana Parishi ya Pandambili Jimbo Kuu la Mpwapwa-Kongwa mkoani hapa, Petro Namga, amesimamishwa kazi kutokana na kashfa ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muumini wake.

Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Dk. Jacob Chimeledya, alilithibitishia gazeti hili jana kutokea kwa tukio hilo na kuwa tayari hatua za awali zimechukuliwa dhidi ya mchungaji huyo.

Alisema kutokana na kashfa hiyo, mchungaji Namga amesimamishwa kutoa huduma katika Kanisa la Parishi hiyo, kwa muda wa miezi mitatu kama hatua ya awali huku uchunguzi ukiendelea.

Askofu huyo alifafanua kuwa uamuzi huo ulitokana na uchunguzi wa awali uliofanywa na viongozi wa Kanisa ngazi ya jimbo na kubaini ukweli wa mchungaji huyo kufanya hivyo kinyume cha taratibu na Sheria za Kanisa.

“Hatua zaidi zitachukuliwa kwa kuwa kitendo kilichotokea ni utovu wa nidhamu na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya huduma za kiroho,” alisema Askofu Chimeledya.

Aidha Askofu huyo alibainisha kuwa kitendo hicho kimeliaibisha Kanisa na hawezi kuendelea na kazi ya kumtumikia Mungu.

Mchungaji Namga anatuhumiwa kwa kashfa hiyo, baada ya simu ya mwanamke huyo kukutwa na ujumbe wa mapenzi kutoka kwa mchungaji huyo. Mmoja wa waumini wa Kanisa hilo, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alidai kuwa baada ya mwanamke huyo kubanwa, alimtaja mchungaji huyo kuwa ndiye humtumia ujumbe huo wa mapenzi.

Alifafanua kuwa mume wa muumini huyo, alikuta ujumbe wa mapenzi katika simu ya mkewe na alipombana zaidi kuwa ujumbe huo ulitumwa na mchungaji huyo ambaye alikuwa akimtaka kimapenzi kwa muda mrefu.

Mume aliwaagiza baadhi ya watu kwenda kumweleza mchungaji huyo juu ya tabia yake lakini hakuna kilichobadilika, kwani aliendelea kumfuatilia mkewe.

Aliongeza kuwa kutokana na mchungaji kuendelea na tabia yake alimwekea mtego na kumkamata akiwa na mkewe na kuifikisha kesi hiyo katika uongozi wa juu wa Kanisa hilo.

Muumini huyo alifafanua kuwa baada ya vikao kadhaa vya usuluhishi kati ya mume, mchungaji na uongozi wa Kanisa, tangu Januari mwaka huu, hatimaye walifikia muafaka, ambapo Februari 25 mchungaji aliamriwa kulipa faini ya Sh 100,000.

Pamoja na faini hiyo pia viongozi wa juu ngazi ya jimbo akiwamo Askofu Mkuu, walikubaliana kutoa adhabu ya kumsimamisha mchungaji huyo mpaka uchunguzi wa kina utakapofanyika.

HabariLeo ilimtafuta Mchungaji huyo lakini alipopigiwa simu na kujulishwa juu ya suala hilo, alikata, na baadaye alipopigiwa tena simu iliita kwa muda mrefu bila majibu na hatimaye kuzimwa.
 
Mmh! Nao ni watu wenye hisia kamili. Udhaifu wa mwili huo, japo wengine wanajipumbaza wakidhania watumishi wa Mungu hawana tamaa. Roho ni imara lakini mwili ni dhaifu.
 
Amini amini nawaambia ole wake mtu atakaye wakwaza wadogo hawa. Kwa maana ingalikuwa heri kwake kufungiwa jiwe la kusaga shingoni mwake na kutumbukizwa katika kilindi cha bahari ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Huyu mchungaji badala ya kuwaongoza watu katika njia ya wokovu yeye anawaongoza katika njia ya jehanamu.

Hivyo ni haki yake kutimuliwa
 
Mbaya sana, sio nzuri, ila watu wataweka asante na pale sasa sijui ni kumshukuru mtoa mada au mchungaji huyu firauni? Nway ndio utamaduni wenu labda hapa
 
mmh hiki ni kisa cha pili kuwakumba wachunga kondoo wa bwana kutokea Mkoa wa Dodoma?

Wakristo wa Dodoma simameni kukemea roho hii inayowatafuna watumishi wa bwana!
 
Back
Top Bottom