Uzinduzi Wilaya ya Kigamboni: Rais Magufuli anazindua Jengo la Manispaa na Jengo la Mkuu wa Wilaya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,792
11,952
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, 2020 anazindua Jengo la Manispaa ya Kigamboni na Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni katika Eneo la Gezaulole Kigamboni Jijini Dar es Salaam




1.PNG

Rais Magufuli akikata utepe wa uzinduzi wa Jengo hilo lenye gharama ya Bilioni 5.2

Gharama ya Jengo hilo ni Bilioni 5.2. Mshauri mwelekezi ambaye ni Chuo Kikuu Ardhi analipwa milioni 163 na Mkandaraesi analipwa Bilioni 5.1

Eneo la ofisi lina kubwa wa Mita za Mraba 8,000 lakini eneo lililopendekezwa kuwepo kwa Taasisi zote za Serikali ni Ekari 750. Jengo hilo linaweza kuchukua Watumishi 50 na limeanza kutumika tangu Agosti 30 mwaka 2019

1.jpg

Jengo lililozinduliwa lenye Ofisi ya Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni
Aliyoyaongea Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
Ifikapo mwaka 2030, Jiji la Dar es Salaam litakua miongoni mwa Majiji matano Afrika yatakayokuwa na idadi kubwa ya watu hivyo tuliamua kuongeza wilaya mbili ili kupanua Mamlaka ya Serikali pamoja na kusogeza huduma muhimu kwa wananchi.

Natoa siku saba kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kurudisha umiliki wa ardhi ya Manispaa ya Kigamboni kuwa chini ya Manispaa hii na si Wizara ya Ardhi.

Nataka ndani ya wiki hii wafanyakazi hasa Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wahamie Kigamboni ili iwe rahisi kutoa huduma kwa wananchi, nyumba za NSSF ni nyumba za Serikali hivyo wafanyakazi hawa wakae bure kwa mwaka mmoja.

Natoa agizo kwa TAMISEMI kutafuta shilingi Bil.2 kwa ajili ya kujenga nyumba za watumishi wa wilaya ya Kigamboni ili baada ya muda watoke kwenye nyumba za NSSF na kuhamia kwenye nyumba zao, nyumba hizo zijengwe kwa miezi 6.

Natoa agizo kwa Waziri Mhagama na Mkurugenzi wa NSSF kuwa ndani ya siku 7 wazungumze na mkandarasi kuwa Serikali haipo tayari kumlipa sh. Bil.36 kwani hakuna barabara inayojengwa kilomita moja kwa sh. Bil.6.

Fedha nyingine za Mfuko wa Barabara ambazo zinatolewa na Serikali Kuu zibadilishiwe matumizi ili tenda ya ujenzi wa barabara ya wilayani yenye urefu wa km 78 itangazwe kwa ajili ya kuanza kujengwa hata kwa awamu, na katika miradi mingine ya DMDP itakayokuja wilaya hizi mbili mpya zipewe kipaumbele

Natoa rai kwa wananchi waliojenga na wanaoendelea kujenga mabondeni kuacha mara moja kwani Serikali haitohusika na changamoto zitakazowapata, pia tutumie mvua hizi kufanya shuguli za kiuchumi hasa kilimo ili mvua zitakapoisha tusianze kulalamika njaa.

Aliyoyaongea Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ludigija Ngwilabuzu.
Tunashukuru Serikali kwa kutupatia sh. Bilioni 4.3 kwa ajili ya jengo la Manispaa ya Kigamboni lenye uwezo wa kuchukua watumishi 450.

Tumepokea shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya, majengo yako saba na yote yamekamilika.

Pia tulipatiwa shilingi Milioni 800 kwa ajili ya upanuzi wa vituo viwili vya afya vya Kigamboni na Kimbiji, majengo yamekamilika na huduma zinaendelea kitolewa.

Mwaka 2018/19 kwa upande wa Elimu ya sekondari tulipokea shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na maabara,manispaa hii haikuwa na masomo ya kidato cha 5 na 6,hivi sasa wanafunzi wameanza masomo.

Waliyoyasema viongozi wengine
Kigamboni tuna changamoto ya ujenzi wa kipande cha barabara cha darajani kuja kigamboni hakijakamilishwa,tunaomba utukamilishie suala hili - Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile.

Wananchi wa eneo hili walikuwa wanatembea umbali mrefu kufika kwa mkuu wa wilaya, mkurugenzi na taasisi nyingine, leo hii wananchi wanapata huduma zote sehemu moja - Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri.

Tuna mradi wa umeme wa dege unaotekelezwa kwa shilingi Bilioni 26, mradi wa maji visima 8 wa kimbiji vimekamilika, DAWASA wanajenga tenki kubwa na kusambaza maji kwa kilomita 65 - Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri.

Tume ya uchaguzi imetangaza kuwa kuanzia tarehe 14-20 Februari 2020 uhuishwaji wa daftari la wapiga kura mkoa wa Dar es Salaam utaanza na tutakuwa na vituo 1661 ambapo vimeongezeka vituo vipya 47 - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Nawasihi na kuwaonya kuwa mifuko inayotoka nchi jirani si salama kwani iko chini ya viwango na hailipi kodi hivyo, yoyote atakayekamatwa anahusika na mifuko hiyo atachukuliwa hatua - Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu.
 
Hivi jambo dogo kama hili haiwezekani kuzinduliwa na Waziri tu ?
Viongozi wa Afrika Mashariki wamejaa Nairobi kumuaga mwenzao Daniel Moi sisi wa kwetu kaenda kusikiliza sifa zake kuzindua jengo la wilaya.
Hii ni aibu sana kwa EAC nzima, kweli jirani yetu kafiwa na mmoja ya viongozi walio changia sana kuirudisha EAC na sisi kung'ang'ania kuifanya kazi ambayo hata Jafo anaweza kufanya!
Tumeingia cha kike kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa Afrika Mashariki wamejaa Nairobi kumuaga mwenzao Daniel Moi sisi wa kwetu kaenda kusikiliza sifa zake kuzindua jengo la wilaya.
Hii ni aibu sana kwa EAC nzima, kweli jirani yetu kafiwa na mmoja ya viongozi walio changia sana kuirudisha EAC na sisi kung'ang'ania kuifanya kazi ambayo hata Jafo anaweza kufanya!
Tumeingia cha kike kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Mkapa na Kikwete hujawaona huko Nairobi?
 
Back
Top Bottom